26/07/2020
MAIKO 1.
Maiko ni mwanafunzi wa chuo cha Veta Songea akisomea kozi ya umeme wa magari, ni mtoto ambaye hamjui baba ake wala mama ake. Amekuwa akilelewa na mzee Kapinga ambaye alimchukua kwenye kituo cha kulelea watoto yatima peramiho baada ya kumtafuta mtoto wa kiume kwa miaka kadhaa na kushindwa kumpata.
Akiwa na miaka 19 baada ya kumaliza kidato cha nne, London sekondari mzee wake ambaye alikuwa akimlea k**a mwanae alifariki dunia kwa maradhi ya kisukari na ni mwaka mmoja tu baada ya mke wake kufariki. Maisha yalikuwa magumu kwa Maiko ambaye lengo lake la kuwa fundi mkuu wa magari Tanzania yote lilififia.
Dada ake mkubwa, mtoto wa mzee Kapinga aliyeitwa Mage aliyemzidi miaka 15 alijitolea kumlea Maiko kwa sharti la kumtimizia haja zake za kimapenzi,kwa shingo upande Maiko alikubali baada ya maneno ya "mtumikie kafiri upate ujira wako" kupita kichwani mwake.
Maisha yaliendelea hivyo kwa Maiko kufanywa ki ben ten wa Mage, siku moja Maiko akiwa chuo, ulitokea mchango wa Tsh 20000 kwa kila mmoja katika kundi lao ilivwaweze kukamilisha kuitengeneza video iliyokuwa ikielezea namna mfumo wa umeme wa gari aina ya Voxwagen k**a group assignment. Kwa kuwa hakuwa na pesa aliona aikope kwa mwanachuo mwenzie aliyeitwa Clara. Clara alikubali kwa sharti la kulipwa baada ya mwezi mmoja.
Aliporudi nyumbani alimkuta Mage amesharudi kutoka kazini kwake, Mage alikasirika sana kuona Maiko amechelewa kurudi kutoka chuo. Alimnunia bila kujua nini kilikuwa kimetokea chuo. Namna ambavyo Maiko alijaribu kueleza kwa nini amechelewa ndivyo Mage alikasirishwa zaidi.
Siku chache mbele Maiko alimwomba Mage hela kwa ajili ya Matumizi binafsi na kulipa deni kwa Clara. Mage hakujibu chochote na kuwasha gari lake na kuondoka kuelekea kazini kwake. Haikuwa shida sana kwa Maiko kwani alizoea hali ile japo aliona k**a dharau zinazidi kuongezeka. Aliondoka na kuelekea chuoni akitembea kutoka Ruhuwiko mpaka msamala Veta. Alifika kwakuchoka sana huku nguo zake ambazo alikuwa hazibadilishwi na kuu kuu zikibeba vumbi lote la bombambili na matarawe.
Siku moja aliamka mapema na kujaribu tena kuomba pesa za matumizi kwa Mage. Mage aliingia ndani na kutokana kiadi cha shillingi laki mbili. Akiwa anampa alimtamkia maneno kuntu " we mbwa, nakupa hizi pesa,kahonge malaya wako, nikigundua utamfukua mama ako kaburini, huna shukrani hata kidogo, kunguru gani usiyefugika wewe? Alipojaribu kumjibu kwa kushukuru alichapwa kibao ambacho kilimfanya asione mbele, alipepesuka akiwa ameshika zile hela na hatimaye akili ilirudi. Alipoangalia alimuona mage akitoka getini kuelekea kazini kwake.
Kiukweli Maiko aliumia na aliamua kuziacha zile pesa pale pale, aliondoka kuelekea chuo huku akiwaza na kulaani kwa nini hakuwahi kumuona mama ake wala baba ake. Alipokaribia chuo alimuona Clara akinunua chipsi kwa Mudi ambaye alikuwa mchoma chipsi jirani na chuo. Clara alipomuona tu, alimfuata na kumkumbusha hela yake kwa masauti makali. "Nipe hela yangu"
Nitaendelea.....