Mafundi Magari

Mafundi Magari Karibu kwenye page hii tushauriane kuhusu Magari kiujumla

Ni page kwaajili ya Mafundi Na Wote Wanaopenda Kufahamu Kuhusu Magari Unaruhusiwa Kusema Chochote Kuhusu Magari Ila Matusi na Picha Zisizofaa Kimaadili Haziruhusiwi

Elimu kiasi ndio tuendelee ... Manual Transmission (MT):Operation: The driver manually shifts gears using a gear stick a...
27/01/2025

Elimu kiasi ndio tuendelee ...

Manual Transmission (MT):
Operation: The driver manually shifts gears using a gear stick and engages/disengages the clutch using a clutch pedal.

Automatic Transmission (AT):
Operation: The transmission automatically shifts gears based on speed and load without any input from the driver.

Continuously Variable Transmission (CVT):
Operation: Uses a belt or chain and pulleys to provide an infinite range of gear ratios, instead of fixed gears.

Intelligent Manual Transmission (iMT):
Operation: A manual transmission without a clutch pedal. The system uses sensors to automatically engage/disengage the clutch when the driver shifts gears.

Dual-Clutch Transmission (DCT):
Operation: Uses two clutches—one for odd-numbered gears and one for even-numbered gears—for faster, smoother gear shifts.

Automated Manual Transmission (AMT):
Operation: A manual transmission with an automated clutch system. It uses actuators and sensors to perform clutch operation and gear shifts.

Regulator (Cut Out)
09/04/2022

Regulator (Cut Out)

High Na Low Gear System
02/03/2022

High Na Low Gear System

Armature Diagram
19/02/2022

Armature Diagram

ELIMU YA MASEGAEXHAUST SYSTEM YA GARI.Huu NI mfumo ambao ni Muhimu Sanaa kwa ajili ya AFYA YAKO na AFYA ya GARI.Mfumo hu...
15/02/2022

ELIMU YA MASEGA

EXHAUST SYSTEM YA GARI.
Huu NI mfumo ambao ni Muhimu Sanaa kwa ajili ya AFYA YAKO na AFYA ya GARI.
Mfumo huu unajihusisha na kazi kuu tatu ambazo ni Muhimu Sanaa kuliko watu wanavyojua, kazi hizo ni K**a zifuatazo hapa chini:-

1️⃣ Mfumo huu ndo unaokusanya gesi chafu na mabaki hatarishi yanayozalishwa na Engine kipindi engine inafanya kazi.

2️⃣ Unatoa nje taka hatari hasa Gesi zenye Sumu zinazozalishwa na Engine.

3️⃣ Inapunguza ukali wa sauti wa Gari yako, ko Mfumo huu ndo SOUND CONTROLLER ya Gari yako.

FAHAMU ZAIDI
Utendaji wa engine unazalisha gesi sita na gesi tatu Kati ya hizo sita ni Sumu hatari kwa Afya yako wewe mtumiaji wa Gari, gesi tatu ambazo ni sumu ni K**a zifuatazo:-
1️⃣ Carbon monoxide
2️⃣ Nitrogen dioxide
3️⃣ Nitrogen monoxide

N:B
Lakini Sumu zote hizi zinazibitiwa na Mfumo tajwa hapo juu Ila ukiwa upo kamili. Bila Shaka ushaanza kupata picha umuhimu wa huu Mfumo kwenye Gari yako na AFYA yako.

NINI HUTOKEA IKIWA EXHAUST SYSTEM HAIPO SAWA.??
K**a umeibiwa masega maanake tayari Mfumo haupo sawa na zifuatazo ndo madhara yake kwa mtumiaji na Gari.

1️⃣ Inapunguza ufanisi wa mafuta na kusababisha Gari kukosa nguvu K**a tatzo litakuwepo kwa muda mrefu kwenye Gari.
2️⃣ Gari itazalisha sauti Kali ambayo ni kero .
3️⃣ Gesi na emissions hatarishi inayozalishwa na engine kusambaa ndani na nje ya Gari na kuathiri Afya za dereva,abiria na watu wanaoizunguuka Gari.
4️⃣ Pia huzalisha harufu mbaya K**a yai lenye kuoza .

SEHEM KUU ZA EXHAUST SYSTEM

1️⃣ EXHAUST MANIFOLD
Hii ndo part inayounga Engine na Exhaust system na kazi yake ni kukusanya Gesi kutoka kwenye kila cylinder ya engine na kuzielekeza kwenye Pipe kuelekea nje kupitia exost pipe.

2️⃣ CATALYTIC CONVERTER
Hiki ndo kibuyu nyeti Sanaa, ndo kina unga unga maarufu K**a MASEGA mengi Sanaa. Hayo MASEGA kitaalamu ndo yanaitwa CATALYST. Mfano wa hizo CATALYST zinazopatikana humo NI:-
➡️ PLATINUM
➡️ PALLADIUM
➡️ RHODIUM

Copied Somewhere

30/01/2022

Canter

Hili Ni Kundi Linalohusu Magari Aina Yote Karibuni Kushare Chochote Kinachohusu Ufundi Tutakapokuwa Wengi Zaidi Tutafung...
22/01/2022

Hili Ni Kundi Linalohusu Magari Aina Yote Karibuni Kushare Chochote Kinachohusu Ufundi Tutakapokuwa Wengi Zaidi Tutafungua WhatsApp Group Kwaajili Ya Kuendelea Kubadilishana Ujuzi Mm Binafsi Ni Fundi Upande Wa Umeme Naomba Kwa Kila Aliyejiunga Kwenye Kundi Tufahamiane Kwa Kutaja Ufundi Wake Na Mahala Anapopatikana Ili Iwe Rahisi Kusaidiana Kikazi

17/03/2021
Diagnosis Machine
14/03/2021

Diagnosis Machine

14/03/2021

MLIPE MTU KUTOKANA NA AINA YA KAZI ALIYOIFANYA SIO UMLIPE MTU KUTOKANA NA MDA ALIOTUMIA KUFANYA HIO KAZI✨

Kulikuwa na meli kubwa (Giant ship) iliyokuwa imekaa tu bila kufanya kazi yaani imekua useless. Tatizo lake kubwa ilikuwa ni Engine , engine iligoma kufanya kazi.

Mmiliki wa hiyo Meli alihitaji Mechanical engineer mwenye uzoefu wa miaka 40.

Engineer alianza kuichunguza engine kwa umakini wa hali ya juu kutoka juu hadi chini, baada ya k*maliza kuikagua akafungua bag la vifaa vyake vya kazi na kutoa kajinyundo kadogo tu.
Akaanza kugonga kajisehemu fulani kwenye hio engine kwa umakini zaidi na ghafla engine ikapata uhai ikarudi kwenye utendaji kazi wake wa zamani. Hivyo tatizo likawa limetatuliwa.

Siku 7 mbeleni baada ya kazi engineer alimuorodheshea mmiliki wa hio meli gharama za utengenezaji wa engine ya hiyo Giant ship, gharama ilikuwa ni dolar $20,000 (Tsh mill ≈45).

"Nini?" Mmiliki wa meli alihamaki kwa kuuliza.
"Kazi aliyoifanya ni sawa na bure tu" naomba unipe mtiririko wa kazi ulivyoenda na malipo yake"

Na jibu lilikuwa ni rahisi tu;
Kutatua tatizo kwa njia ya nyundo 🔨 ni $2.
Kujua sehemu gani ya kugonga na gharama ya ugongaji na nyundo ni $ 19,998.

Kuna umuhimu wa k*m- appreciate mtu kutokana na ujuzi na uzoefu wa kazi anayoifanya.. kwasababu hayo ni matunda ya huyo mtu kustruggle huku akipitia mitihani mbalimbali na hata mda mwingine kutoa machozi.

K**a unafanya kazi kwa dakika 30 hii ni kwasababu ulitumia miaka zaidi ya 20 kujifunza kufanya kazi ngumu kwa dakika hizo 30. Hivyo basi unalipwa kwa hio miaka na sio hizo dakika 30.

NOTE: Hizi ni changamoto wanazokutana nazo mafundi kwenye kazi mbalimbali, inafika mahali watu wanachelewesha kazi ili wasionekane wamewaibia maboss.

Imeandaliwa na Fahamu Magazine
SHARE NA MARAFIKI

10/03/2021
18/02/2021

UFANYE NINI TAIRI LIKIPASUKA (BASTI)??

Kuna hatua 6 za kufuata ndani ya dakika 2 tangu kupasuka tairi ambazo unapaswa kuzifuata.

1. USIHAMAKI wala Kukanyaga Breki, tulia kwanza kwa sababu mara baada ya kupasuka tairi gari lako litaanza kwenda kombo na hivyo utahitajika kulimudu.

2. KAMATA USUKANI Kwa nguvu kwa mikono yote miwili, USIPINDEPINDE KONA huku ukiwa makini na barabara na vioo vya gari lako. Wakati huo soma mwenendo wa gari lako, ambapo mara nyingi litakuwa linakuvuta upande uliopasuka tairi.

3. ONGEZA MWENDO wa wastani ili kudhibiti mwenendo wa gari. Hivyo k**a ulikuwa umekanyaga eksileleta usiondoe mguu haraka kwenye hiyo p**o.

4.ONDOA mguu wako taratibu kwenye eksileleta. USIJARIBU KABISA KUKANYAGA BREKI,Ukijaribu kufanya hivyo utabinuka na gari.

Ilhali k**a usipokanyaga breki gari litapunguza mwendo lenyewe taratibu, wakati wewe ukiwa makini kuangalia watumiaji wengine wa barabara.

5. ONDOA gia zote na uziweke kwenye nyutro huku bado ukiwa umeshikilia vema usukani wako na macho mbele kwenye barabara.

6. Baada ya muda mfupi, kulingana na mwendo wako, gari ikiwa imefika spidi chini ya 60kph, sasa kanyaga breki zako taratibu huku ukisogea kandoni mwa barabara ili usimame.

7. Hatimaye, itakuwa salama zaidi kusimamisha gari lako na kuzima injini.
Hapo utakuwa umeokoa maisha yako na ya abiria wako kutoka kifo.

NYONGEZA: Inapotokea tairi imepasuka ni mara 10 salama kuongeza mwendo kuliko kuhamisha mguu na kukanyaga breki.

Tafadhali, washirikishe na wenzio kwa kusambazai ujumbe huu. Jambo hili linaweza k*mpata mtu yeyote, wakati wowote barabarani.

Imetafsiriwa kwa hisani ya Mutalemwa Blog http://mutalemwa-masgider.blogspot.com

Address

Mabibo
Mabibo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mafundi Magari posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share