05/01/2026
Nikiyatazama maendeleo ya teknolojia naogopa mno
Changamoto ya ukosefu wa ajira itakuwa kubwa zaidi sababu ya kazi nyingi kuchukuliwa na AI..hata kazi za ndani tu Sasa zinachukukiwa na mashine nyingi ndogondogo za kufua, kupika, kufanya usafi n.k SEMBUSE KAZI ZA KITAALAMU ambazo mifuko inaendana nazo zaidi?
Changamoto ya usalama kutokana na kuongezeka kwa zana nyingi zenye kuweza kukata vitu kwa haraka mfano cordless chainsaw, grinder n.k matumizi ya drone yanavuka vizuizi vikubwa.
Kukupa kwa vyakula bandia; vyakula vilivyolazimishwa kukuzwa k**a kuku, matunda mengi k**a vile matikiti, nyanya, mahindi, maparachichi, mbogamboga n.k
Kuongezeka kwa bidhaa feki; teknolojia inarahusisha kunakili(kucopy bidhaa) siku hizi Leo toleo Bora la bidhaa fulanj kesho unakuta toleo lenye muonekano uleule lakini sio halisi.
Elimu bandia; kutakuwa na elimu iliyopatikana mitandaoni lakini ikiwa k**a halisi! Walimu na wanafunzi watategemea sana AI kupata taarifa na maarifa .
Mwisho lakini si kwa umuhimu PICHA, VIDEO NA SAUTI si ushahidi wa uhakika Tena kwa sababu watu wanaweza kubuni.
Nitaendelea kuwakumbusha athari mbaya kabisa ya teknolojia.
Jenerali
Safarini