RADIO BOMA HAI 89.3 Mhz

RADIO BOMA HAI 89.3 Mhz Boma Hai 89.3 FM is a radio station situated at Hai District in Kilimanjaro Region, it is a people's

16/04/2025
HaiNa Olver JoelDiwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani amewataka wakazi wa vijiji vya Kware na Mkombozi kutunza...
08/04/2025

Hai
Na Olver Joel

Diwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani amewataka wakazi wa vijiji vya Kware na Mkombozi kutunza miundombinu ya shule ya sekondari Mkombozi iliyopo katika kijiji cha MKombozi ikiwa ni pamoja na kutunza miti elfu moja iliyopandwa leo shuleni hapo.

Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo waliojitokeza kwa wingi leo kwa ajili ya zoezi la kupanda miti shuleni hapo ,diwani Pangani amesema kuwa shule hiyo ni manufaa kwa wananchi wa masama kusini kwa ujumla na si kijiji cha Mkombozi pekee,hivyo kila mwananchi anapaswa kutunza rmiundombinu ya shule hiyo ikiwa ni pamoja na kutunza miti hiyo lwa kuepuka kupeleka mifugo katika eneo hilo la shule lililopandwa miti.

Naye afisa maliasili wilaya ya Hai John Katikiro amesema kuwa lengo la kupanda miti elfu moja shuleni hapo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kupanda miti katika taasisi za uma pamoja na utunzaji wa mazingira,ambapo pia amewataka wakazi wa Hai kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda miti katika maeneo yao.

Naye katibu wa umoja wa wazazi Ccm Benard Gisunte amesema kuwa wananchi wanapaswa kutunza vyema miundombinu ya shule hiyo ikiwa ni pamoja na kutunza miti hiyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Kware Sebastian Kimaro amesema kuwa atashirikiana vyema na wananchi wake kuhakikisha kuwa wanatunza vyema shule hiyo kwani shule hiyo ni inayoitwa Mkombozi imekuwa mkombozi kwa wanafunzi waliokuwa wanatembea umbali mrefu kwenda katika shule ya sekondari ya mukwasa.

Hai Na James Gasindi.Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai, leo tarehe 4 Aprili 2025, imeshuhudia t...
04/04/2025

Hai

Na James Gasindi.

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai, leo tarehe 4 Aprili 2025, imeshuhudia tukio muhimu la makabidhiano rasmi ya ofisi ya Katibu wa CCM wilayani humo.

Katika hafla hiyo, Katibu aliyemaliza muda wake, Ndg. Ally Ballo, alikabidhi rasmi majukumu kwa Katibu mpya, Ndg. Mkaruka Kura. Ndg. Ballo amehudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu na sasa anastaafu kwa heshima kubwa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, viongozi wa chama wilayani hapa walimpongeza Ndg. Ballo kwa utumishi wake uliotukuka na kumtakia maisha marefu, yenye afya na baraka tele katika kipindi chake cha kustaafu.

Wakati huo huo, Katibu mpya Ndg. Mkaruka Kura alipokelewa kwa shangwe na matumaini makubwa, huku akiahidi kuendeleza misingi ya chama na kushirikiana kikamilifu na viongozi na wanachama katika kuimarisha maendeleo ya CCM Wilaya ya Hai.

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Hai kinamtakia kila la heri Ndg. Mkaruka Kura katika majukumu yake mapya, na kinamkaribisha kwa moyo mkunjufu.

Hai Na James GasindiKatika kuadhimisha Sikukuu ya Idd, Taasisi ya Jami’iyatul Akhlaaqul Islam imeonesha moyo wa upendo k...
31/03/2025

Hai
Na James Gasindi

Katika kuadhimisha Sikukuu ya Idd, Taasisi ya Jami’iyatul Akhlaaqul Islam imeonesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kutoa chakula na vinywaji kwa wagonjwa pamoja na wahudumu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Hai, Sheikh Omary Maamud, alisema lengo la taasisi hiyo ni kushiriki furaha na wale wanaopitia changamoto za kiafya, ili kuwafariji na kuwaombea dua katika kipindi hiki muhimu cha kiimani.

“Sheikh Omary alieleza kuwa taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kutembelea wagonjwa na watu wenye changamoto mbalimbali kila Jumapili, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusaidia jamii. Pia, alibainisha kuwa wanashiriki katika kugharamia matibabu kwa wasio na uwezo na kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji.”

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Bomang’ombe, Mheshimiwa Ivod Njau, aliipongeza taasisi hiyo kwa moyo wao wa kujitolea na kutoa wito kwa jumuiya nyingine pamoja na wananchi kuiga mfano huo mzuri wa kusaidia wenye uhitaji.

Naye Fuya Kimbita, mkazi wa Wilaya ya Hai, alisifu hatua hiyo akisema kuwa kutoa sadaka kwa wagonjwa na wenye uhitaji ni kitendo cha thamani kubwa. Akionesha kuunga mkono juhudi hizo, alichangia shilingi laki moja ili kusaidia shughuli za taasisi hiyo.

Mmoja wa wagonjwa waliopokea msaada huo, Marko Lukas, alieleza furaha yake na kushukuru taasisi kwa upendo waliouonesha. “Nimejiona kuwa si peke yangu kwenye changamoto hii. Upendo huu umenipa faraja kubwa, na naomba Mungu aibariki taasisi hii ili iendelee kusaidia wengine wenye mahitaji,” alisema Marko kwa shukrani.

Taasisi ya Jami’iyatul Akhlaaqul Islam imeendelea kuwa kielelezo cha mshik**ano wa kijamii, ikijikita katika kusaidia makundi yenye uhitaji k**a sehemu ya utekelezaji wa maadili ya kiimani na utu wa kibinadamu.

25/03/2025

Baada ya taarifa potofu inayo sambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya Shule ya msingi Nkweshoo Wilayani Hai kuwa na walimu watatu,ambao Kwa Mujibur wa taarifa hiyo waalimu Hao pia wamendika Barua ya kutaka kuhama kutokana na ubaguzi unaofanywa na wananchi.
Waandishi wetu Elia Sabai na Faraja Ulomi walifuatilia na kuja na taarifa hii hapa.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mukwasa iliyopo katika kata ya Masama Kusini wameishukuru serikali kwa kuwafikishia hudu...
06/02/2025

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mukwasa iliyopo katika kata ya Masama Kusini wameishukuru serikali kwa kuwafikishia huduma ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid.

Wanafunzi hao wametoa shukrani hizo baada ya kupata elimu ya ukatili wa kijinsia na haki kwa watoto iliyotolewa na Timu ya wataalam wa Msaada wa kisheria huku ikiambatana na utoaji wa msaada wa kisheria.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Fransis Hendry amesema elimu hiyo itawasaidia kutambua viashiria vya ukatili na namna ya kutoa taarifa wanapokutana na viashiria vya ukatili wawapo shuleni, nyumbani na maoeneo yoyote.

“napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mama samia Legal Aid kwa kutufikishia elimu ya sheria na tuna amini changamoto zilizo ibuliwa zitapatiwa ufumzuzi, tunakushuru sana mama lakini pia tunaomba utaratibu kwa wanafunzi ambao hawana uwezo waweze kusaidiwa ili waendelee na elimu”

“Sisi k**a wanafunzi tunapaswa kulindana sisi wenyewe kwa kutoa taarifa ya viashiria vya ukatili k**a ambavyo tumefundishwa, na kupitia sisi ukatili utapungua”

Wanafunzi hao pia wameomba wazazi kuwasikiliza na kuwa karibu nao ili kumwekea mtoto mazingira ya kuweza kutoa taaarifa kwa urahisi ya ukatili na changamoto zozote wananzokabiliana nazo.

Kampeni ya Mama Samia Legal Aid inaendelea wilayani Hai kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi walio maeneo ya pembezeni na wasio na uwezo wa kusimamia mashauri yao ikiwa ni pamoja na ardhi,ndoa,miradhi,ukatili,matunzo na mengine mengi.

Hai Na Gasper JosephChama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (Hai Rural Teachers SACCOS) kilichopo Wilaya ya Hai Mkoa wa Ki...
29/12/2024

Hai

Na Gasper Joseph

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (Hai Rural Teachers SACCOS) kilichopo Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, tarehe 28.12. 2024 kimetoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Tzs 4,000,000 (Milioni nne) kwa watoto 100 wenye mahitaji maalumu katika Shule ya St. Francis iliyopo Bomang’ombe Wilaya ya Hai.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Meneja wa HRT SACCOS Bi Upendo Lyatuu amesema vitu walivyokabidhi ni pamoja na majora ya vitambaa kwa ajili ya kushona sare za Wanafunzi, Sabuni, Mafuta ya kupikia, Mchele, Shajala na mahitaji mengine ya muhimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama, Mwalimu Alex J. Warioba amesema chama hicho cha Ushirika kwa sasa kina zaidi ya wanachama 2700 ambapo Chama kilianza na wanachama 67 tu mwaka 2000. Amesema kutoa kwao kwa jamii ni kutekeleza msingi wa saba wa ushirika wa kujali jamii na ni utaratibu ambao Chama kimejiwekea kufanya kila mwaka.

Uongozi wa shule hiyo ya St Francis ya watoto wenye mahitaji maalumu wameshukuru sana uongozi wa SACCOS ya HRT kwa kuwakumbuka watoto hao kwani kwa kufanya hivyo wamesaidia maisha na malezi ya watoto hao wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutimiza ndoto zao. Sister wa watoto hao amesema wana changamoto kubwa ya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kuanzia kidato cha kwanza.

HaiTaasisi ya  Shiri United Sport Academy Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imezindua rasmi bonanza la michezo ambalo ni m...
01/12/2024

Hai

Taasisi ya Shiri United Sport Academy Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imezindua rasmi bonanza la michezo ambalo ni mahususi Kwa ajili wa kuwapata watoto wenye vipaji vya kucheza mpira wa miguu ili kuwajengea uwezo na kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Bonanza Hilo la aina yake limefanyika novemba 30 2024 katika viwanja vya shule ya secondari Mailisita na watoto zaidi ya mia Moja kutoka kata ya Mnadani wamepata fursa ya kushiriki.

Akizungumza kuhusu Shindano hilo lilolopewa jina Nyota Challenge Mwenyekiti wa Shiri United Sports Academy Robert Msemo amesema kuwa lengo la Shindano hilo ni kupata watoto wanaotamani kucheza soka zuri la Kimataifa na kuwapeleka katika Masoko mazuri ndani na nje ya nchi.

"Tumefanikiwa kupata watoto 167 kutoka shule kumi za Msingi Kata ya Mnadani na lengo lilikuwa kupata watoto 60 ila kutokana na uwezo walio onesha tumeamua kuwachukua watoto wote na tutakuwa nao katika mazoezi kwa miezi mitatu hadi sita" amesema Msemo.

Nae afisa utamaduni na michezo Wilaya ya Hai ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shindano hilo Faston Kagimbo amepongeza jitihada za Shiri United Sports Academy kwa kusaka vipaji kwa watoto Nyota Challenge na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwao ili watoto watakao fanikiwa kuingia kambini waweze kutimiza ndoto zao.

"Miundombinu ya michezo Wilaya ya Hai inaboreshwa hasa katika viwanja vya shuleni na vile vya kijamii lengo ni kutengeneza mazingira mazuri ya michezo" amesema Kagimbo

Kwa upande wake Kassim Shaki Afisa wa Azania Benki tawi la Moshi waliodhamini shindano hilo ameeleza kuwa sula la michezo siyo la burudani peke yake bali ni fursa ya ajira kwa vijana,biashara na fursa inayofungua milango mingi ya mafanikio

"Azania Benki tupo kwaajili ya kukuza vipaji vya watu na kuwanyanyua kupitia fursa mbalimbali kupitia sera yetu ya kurudisha kwa jamii hivyo shindano hilo la Nyota Challenge tutalitizama kwa ukaribu ili mafanikio yaonekane kwani tumeweza kushiriki katika ligi ya mkoa wa Kilimanjaro na mafanikio yamefikiwa" amesema Kassimu

Baadhi wa watoto walioshiriki katika bonanza hilo wamesema kuwa wamefurahishwa na kile wanachokifanya Shiri United Sport Academy na kwamba Wana ndoto za kuwa wanamichezo wa kimataifa na wanaamini kupitia taasisi hiyo wataweza kutimiza ndoto zao.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Mhe Edmund Rutaraka Leo Novemba 27,2024 ameshiriki zoezi la kupiga Kura kucha...
27/11/2024

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Hai Mhe Edmund Rutaraka Leo Novemba 27,2024 ameshiriki zoezi la kupiga Kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Rutaraka amepiga Kura katika Kituo cha st Joseph kata ya Muungano.

Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe leo Novemba 27 ,2024 amepiga kura.Mafuwe  ameshiriki zoezi hilo katika kijiji ch...
27/11/2024

Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe leo Novemba 27 ,2024 amepiga kura.

Mafuwe ameshiriki zoezi hilo katika kijiji cha Uduru kata ya Machame Kaskazini ambapo mbali na kushiriki zoezi hilo amewahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura.




Halmashauri ya Wilaya ya Hai leo imetoa mkopo wa shilingi 198,437,000 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulem...
19/11/2024

Halmashauri ya Wilaya ya Hai leo imetoa mkopo wa shilingi 198,437,000 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Katika mkopo huo vikundi 14 vya wanawake wamepewa 139,142,000,vikundi 2 vya vijana 36,211,000 na vikundi 4 vya watu wenye ulemavu 23,084,000.

Address

Bomang'ombe
Kilimanjaro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when RADIO BOMA HAI 89.3 Mhz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to RADIO BOMA HAI 89.3 Mhz:

Share