08/09/2025
Mwanamume Alimpiga Mke wake Mbele ya Watoto wake Mpaka watoto wakaingiwa na Fazaa na Khofu..Mama Akahuzunika Sana baada ya Mumewe kumpiga usoni na Kusema Huku analia Nitaenda kukushtaki...
Mume akamjibu:- Nani aliyekuambia kua Nitakuruhusu Utoke?
Mke akasema: Je Unadhani Kua Umefunga milango yote Na madirisha mpaka nisiweze kukushtaki!!?
Mume akajibu kwa mshangao:- Kwani Utafanya Nini!
Mke akasema:- Nitatumia njia ya mawasiliano.
Mume akasema:- Simu zako Zote Niko nazo, Fanya utakalo.
Mke Akaelekea Chooni, Mume akadhani mke atatoroka na dirishani Akatoka nje kusubiria k**a atatoka na dirishani, lakini hakuona lolote akarudi ndani na kusimama mlangoni, Mara Mke akatoka huku akiwa Na maji Kwa athari ya Udhu Akiwa na tabasamu Lake K**a maji yaliyokua yakitona mwilini mwake.
Mke akamwambia mumewe: Nitakushtaki Kwa yule Ambaye Umechukua kiapo kwa Jina lake, Kwani milango yako Na madirisha yako wala simu zangu ulizozishika Haziwezi kunizuia kushtaki, Milango Ya Allah Haifungwi... mume akamuondokea mke wake, kisha akaketi kochini Kimya Anafikiria.
Mke akaenda Kuswali, Na akarefusha sijda, huku Mume anamfuatilia kwa makini, mke alipomaliza swala yake, Na kunyanyua mikono yake anaomba, Mume aliemuendea Na kimshika mikono yake.... Huku akisem: Mke wangu Dua ulizoniombea Ukiwa katika sijda hazikutosha?
Mke akamuangalia kwa jito la mapenzi na huruma kisha akasema: Je Unadhani nitawacha kukuapiza baada ya yote uliyonifanyia?
Mume akasema: Wallahi Ilikua hasira tu sikukusudia, Mke akasema: Na kwa sababu hiyo Mie sikukuapiza Bali nimekuombea dua ya rehma! Na kumlani shetani, Mie Sio mjinga wa Kumuapiza mume wangu, kitulizo cha jicho langu, Mume akaangusha machozi, na kubusu mikono yake, na kusema: Nakuahidi mke wangu kuanzia Leo Sitokugusa Kwa ubaya...
Huyu ndie mwanamke wa Kiislamu ambaye mtume S.A.W Alituusia Juu yake, Basi Kuweni wema kwao Nao watakuwa wema kwenu.
Ukimaliza kusoma andika (Al-Hamdulillah)
🤲🤲🤲🤲