
30/04/2025
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha.
TAREHE: 30/04/2025
SOMO: BAADA YA MAOMBI KIRI USHINDI.
Marko 11:24 "Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu."
Ukishamaliza kuomba hakikisha unachoongea kila siku kinakubaliana na kile ulichoomba, k**a uliomba Mungu akuondolee umasikini na ufukara basi kuanzia hapo usiongee kwamba mimi sina hela, la! Bali anza kusema Mungu amenibariki sitakufa masikini, nitajenga nyumba nzuri nitakuwa na Maisha mazuri; ongea yale yanayohusu baraka, usianze kuongea unajua mimi sina fedha au sina hiki wala kile; anza kuongea k**a ulivyoomba, usiongee tena k**a mtu ambaye haelewi nini anataka.
Ukishaomba amini ya kwamba Mungu anasikia na ameshasikia kile ulichoomba. Kuanzia hapo ondoa unyonge ya kwamba hakuna mtu anayekupenda, tambua kuwa yupo aliyekufia anakupenda, hata k**a watu hawakupendi Yesu anakupenda na k**a Yeye anakupenda basi hata watu watakupenda.
Hakikisha unatenda k**a mtu aliyejibiwa maombi, acha kuwaza shida zako waza jinsi unavyokwenda kutumia baraka zako. Anza kuchora kitu au kuumba kitu unachokitaka au namna utakavyotumia zile Baraka ulizoomba.