Janson NewsUpdates

Janson NewsUpdates Publicity

04/04/2026

With Simba SC Tanzania – I'm on a streak! I've been a top fan for 17 months in a row. 🎉

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, mwezi Mei mwaka huu anatarajiwa kufanya ziara nchini Ke...
29/03/2026

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, mwezi Mei mwaka huu anatarajiwa kufanya ziara nchini Kenya ili kukagua maendeleo ya miundombinu ya viwanja na maandalizi ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Michuano hiyo mikubwa barani Afrika inatarajiwa kuandaliwa kwa pamoja na nchi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda, jambo ambalo ni la kihistoria kwa ukanda huo kupata fursa ya kuandaa mashindano ya hadhi ya juu ya CAF.

Motsepe amesema ziara hiyo itampa nafasi ya kujionea hali halisi ya maandalizi, ikiwa ni pamoja na ubora wa viwanja, miundombinu ya usafiri, na huduma za wageni zitakazohitajika wakati wa mashindano.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Cairo nchini Misri, Motsepe amebainisha kuwa CAF imejipanga kuhakikisha AFCON 2027 inakuwa ya kiwango cha kimataifa, huku akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo tatu ni mfano bora wa mshik**ano wa Afrika katika kuendeleza soka.

Aidha, viongozi wa serikali na sekta ya michezo kutoka nchi husika wanatarajiwa kushirikiana kwa karibu na CAF ili kuhakikisha maandalizi yote yanakidhi viwango vinavyotakiwa kimataifa.

CAF PRESS | ‘‘…mechi ya fainali Morocco kati ya Senegal na Morocco, si jambo muhimu sana kwetu kuendelea kulijadili…’’ R...
29/03/2026

CAF PRESS | ‘‘…mechi ya fainali Morocco kati ya Senegal na Morocco, si jambo muhimu sana kwetu kuendelea kulijadili…’’ Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe akizungumza na waandishi wa habari mjini Cairo, Misri.

Motsepe amesema mpira wa miguu ni mchezo wenye hisia kubwa, lakini tukio lililotokea katika fainali kati ya Senegal na Morocco halipaswi kupewa uzito mkubwa wa mijadala kwa sasa.

‘‘Tunachotaka kusisitiza ni kwamba suala hilo tayari liko mbele ya Mahak**a ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), ambayo ni chombo cha juu cha maamuzi katika masuala ya michezo duniani, na sisi tutaheshimu na kutekeleza uamuzi wowote utakaochukuliwa na CAS''.

Ameeleza kuwa CAF haioni umuhimu wa kuendelea kujadili suala hilo hadharani, bali inaelekeza nguvu katika kuheshimu taratibu na mifumo ya kisheria ya michezo.


Iran imesema kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeshambulia vyombo sita vya kijeshi vya Marekani, na kusababisha kuuawa kwa...
29/03/2026

Iran imesema kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeshambulia vyombo sita vya kijeshi vya Marekani, na kusababisha kuuawa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani waliowataja k**a magaidi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa Ijumaa na Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), mashambulizi hayo ni sehemu ya awamu ya 84 ya operesheni iitwayo “Ahadi ya Kweli 4”.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa jeshi la majini la IRGC lilifanya mashambulizi ya usahihi dhidi ya malengo ya Marekani na Israel katika bandari ya Al-Shuwaikh pamoja na fukwe na bandari ya Dubai, likilenga wanajeshi wa Marekani na vifaa vyao vya kijeshi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo ilihusisha matumizi ya makombora ya masafa marefu (ballistic missiles) pamoja na makombora ya cruise aina ya Qadr 380. Vyombo sita vya kutua vikosi (LCU) vya Marekani viliripotiwa kupigwa katika bandari ya Al-Shuwaikh, ambapo vitatu vilizama na vingine vinaendelea kuungua.

Aidha, Iran ilisema ilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo ya kukusanyika wanajeshi wa Marekani, ikiwemo ufukweni na katika moja ya hoteli jijini Dubai, na kwamba malengo hayo yalipigwa kwa usahihi mkubwa.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mbali na kuharibiwa kwa vyombo hivyo vya kijeshi, idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani waliuawa katika operesheni hiyo.

  Wachezaji wa Senegal wamewasilisha Kombe la Mataifa ya Afrika mbele ya maelfu ya mashabiki leo, licha ya uamuzi wa Shi...
29/03/2026

Wachezaji wa Senegal wamewasilisha Kombe la Mataifa ya Afrika mbele ya maelfu ya mashabiki leo, licha ya uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuinyang’anya timu hiyo taji hilo na kulikabidhi kwa Morocco. Kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Peru katika uwanja wa Stade de France, kikosi cha Senegal kilichoongozwa na nahodha Kalidou Koulibaly kiliingia uwanjani na kombe hilo k**a sehemu ya shamrashamra za kabla ya pambano hilo.

Chama cha Soka cha Senegal kilikuwa kimetangaza mapema kuwa kingeliwasilisha kombe kwa mashabiki wake mjini Saint-Denis, Paris jiji lenye idadi kubwa ya raia wenye asili ya Senegal wakati huo timu hio inapinga uamuzi wa ghafla wa CAF wiki iliyopita wa kuinyang’anya ubingwa ilioupata katika fainali yenye vurugu mwezi Januari na kuutangaza Morocco k**a mabingwa wapya. Kwa mujibu wa k**ati ya rufaa ya CAF, Senegal “imetangaza kupoteza fainali” na ushindi wao wa 1-0 katika muda wa nyongeza kubadilishwa kuwa ushindi wa 3-0 kwa Morocco, kwa hoja kwamba wachezaji wa Senegal, wakiongozwa na kocha wao, walitoka nje ya uwanja kupinga penalti, jambo lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika 15.

  news updates
28/03/2026

news updates

28/03/2026

I got over 100 reactions on my posts last week! Thanks everyone for your support! 🎉

Address

Kasulu

Telephone

+255628193183

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Janson NewsUpdates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Janson NewsUpdates:

Share