Kibaha Yetu Media

Kibaha Yetu Media Habari,Burudani na michezo kibaha yetu

🚨🚨Mohamed Hussein ndiye atakayeongoza parade letu Jumamosi, Afisa Habari wa Young Africans SC, Ally Kamwe, ameendelea ku...
02/07/2026

🚨🚨Mohamed Hussein ndiye atakayeongoza parade letu Jumamosi,

Afisa Habari wa Young Africans SC, Ally Kamwe, ameendelea kuchanja mbuga na utani wa jadi mara baada ya timu yake kutwaa ubingwa, safari hii akimfanyia dhihaka nahodha wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr'. Kamwe amedai kwa utani kuwa Zimbwe Jr ndiye atakayeongoza gwaride lao la ubingwa Jumamosi akiwa juu ya basi la wazi la Yanga, akijumuisha kijembe kuwa mara ya mwisho kwa beki huyo kufanya gwaride la ubingwa alipanda gari la mizigo aina ya kenta.

​Ujumbe wa Ally Kamwe ulisikika hivi: ​"Mohamed Hussein ndiye atakayeongoza parade letu Jumamosi, atakaa juu pale kwenye lile bus la ubingwa. Mara yake ya mwisho kufanya parade alipanda kenta.

​Jana alinionyesha kivideo cha miaka sijui elfu moja mia nane na ngapi huko, yupo kwenye k**enta anachungulia".

🚨Alex Ngereza 🗣️Natamani kuwaona viongozi wa Simba au baadhi ya wachezaji wa Simba waende kumjulia hali Pacome Zouzou ku...
02/07/2026

🚨Alex Ngereza 🗣️Natamani kuwaona viongozi wa Simba au baadhi ya wachezaji wa Simba waende kumjulia hali Pacome Zouzou kutokana na majeraha ambayo amepata

Nimeona Azam Fc wameenda na JKT Tanzania ila pia nimeona mchezaji mmoja wa Dodoma Jiji

This is football, sometimes kwenye matatizo watu waonyeshe ubinadamu

Bila Shaka Yoyote, Eng. Hersi Said, Rais wa YANGA SC ndiye Kiongozi mwenye Mafanikio zaidi kwenye Historia ya Football h...
02/07/2026

Bila Shaka Yoyote, Eng. Hersi Said, Rais wa YANGA SC ndiye Kiongozi mwenye Mafanikio zaidi kwenye Historia ya Football hapa Tanzania.

Katika kipindi cha MIAKA 4 ya Uongozi wake ndani ya Klabu ya YANGA, Eng. Hersi amewaongoza Wananchi, kutwaa Jumla ya MAKOMBE 15 ya Mashindano ya Ndani.

Kwenye Michuano ya CAF, Eng. Hersi ameitoa Klabu ya YANGA Kucheza Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika MARA 3 MFULULIZO. Awali, Hakuna Klabu Tanzania iliyowahi kucheza GROUP STAGE 3 za Ligi ya Mabingwa.

Ilionekana Haiwezekani mpaka Wanayanga walipompa Eng. Hersi kiti cha kuiongoza YANGA yao.

K**a haitoshi, kwenye Kipindi cha MIAKA 4, Eng. Hersi ameipa Yanga heshima ya MEDALI YA CAF kupitia Kombe la Shirikisho Afrika Baada ya YANGA kupoteza mchezo wa Fainali kwa Sheria ya Goli la Ugenini🥈

Huyu ndio Eng. Hersi Said ambaye hata katika Msimu ambayo YANGA ilionekana kuwa chini bado Wananchi wameumaliza kwa kubeba MAKOMBE MANNE🙌🏽

Huyu ndie Role Model wa Viongozi wote wa Soka nchini... Wako “Wenyeviti” wengi tu wanatamani kuiga njia za Eng. Hersi Lakini Shida inakuja kwenye STANDARD.

Wako “Wenyeviti” wanaotamaani kuiga Hotuba zake, Tatizo linakuja kwenye Lugha. Wako wanaotamani kuiga mitupio yake, Tatizo Vitambi vinawaangusha

Na wako “Wenyeviti” wanaotamani kuiga hata anavyonyoa Tatizo vichwa vyao havikai na nywele😀

Kushindana na Eng. Hersi IMESHASHINDIKANA..

Ishi sana President Hersi Said .. WANANCHI WANAKUPENDA SANA🔰🏆🏆🏆🏆🏆

Bado nafuatilia kujua k**a viongozi wa juu wa Simba watafika Hospital ya Agha Kan kumuona mchezaji wa Yanga Pacome Zouzo...
01/07/2026

Bado nafuatilia kujua k**a viongozi wa juu wa Simba watafika Hospital ya Agha Kan kumuona mchezaji wa Yanga Pacome Zouzoua aliyefanyiwa upasuaji baada ya kuumia kwenye mchezo wa jana dhidi ya JKT.

Mpira ni mchezo wa kiungwana sitegemei kuona watani wakiweka upinzani wao mbele kwenye hili, Mpaka sasa tayari viongozi wa Yanga, Azam na JKT wameshafika kumuona pamoja na baadhi ya wachezaji wao.

Tufuatilie Instagram
Facebook
YouTube
TikTok
Tumekuchagua|Tutakuhudumia

Salama Jabir alianza kupenda michezo na kucheza mpira wa miguu na table tennis akiwa bado msichana mdogo. Baadaye aliing...
01/07/2026

Salama Jabir alianza kupenda michezo na kucheza mpira wa miguu na table tennis akiwa bado msichana mdogo. Baadaye aliingia katika tasnia ya utangazaji kupitia Times FM na baadaye East Africa Radio.

Ingawa, katika safari yake ya utangazaji alifanya pia vipindi vya michezo, lakini vipindi vya burudani vilimpa umaarufu zaidi hasa vipindi vya Planet Bongo na Mkasi vilitokea kupendwa na watu wengi alipokuwa akikosoa video za muziki kwa nia ya kuboresha fani hiyo na kufanya mahojiano na watu maarufu kutoka kada mbalimbali.

Mbali na utangazaji, kwa muda mrefu tangu mwaka 2006, Salama amekuwa sehemu ya majaji wa Bongo Star Search(BSS), shindano la kutafuta vipaji.

Amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa watangazaji maarufu wanaopendwa zaidi na ambaye ametoa mchango chanya katika ukuaji wa tasnia ya muziki na burudani Tanzania. Ni miongoni mwa watangazaji wa muda mrefu ambaye hata baada ya ujio wa mitandao ya kijamii, bado ameweza kupata wafuasi wengi mitandaoni.

Msanii wa Bongo Fleva official gachi leo ameachia wimbo wake mpya katika siku ambayo pia Jux na Mbosso wameachia kazi ya...
01/07/2026

Msanii wa Bongo Fleva official gachi leo ameachia wimbo wake mpya katika siku ambayo pia Jux na Mbosso wameachia kazi yao mpya.

Wengi wanaona huu ni mtihani mkubwa kwa msanii anayekuja kwa kasi, huku baadhi ya mashabiki wakimpa jina la "Diamond wa k**e" kutokana na kujiamini kwake na kutorudi nyuma hata anapokutana na majina makubwa sokoni.

Je, ni wimbo upi utakaoteka hisia za mashabiki leo?

Toa maoni yako

Ana zaidi ya miaka 35 tangu awe kwenye sanaa ya muziki. Prince Mwinjuma Muumini amezitumikia bendi mbalimbali za muziki,...
01/07/2026

Ana zaidi ya miaka 35 tangu awe kwenye sanaa ya muziki. Prince Mwinjuma Muumini amezitumikia bendi mbalimbali za muziki, huku miongoni mwa nyimbo zake zilisofanya vizuri zikiww ni pamoja na Tunda, Maisha Kitendawili, Ndugu Lawama na nyinginezo. Anatajwa kuwa miongoni mwa wanamuziki bora wa dansi Tanzania, bado anaendelea na muziki hadi sasa.

Harmonize amesema historia ya Bongofleva haiwezi kukamilika bila kumtaja Alikiba pamoja na lebo yake ya Kings Music. Ame...
01/07/2026

Harmonize amesema historia ya Bongofleva haiwezi kukamilika bila kumtaja Alikiba pamoja na lebo yake ya Kings Music.

Amesema Alikiba kupitia lebo hiyo ameinua vipaji vingi ambavyo vimeweza kushindana na wasanii wa lebo nyingine.

Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfu...
01/07/2026

Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi.

Mojawapo ya tawala ilikuwa ni dola ya wachagga (Chagga state). Dola hiii ilikuwa na Kiongozi Mmoja aliyeitwa Mangi Mkuu

Mangi mkuu aliteua Mamangi wadogo wadogo (RC, DC) mfano Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc.

January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu, Petro Marealle, John Maruma na Thomas Marealle. Thomas Marealle aliibuka Mshindi katika Uchaguzi huo

Turudi nyuma Kidogo, mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya).

Huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi.

Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa miaka hiyo hadi sasa ndio Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya.

Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasi ya maendeleo.

Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo.

Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University.

Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe,

Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala.

Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka 1884/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state' iliyogawanywa.

Shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru kutokana na umahiri wake katika uongozi lakini Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabila mengine nje ya wachagga.

Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake. Nyerere alisema ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine.

Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza.

Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.

Leon Mpasi Golikipa wa timu ya Taifa ya Congo alikuwa bora sana kulinda lango lake dhidi ya England. Nanda huyu amefuta ...
01/07/2026

Leon Mpasi Golikipa wa timu ya Taifa ya Congo alikuwa bora sana kulinda lango lake dhidi ya England.

Nanda huyu amefuta big chances 5 za England ambazo zingeweza kwenda nyavuni.

Congo wanaondoshwa kombe la Dunia ila Leon Mpasi ameonyesha yeye ni Golikipa wa kiwango cha juu.

England wamepata Big chances 7 ila mchawi wao ni Leon Mpasi tuu.

👉NENO MOJA LA FARAJA KWA LEON MPASI ???






Address

Manzizuber818@gmail. Com
Kibaha
MAILIMOJA

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kibaha Yetu Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share