Vox News Tz

Vox News Tz The Host Elias sasa inapatikana YouTube

ingia YouTube search the host elias kisha subscribe baada bonyeza alama ya kengele ili uw wa kwanza kupata habari kupitia the host elias

18/04/2025
“Kiasi ambacho kimetajwa ni kiasi ambacho tumezingatia mambo mengi k**a klabu. Nipende kuwahakikishia kabla hata hatujaf...
16/04/2025

“Kiasi ambacho kimetajwa ni kiasi ambacho tumezingatia mambo mengi k**a klabu. Nipende kuwahakikishia kabla hata hatujafanya kitu chochote tumeshaweka 30% ya hiki kiasi cha mwaka wa kwanza.”

“Jambo la kwanza ambalo tunakwenda kutekeleza ni kujenga uwanja wa mpira, uwanja ambao utachukua mashabiki 10,000 hadi 12,000 na tumekubaliana kwamba Simba wana uwanja Bunju na tutakwenda kujenga uwanja Bunju lakini k**a watakuja na mapendekezo mengine basi tutayafata.”

“Simba ni timu kubwa Afrika na sisi tumesema kwamba tutanunua basi jipya la Irizar, kila kitu kipo sawa. Muda si mrefu mtaliona hapa. Tutaangalia pia upande wa media, tunakwenda kujenga media kubwa k**a klabu zingine kubwa na tumeshaanza utaratibu.”

“Tunajua kwamba Simba makao makuu yapo Msimbazi lakini tunakwenda kujenga ofisi za kisasa. Lakini pia kila mwaka tutatoa Tsh. 100 milioni ya kusaidia kukuza soka la vijana. Kila mwaka pia tutachangia Tsh. 100 milioni kuchangilia pre season. Pia tumeahidi kujenga kituo maalumu cha matibabu ya wachezaji. Kila mwaka pia tutashiriki bega bega katika Simba Day, tutachangia Tsh. 100 milioni kila mwaka.”- Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Jayrutty Investment Company Limited, CPA Joseph Rwegasira ().

“Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu imewekeza sana kwenye michezo na hasa mchezo huu pendwa wa mpira wa miguu. Ki takwim...
16/04/2025

“Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu imewekeza sana kwenye michezo na hasa mchezo huu pendwa wa mpira wa miguu. Ki takwimu hakuna kipindi tumefanya vizuri k**a kipindi hiki. Mchezo huu unaendelea kutupa raha mioyoni na kututangaza nje ya mipaka ya nchi.”

“Hili nililosikia leo la ujenzi wa uwanja limenivutia sana. Mkiwa na kiwanja cha watu 10,000 au 12,000 kinaweza kutumika kwa michezo ya ndani, michezo ya nje ndio mkawa mnatumia Uwanja wa Mkapa, mtaupunguzia hata majukumu.”

“Itoshe kusema ni uwekezaji wa mkakati ambao umekuja wakati sahihi. Serikali k**a mlezi wetu tunawapongeza sana.”

“Naamini mna maarifa ya kucheza mchezo wa nusu fainali utakaochezwa Zanzibar na kule Afrika Kusini na kuhakikisha mnavuka na kuingia fainali hadi kushinda ubingwa wa Afrika. Na sisi k**a serikali k**a mara zote ambavyo tunawaunga mkono hatutawaacha hata wakati huu. Tupo nyuma yenu kuhakikisha mnashinda ubingwa wa Afrika. Hatuishii Hapa.”- Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vox News Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Vox News Tz:

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share