
13/07/2025
Hatua 10 Jinsi ya Kutengeneza Mtoto anayejiaminina Kujitambua Mbele za watu! Sevu au Share isijepotea!
Kujiamini siyo kitu ambacho mtoto huzaliwa nacho — ni kitu anachojifunza kwa kupitia malezi, mazingira, na uzoefu wa kila siku. Mtoto anayejiamini huwa jasiri kusema mawazo yake, kuuliza maswali, kuonyesha kipaji chake na kujieleza bila woga mbele za watu. K**a mzazi au mlezi, una nafasi kubwa ya kumjenga mtoto wa aina hii.
(1) Hatua ya Kwanza: Mpe Mtoto Nafasi ya Kujieleza
Usimakatishe mtoto kila mara anapoongea. Mruhusu aseme mawazo yake hata k**a si sahihi. Ukimkata mdomo, atahisi mawazo yake hayana maana.
Mfano wa kufanya:
Badala ya kumwambia “Unasema nini sasa, kaa kimya!” sema “Acha tusikilize kidogo unachotaka kusema.”
(2) Hatua ya Pili: Sifia Juhudi Zake — Siyo Matokeo Tu
Watoto wengi huanza kujiona hawawezi kwa sababu wanasifiwa tu wanapofanya vizuri sana. Sifia hata pale anapojitahidi, sio tu akishinda.
Mfano:
“Umejitahidi sana kufanya hiyo kazi ya shule peke yako, najivunia wewe!”
(3) Hatua ya Tatu: Mpe Majukumu Madogo
Mtoto anapopewa kazi ndogo k**a kumkaribisha mgeni, kutangaza kitu shuleni, au kuongoza wenzake kwenye michezo, hujijengea ujasiri na kujiona ana uwezo.
Anza na majukumu ya familia:
• Kumkaribisha mgeni
• Kuombea chakula mezani
• Kusoma aya ya Quran
Au Mstari wa Biblia mbele ya familia
(4) Hatua ya Nne: Mwonyeshe Mifano Hai ya Kujiamini
Watoto hujifunza kwa kuangalia. Ikiwa wewe mwenyewe una aibu kuongea mbele ya watu, kuwasalimia wageni au kuongea hadharani, mtoto wako naye atakuwa hivyo.
Fanya hivi:
• Muonyeshe jinsi ya kusalimia watu kwa kujiamini
• Ongea naye kwa macho
• Mfundishe jinsi ya kutoa “salamu ya nguvu” (firm handshake)
(5) Hatua ya Tano: Usimlinganishe na Wengine
Kauli k**a “Angalia fulani alivyoongea vizuri mbele ya darasa!” huua kabisa hali ya kujiamini kwa mtoto wako.
Badala yake sema:
“Nilifurahia ulivyothubutu kusimama mbele ya watu, kila mtu alianza hivyo kabla ya kuwa mzuri.”
(6) Hatua ya Sita: Mpe Nafasi ya K