
03/01/2024
MAKALA AGUSTIN OKRAH USAJILI MPYA YANGA⚽👣
Agustin okrah magic ni midifilder au mido wa mpira Ambae pia anaweza kucheza nafasi ya winga na kuutumi vyema mguu wake wa kushoto
Agustin okrah magic ni mzaliwa wa nchini Ghana ana umri wa miaka 30 akiwa na urefu172cm mghana uyu amekuwa gumzo baada ya kusajiliwa na young African baada ya kuachwa na timu ya Simba sports club na kurudi bechem ya nchini kwao Ghana
Agustin okrah amekuwa na kiwango Bora zaidi kwa msimu uliopita nchini kwao Ghana akitoka na wastan wa mabao 16 kwa nusu msimu ambao ni wastan wa mabao tisa kwa msimu mzima akicheza dk141 akiwa ndie top scorers katika club hiyo
Agustin okrah amecheza vilabu kadhaa vikubwa akianzia maisha ya soka katika club ya rb ya Ghana na kusajiliwa kwa ada ambayo haikuwekwa wazi kwenda asante kotoko ya huko huko Ghana pia amecheza katika club ya al merrikh ya Sudan pamoja na al hilal omrduman ya Sudan pia.
Ikiwa k**a okrah akifanya vizuri YANGA na kurudi katika ubora wake hakuna Ambae hatompenda kwa kuwa ni mcheshi sana k**a walivyo waghana wengi k**a winga wa zamani wa yanga anayekipiga kunako club ya far rabat ya Morocco benard Morrison⚽
Mara kadhaa inasemekana ndugu wawili wakigombana ugomvi uache tu hii ni watani wa jadi yanga na Simba waliibiana au walipeana wachezaji lakini sio kwa furaha ila ni ugomvii mkubwa na huu ndio utani wa jadi itoshe kusema kuwa Agustin okrah ni mchezaji mzurii ila tusubiri muda utaamua
Mimi ni kijana wenu soka letu kitaani KWETU hadi wakati ujao⚽⚽👣