07/12/2024
STORY: HOUSE GIRL BIBI {10}
NA: ASHROUPH K.A
https://youtu.be/7EKvuOen1rM?si=jVxEt-ZNX5Z5cnJC
Pale pale niliichukua simu yangu na kumpigia mama yangu. Lakini cha kushangaza, alipokea nakuzidi tu kucheka simuni huku akisema,
"Deo, hivi huyo bibi anakupa nini kikubwa hivyo!? Mbona unampenda kupita maelezo! Eenh..! nidanganye tena kuwa haumpendi. Nidanganye, nidanganye tu baba'angu!".
Maneno hayo ya mama yalizidi kunichanganya maradufu. Nikajua kuwa, rafiki yangu Chichi kani double cross. Lazima mama kautumia udhaifu wa Chichi wa kupenda hela, ili tu anibananishe.
Nilikata simu ile niliyokuwa nimempigia mama yangu, kisha nikaipigia simu ya Chichi muda huo huo, nikakuta Chichi akiwa anatumika. Na nilipojaribu tena nikaambiwa namba haipatikani.
Aloo! Nilizidi kuchemkwa na jasho pale kitini nilipokuwa, na ukizingatia msimu huo ulikuwa ni wa joto kali ndani ya jiji la Dar.
Watu walihisi k**a sipo sawa hivi, maana hata macho yangu yalikosa kabisa utulivu. Nikawa na angaza angaza huku na kule k**a mwizi.
Ndipo Patron akaja pale nilipokuwa nimeketi na kuniletea chupa kubwa ya maji ya Kilimanjaro. Huku akisema,
"Kijana, acha presha. Hii ni graduation sio ndoa, mbona una wenge namna hii!?". Nilimtizama kwa jicho kali na kumsonya, maana huyo naye ni wale wale vibaraka wa mama.
Bhasi, sherehe ili pamba moto, japo kwa upande wangu nilitamani ishe mapema ili nikasikie atakacho kisema mama yangu. Japo sitaki kukuficha, awamu hii niliamua iwe, ubaya ubwela. Maana mama mwenyewe haogopi. Siananichimba chimba ili mradi aniharibie penzi langu kwa Bi. Theodora!?
Ngoja nimkomeshe! Deo nilikata shauri.
Bhasi bhana, tulitunzwa zawadi zakutosha sana. Kisha Mgeni rasmi ambaye alikuwa pia ni mbunge na mfanyabiashara mkubwa wa kampuni la kiteknolojia liitwalo R.Z.J mheshimiwa Kombo Abdallah M. Alituhutubia hotuba nzuri sana. Yote kwa yote akituhimiza tuzipambanie ndoto zetu. Wala tusikubali mtu aturudishe nyuma kwa namna yeyote ile.
Wakati hotuba hii ikitolewa, nilibahatika kugonganisha macho yangu na ya mama. Kisha nikanoti jambo fulani kwa mama huyo. Mara moja nikachukua simu na kumtumia mama ujumbe mfupi wa meseji uliosomeka hivi,
"Mama. Sipo tayari uikwamishe ndoto yangu. Nitapambana hadi kieleweke. Theodora ndiye mke wa chaguo la moyo wangu. Mwambie hata baba naye ajue. Sina shida tena na utajiri wenu, wacha nikatesekee pendo langu!".
Wala hakunijibu. Bali alituma tu emoji ya makopa kopa. Nikazidi kuisoma akili yake.
**
Siku hiyo usiku, baba yangu aliwaalika matajiri wenzake wa maeneo yale ya mbezi beach tulipokuwa tukiishi. Kisha akanunua vinywaji k**a kawaida yake. Akataka sote tunywe kwa kusherehekea matokeo yangu. Lakini, wakati tukiwa katikati ya sherehe, nilishangaa kumuona mwanasheria wa baba akiingia nyumbani hapo na makabrasha kibao ya kisheria. Alafu akamsogelea baba na kumnong'onezana jambo la siri sikioni.
Baba akainuka juu na kusema,
"Aidha, nipende kiitumia siku hii ya leo kumsainisha mwanagu Deogratias k**a mrithi namba moja na namba mbili wa mali zangu zote. Hivyo. Deo mali hizi ni zako sasa!". Baba aliongea, nami nikaitwa mbele ya ukumbi huo wa nyumbani. Nikaonyeshwa sehemu ya kusaini na kuweka fingerprint yangu. Mama akabaki tu amepigwa na butwaa, kwani hakutarajia kuwa, baba angelifanya jambo hilo adhimu kwa siku hiyo.
Mchezo ukawa umekwisha. Alama zote tatu nikazikomba mbele ya macho ya mama yangu. Akawa hana la kunambia tena. Maana alishaitambua nguvu yangu kuanzia hapo.
Deo nikawa rasmi tajiri mtoto. Maana baba alinikabidhi utajiri wenye thamani ya zaidi ya shingingi bilioni kumi za kitanzania.
"Ahsante mungu, kilichobaki nikumsaka Theodora wangu. Ili maisha yaendelee maana k**a ni mali tayari ninayo kibindoni", hovi ndivyo nilivyokuwa nikijiwazia kichwani kwangu kila sekunde. Maana sio siri nilikuwa nikimpenda Theodora kupita kiasi, licha ya umri wake ule mkubwa aliokuwa nao....ITAENDELEA
Chimba dawa, safari iendelee.
Pata full story kwa kulipia Tsh 1000/=
Kwenda namba hizi
Kwetu hadithi ni burudani yenye soma zito ndani yake. Karibu tuelimike.
Malenga mwenye kalamu iliyosahaulika nyikani!