26/06/2025
TRA KILOMBERO YASISITIZA ULIPAJI KODI AWAMU YA PILI KABLA YA JUNE 30 ,MWAKA HUU
Hayo amezunumza Meneja TRA wilaya ya Kilombero Wilfred Makamba wakati akizungumza katika kipindi cha Taswira pambazuko fm iliyopo Ifakara mapema leo June 26,2025
Ambapo amesema ikiwa k**a mfanyabiashara hujalipa kodi awamu ya pili hadi leo ni vema kulipa kwa wakati kabla kufika June 30 mwaka huu ;huku akisisitiza kwa kufanya hivi itasaidia kuepuka faini na adhabu
Hata hivyo ameongeza kuwa ulipaji wa kodi ni faida kwa taifa la Tanzania na kutoa wito kwa jamii kuendelea kulipa kodi kwa uaminifu