20/06/2025                                                                            
                                    
                                                                            
                                            NAMNA YA KUOMBA UKIWA KWENYE MAJARIBU...
  Somo hili Lina part 2 usikose 
Katika Somo hili kuna mambo kadhaa pia tutayaangalia nayo NI k**a hivi yafuatavyo.........
1Nini maaana ya karibu
2Namna ya Majaribu yanavyo kuja
3Lengo la Majaribu.
Tuanze kabisa kuangalia nini maana ya Majaribu π€
MAJARIBU β‘οΈNi Mtihani wa Imani zetu au ,Ni Kipimo cha Imani zetu 
K**a Mtu unaye mwamini Kristo Majaribu kwako nikwamba huo NI Mtihani wako WA kupima Imani yako katika Yesu ,kuangalia je Kweli wampenda Yesu au waigiza na je Kweli Huwezi kumuacha na kugeukia kungine mfano,Kwa waganga ,miungu NK 
Mfano ,Kwanini shuleni Mwanafunzi hupaswa kupewa Mtihani ? 
Nikwa sababu moja Tu  kumpima k**a Mwanafunzi anaelewa na kile ambacho mwalimu amekuwa akifundisha Kila SIKU na Mwanafunzi Huyo anapo Fanya vizur ,mwalimu hujisikia vizuri,na kusema kwamba hakika Mwanafunzi Huyu alikuwa anasoma na alielewa vyema Somo.
Kwa mtu ambaye amemwamini Kristo kuwa Bwana na Mwokozi WA MAISHA yake nilazima ajaribiwe ,ili ijulikane Huyu mtu amesimamia wapi!, utaona ata watu wengi walio mcha Mungu walipitia Majaribu mbalimabali hiyo ikionyesha kwamba wanapimwa katika Imani zao
SASA EMBU TUANGALIE JINSI MAJARIBU YANAVYO KUJA AU YANAKO TOKA.          (KATIKA SEHEMU TATU 3)
Kwanza kabisa  unatakiwa kuelewa kwamba kuna Aina 3 za Majaribu ambavyo yanakuja Lakin WATU wengi tumekuwa tuki SEMA kwamba Majaribu hayo hutoka moja Kwa moja Kwa shetani ,Lakin Leo Naomba tuangalie HAPA ,,
1οΈβ£MAJARIBU YANA TOKA KWA SHETANI.
Hii ni Njia ya Kwanza ambayo unatakiwa kufahamu kwamba Majaribu hutoka Kwa shetani,na SIKU ZOTE Majaribu yanayo TOKA kwahuyu Shetani sikuzote yanakuja Kwa lengo la kukutenganisha wew na Mungu kuvunja Mahusiano yako kabisa kuharibu mpango WA MUNGU katika MAISHA yako kuharibu Kila KITU 
Mfano NI HAPA Kwa Yesu mwenyewe.
Mathayo 4
3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.
4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Ukisoma Kwa makini Hapo katika MATHAYO 4;1-10 
Utagundua Huyu Shetani analeta jaribu Kwa  Yesu Kristo ILI atakapo kubali na kumsikiliza BASI mpango wa MUNGU kukomboa mwanadamu uharibike,Shetani aliona kwamba Yesu amekuja kuharibu KAZI yake kwahiyo kaamua kwenda kumjaribu ILI aone k**a atambahatisha na KAZI ya ukombozi iishie Hapo.
2οΈβ£MAJARIBU YALETWAYO,AU YASABABISHWAYO NA MWILI WAKO.
Kunamtu atashangaa Sana kwamba inawezekanaje kujaribuwa Kwa mwili wangu?
Lakin Sikia nikwambie ,Kunamajaribu ambayo mwili wako huo ndio husababisha ,na wew USIPO Elewa BASI moja kwamoja unaingia dhambini ,
Mfano ,Unaanzisha Mahusiano wew na Binti/kijana Lakin Muda wa kuona mnaona kabisa bado,mnaanza KUWA na maongezi nyeti yanayo pelekea kuwasha tamaa za miili yenu ,hatimae mnakubaliana na matokeo yake mna sexy ! Je Hapo NI jaribu KUTOKA Kwa shetani au Ni miiliyenu mliyo chochea vitu vya tamaa ?
Yakobo 1
13 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
Naamini Hapo kunakitu umekielewa wew mwenyewe kwamba yawezekana Kabisaaa Majaribu kuletwa na miili yetu tamaa kuwaka ndani yako unatamani kitu usichokuwa na uwezo nacho.
3οΈβ£MAJARIBU YALETWAYO NA MUNGU MWENYEWE.
Mwana wa MUNGU,nataka nikwambie kwamba Mungu humjaribu Mtumishi wake ,na hata wew Mungu anaweza akawa amekujaribu Kwa jaribu furani,Na jaribu analo kusudia Mungu juu ya MTU ANAKUWA anamaana kubwa Sana kwake
Anakuwa na mpango WA kumtoa Hapo na kumpeleka viwango vingine inawezekana Huyo mtu akaumia Sana akalia ,Lakin Mungu anakuwa na kusudi maarumu,
Mfano.
Yusufu kuuzwa utumwani KULIKUWA jaribu la moja Kwa moja KUTOKA Kwa Mungu,MUNGU AKIWA na mpango WA kumpeleka Yusufu ILI akawe waziri mkuu.
Mwanzo 37
5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia;
6 akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota.
7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.
9 Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.
10 Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?
Hiki ndicho kilicho MFANYA ndugu wa Yusufu kumchukia na kumuuza utumwani Lakin kwake Yusufu lilikuwa jaribu kubwa Sana ,Lakin Lilitokea KWAMUNGU ILI amfikishe alipo kusudia
Mwingine NI Huyu 
Mwanzo 22
1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako k**a nyota za mbinguni, na k**a mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Naamini Hapo umeona ,baada ya kushinda huo Mtihani Mungu anaamua kufunguka juu ya Ibrahim Kwa alicho kufanya juu yake
INAWEZEKANA KUNA MAHALI UNAPITIA NA HILO JARIBU K**A NI LA KIMUNGU HUPASWA KULIKEMEA NA KULIKATAA ISIPOKUWA KUNA NAMNA YA KUOMBA ,MAANA UNAWEZA UKAWA UNAPITIA JARIBU AMBALO MBELEN KUNA BARAKA ZAKO NA KUINUKIA KWAKO SASA UTAKAPO LIKEMEA MAANA YAKE HUTAZIONA HIZO BARAKA ,KWAHYO LITAMBUE JARIBU LAKO K**A LATOKANA NA MUNGU AU SHETANI AU MWILI WAKO KISHA UJUWE NI NAMNA GANI YA KULIOMBEA.
K**A UNAHITAJI MAOMBI ,USHAURI ,MAOMBI NK 
NIPIGIE KWA NAMBA HII NAMI NITAKUHUDUMIA 
NIMEPEWA BURE NA NINATOA BURE 
0787 658 269