Habari za Zanzibar

Habari za Zanzibar Ukurasa utakaokupa habari mbalimbali kutoka Zanzibar na Ulimwenguni kote.

๐——๐—ž๐—ง. ๐— ๐—ช๐—œ๐—š๐—จ๐—Ÿ๐—จ ๐—”๐—ž๐—จ๐—ง๐—”๐—ก๐—” ๐—ก๐—” ๐—ช๐—”๐— ๐—œ๐—Ÿ๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ช๐—” ๐— ๐—”๐—•๐—”๐—ฆ๐—œ ๐—ก๐—–๐—›๐—œ๐—ก๐—œ.Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya mazungumzo na viongozi wa C...
18/09/2026

๐——๐—ž๐—ง. ๐— ๐—ช๐—œ๐—š๐—จ๐—Ÿ๐—จ ๐—”๐—ž๐—จ๐—ง๐—”๐—ก๐—” ๐—ก๐—” ๐—ช๐—”๐— ๐—œ๐—Ÿ๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ช๐—” ๐— ๐—”๐—•๐—”๐—ฆ๐—œ ๐—ก๐—–๐—›๐—œ๐—ก๐—œ.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amefanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA). Kikao hicho kimefanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam leo Septemba 18, 2026.

Tarehe 16 Septemba 2026 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi alitembel...
18/09/2026

Tarehe 16 Septemba 2026 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi alitembelea Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Vienna. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Makamu wa Rais alisaini kitabu cha wageni, kupitishwa kwenye Ofisi za watumishi wa Ubalozi, na kuzungumza na maafisa Ubalozi.

Ziara ya Mheshimiwa Makamu wa Rais imefanyika pembezoni mwa Jukwaa la Kisayansi la Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (The IAEA Scientific Forum) lililofanyika tarehe 15 & 16 Septemba 2026 jijini Vienna ambapo Mheshimiwa Makamu wa Rais alimwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliambatana na Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na wasaidizi wake.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alipokelewa na Mheshimiwa Naimi S.H. Aziz, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Vienna na maafisa Ubalozi.

Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alimwakil...
18/09/2026

Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alimwakilisha Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi kwenye mazungumzo na Dkt. Abudlhamid Alkhalifa, Rais wa Mfuko wa Maendeleo wa OPEC yaliyofanyika tarehe 16 Septemba 2026 Makao Makuu ya Mfuko.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Waziri alimshukuru Dkt. Alkhalifa kwa kuidhinisha miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kwa mikopo na misaada kutoka Mfuko wa OPEC.

Mheshimiwa Balozi Kombo alithibitisha dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na Mfuko katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kipaumbele ikiwemo nishati hususan nishati safi ya kupikia, miundombinu ya usafirishaji, afya, elimu na kilimo.

Dkt. Alkhalifa alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuletea maendeleo wananchi kupitia miradi mbalimbali ya kipaumbele.

Aidha, aliahidi kwa niaba ya Mfuko kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo Kati ya Tanzania na Mfuko wa OPEC na kuifanya Tanzania kielelezo cha ushirikiano wa mfano barani Afrika.

Kwenye mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Kombo aliambatana na Mhe. Saada Salum Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb.), Waziri wa Elimu, Sayansi na Taknolojia; Mhandisi Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Taknolojia, na Bw. Rished Bade, Kamishna wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha.

17/09/2026

๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐— ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—”๐—ช๐—”๐—ง๐—”๐—ž๐—” ๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐— ๐—œ๐—ฃ๐—”๐—ก๐—š๐—ข ๐—ž๐—จ๐—ช๐—” ๐—–๐—›๐—”๐—–๐—›๐—จ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—”๐—š๐—˜๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—œ๐—จ๐—–๐—›๐—จ๐— ๐—œ ๐—ก๐—” ๐—จ๐—ง๐—˜๐—ž๐—˜๐—Ÿ๐—˜๐—ญ๐—”๐—๐—œ ๐—ช๐—” ๐——๐—œ๐—ฅ๐—” ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฑ๐Ÿฌ

โ–ช๏ธ๐—”๐˜€๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฑ๐—ผ ๐—ธ๐˜‚๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฒ๐—ป๐—ฒ๐—ผ ๐—น๐—ฎ ๐˜๐—ฎ๐˜๐—ต๐—บ๐—ถ๐—ป๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—น๐—ถ๐—ฎ๐—ท๐—ถ.

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wanamipango, wachumi, na watendaji wote wa serikali kuongoza mageuzi ya kiuchumi kupitia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2026/27โ€“2030/31).

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 17, 2026) alipokuwa akifungua na kuhitimisha Kongamano la Wanamipango Tanzania lililofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha, ambapo Waziri Mkuu amesisitiza kuwa kupitia utekelezaji wa Dira 2050 taifa limeingia katika awamu mpya ya utendaji kazi inayohitaji kasi, ujasiri, na utendaji wa "business unusual" (akimaanisha kufanya kazi bila mazoea) ili kufikia malengo yaliyowekwa.

"Tanzania imeanza rasmi utekelezaji wa Dira 2050 Julai Mosi, 2026, katika uzinduzi uliofanyika Julai 17. Lengo kuu ni kuijenga nchi kuwa na uchumi wenye thamani ya dola za Kimarekani trilioni moja na pato la mtu mmoja mmoja la dola 7,000 kwa mwaka ifikapo 2050."

"Ili kufikia matokeo hayo, lazima tufanye kazi kwa kasi, tuache mazoea na tubadili mtazamo hasi uliojengeka dhidi ya sekta binafsi kwamba wao sio wazalendo, wakati utekelezaji wa Dira 2050 unaitegemea sekta binafsi kwa asilimia 70," amesema Dkt. Mwigulu.

Ili kuchochea uwekezaji na ajira, Waziri Mkuu ameongeza msisitizo kwa kutoa wito wa kuipatia sekta binafsi heshima na fursa sawa na sekta ya umma ambapo amewataka wanamipango kutumia tafiti na taarifa sahihi kuingia kwenye mikataba ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) bila hofu.

Dkt. Mwigulu amewataka watendaji hao kuisaidia Serikali kujitegemea na kupanua wigo wa mapato ambapo amesema kutokana na kubadilika kwa mfumo wa rasilimali za kimataifa na kupungua kwa misaada na mikopo nafuu, kuna umuhimu wa nchi kupanua wigo wake wa mapato ya ndani na kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Mfumo wa Kodi ili kuongeza kujitegemea.

Aidha, amewahimiza wanamipango na watendaji wa Serikali kuoanisha Sera, Mipango, na Bajeti ili kuhakikisha miradi yote ya kielelezo inakamilika kwa wakati, kwa bajeti iliyopangwa, na kwa viwango vinavyotakiwa, huku wakiepuka kubadili mipango kiholela au kuongozwa na dharura.

"Ninakumbuka nikiwa Waziri wa Fedha, wizara zinapitishiwa bajeti wakati wa Bunge la bajeti, lakini ndani ya mwezi Julai tu wizara zinakuja kuomba kubadili vipaumbele kwa kuwa mambo wanayopaswa kuyafanya hayamo kwenye bajeti waliyoiomba na kupitishiwa na Bunge," amesisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amewataka wataalamu wa tathmini na ufuatiliaji kutobaki na ujuzi/mifumo peke yao, bali watoke na kwenda kusimamia na kufuatilia mipango na utekelezaji wa miradi kwa ujasiri katika ngazi zote, mikoa, wilaya, na halmashauri ili kuzuia dharura na matumizi mabaya ya rasilimali.

"Moja ya eneo ambalo bado hatujafanya vizuri ni hili la tathmini na ufuatiliaji. Kwenye hili, bado tuna kazi ya kufanya. Ufuatiliaji lazima ujikite katika kuhakikisha miradi ya kielelezo na mipango yote iliyowekwa inaleta matokeo yenye tija, inakamilika kwa wakati, na inazingatia bajeti pamoja na viwango vilivyopangwa," amehimiza Waziri Mkuu.

Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, alibainisha kuwa makongamano yajayo hayatakuwa tena ya kujadili mipango pekee, bali itajikita katika kutoa taarifa za matokeo halisi ya utekelezaji kwani Serikali imewezesha upatikanaji wa nyenzo zote za kisheria na kimkakati kwa wakati ili kuongoza nchi kwa miaka 25 ijayo.

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amesema kongamano hilo ambalo ni la pili tangu kuundwa upya kwa Tume ya Taifa ya Mipango mwaka 2023, limewakutanisha zaidi ya washiriki 1,300 kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara. Washiriki hao ni pamoja na wachumi, wataalamu wa takwimu, maafisa mipango, watafiti, watendaji kutoka wizara, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo, lengo likiwa ni kujenga jukwaa la kubadilishana uzoefu na kuimarisha mipango jumuishi.

17/09/2026

Moja ya eneo ambalo bado hatujafanya vizuri ni hili la tathmini na ufuatiliaji. Kwenye hili, bado tuna kazi ya kufanya. Ufuatiliaji lazima ujikite katika kuhakikisha miradi ya kielelezo na mipango yote iliyowekwa inaleta matokeo yenye tija, inakamilika kwa wakati, na inazingatia bajeti pamoja na viwango vilivyopangwa - Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua na kuhitimisha Kongamano la Wanamipango Tanzania lililofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.

๐Ÿ“Arusha - Tanzania.
๐Ÿ“… Septemba 17, 2026.

17/09/2026

Ili kufikia matokeo hayo, lazima tufanye kazi kwa kasi, tuache mazoea na tubadili mtazamo hasi uliojengeka dhidi ya sekta binafsi kwamba wao sio wazalendo, wakati utekelezaji wa Dira 2050 unaitegemea sekta binafsi kwa asilimia 70 - Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua na kuhitimisha Kongamano la Wanamipango Tanzania lililofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.

๐Ÿ“Arusha - Tanzania.
๐Ÿ“… Septemba 17, 2026.

๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐— ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—”๐—ž๐—จ๐—ง๐—”๐—ก๐—” ๐—ก๐—” ๐—ฅ๐—”๐—œ๐—ฆ ๐—ช๐—” ๐—–๐—”๐—™Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 17, 2026 amefanya mazungumzo na Rais w...
17/09/2026

๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐— ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—”๐—ž๐—จ๐—ง๐—”๐—ก๐—” ๐—ก๐—” ๐—ฅ๐—”๐—œ๐—ฆ ๐—ช๐—” ๐—–๐—”๐—™

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 17, 2026 amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐— ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—”๐—ช๐—”๐—ง๐—”๐—ž๐—” ๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐— ๐—œ๐—ฃ๐—”๐—ก๐—š๐—ข ๐—ž๐—จ๐—ช๐—” ๐—–๐—›๐—”๐—–๐—›๐—จ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—”๐—š๐—˜๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—œ๐—จ๐—–๐—›๐—จ๐— ๐—œ ๐—ก๐—” ๐—จ๐—ง๐—˜๐—ž๐—˜๐—Ÿ๐—˜๐—ญ๐—”๐—๐—œ ๐—ช๐—” ๐——๐—œ๐—ฅ๐—” ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฑ๐Ÿฌโ–ช๏ธ๐—”๐˜€๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฑ๐—ผ ๐—ธ๐˜‚๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ...
17/09/2026

๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐— ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—”๐—ช๐—”๐—ง๐—”๐—ž๐—” ๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐— ๐—œ๐—ฃ๐—”๐—ก๐—š๐—ข ๐—ž๐—จ๐—ช๐—” ๐—–๐—›๐—”๐—–๐—›๐—จ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—”๐—š๐—˜๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—œ๐—จ๐—–๐—›๐—จ๐— ๐—œ ๐—ก๐—” ๐—จ๐—ง๐—˜๐—ž๐—˜๐—Ÿ๐—˜๐—ญ๐—”๐—๐—œ ๐—ช๐—” ๐——๐—œ๐—ฅ๐—” ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฑ๐Ÿฌ

โ–ช๏ธ๐—”๐˜€๐—ฒ๐—บ๐—ฎ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฑ๐—ผ ๐—ธ๐˜‚๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜‡๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฒ๐—ป๐—ฒ๐—ผ ๐—น๐—ฎ ๐˜๐—ฎ๐˜๐—ต๐—บ๐—ถ๐—ป๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—น๐—ถ๐—ฎ๐—ท๐—ถ.

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wanamipango, wachumi, na watendaji wote wa serikali kuongoza mageuzi ya kiuchumi kupitia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2026/27โ€“2030/31).

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 17, 2026) alipokuwa akifungua na kuhitimisha Kongamano la Wanamipango Tanzania lililofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha, ambapo Waziri Mkuu amesisitiza kuwa kupitia utekelezaji wa Dira 2050 taifa limeingia katika awamu mpya ya utendaji kazi inayohitaji kasi, ujasiri, na utendaji wa "business unusual" (akimaanisha kufanya kazi bila mazoea) ili kufikia malengo yaliyowekwa.

"Tanzania imeanza rasmi utekelezaji wa Dira 2050 Julai Mosi, 2026, katika uzinduzi uliofanyika Julai 17. Lengo kuu ni kuijenga nchi kuwa na uchumi wenye thamani ya dola za Kimarekani trilioni moja na pato la mtu mmoja mmoja la dola 7,000 kwa mwaka ifikapo 2050."

"Ili kufikia matokeo hayo, lazima tufanye kazi kwa kasi, tuache mazoea na tubadili mtazamo hasi uliojengeka dhidi ya sekta binafsi kwamba wao sio wazalendo, wakati utekelezaji wa Dira 2050 unaitegemea sekta binafsi kwa asilimia 70," amesema Dkt. Mwigulu.

Ili kuchochea uwekezaji na ajira, Waziri Mkuu ameongeza msisitizo kwa kutoa wito wa kuipatia sekta binafsi heshima na fursa sawa na sekta ya umma ambapo amewataka wanamipango kutumia tafiti na taarifa sahihi kuingia kwenye mikataba ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) bila hofu.

Dkt. Mwigulu amewataka watendaji hao kuisaidia Serikali kujitegemea na kupanua wigo wa mapato ambapo amesema kutokana na kubadilika kwa mfumo wa rasilimali za kimataifa na kupungua kwa misaada na mikopo nafuu, kuna umuhimu wa nchi kupanua wigo wake wa mapato ya ndani na kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Mfumo wa Kodi ili kuongeza kujitegemea.

Aidha, amewahimiza wanamipango na watendaji wa Serikali kuoanisha Sera, Mipango, na Bajeti ili kuhakikisha miradi yote ya kielelezo inakamilika kwa wakati, kwa bajeti iliyopangwa, na kwa viwango vinavyotakiwa, huku wakiepuka kubadili mipango kiholela au kuongozwa na dharura.

"Ninakumbuka nikiwa Waziri wa Fedha, wizara zinapitishiwa bajeti wakati wa Bunge la bajeti, lakini ndani ya mwezi Julai tu wizara zinakuja kuomba kubadili vipaumbele kwa kuwa mambo wanayopaswa kuyafanya hayamo kwenye bajeti waliyoiomba na kupitishiwa na Bunge," amesisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amewataka wataalamu wa tathmini na ufuatiliaji kutobaki na ujuzi/mifumo peke yao, bali watoke na kwenda kusimamia na kufuatilia mipango na utekelezaji wa miradi kwa ujasiri katika ngazi zote, mikoa, wilaya, na halmashauri ili kuzuia dharura na matumizi mabaya ya rasilimali.

"Moja ya eneo ambalo bado hatujafanya vizuri ni hili la tathmini na ufuatiliaji. Kwenye hili, bado tuna kazi ya kufanya. Ufuatiliaji lazima ujikite katika kuhakikisha miradi ya kielelezo na mipango yote iliyowekwa inaleta matokeo yenye tija, inakamilika kwa wakati, na inazingatia bajeti pamoja na viwango vilivyopangwa," amehimiza Waziri Mkuu.

Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, alibainisha kuwa makongamano yajayo hayatakuwa tena ya kujadili mipango pekee, bali itajikita katika kutoa taarifa za matokeo halisi ya utekelezaji kwani Serikali imewezesha upatikanaji wa nyenzo zote za kisheria na kimkakati kwa wakati ili kuongoza nchi kwa miaka 25 ijayo.

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amesema kongamano hilo ambalo ni la pili tangu kuundwa upya kwa Tume ya Taifa ya Mipango mwaka 2023, limewakutanisha zaidi ya washiriki 1,300 kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara. Washiriki hao ni pamoja na wachumi, wataalamu wa takwimu, maafisa mipango, watafiti, watendaji kutoka wizara, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo, lengo likiwa ni kujenga jukwaa la kubadilishana uzoefu na kuimarisha mipango jumuishi.

16/09/2026

Kitambulisho chenyewe k**a nchi tumeingia gharama, tumeahirisha baadhi ya shughuli za maendeleo ili tutoe vitambulisho. Lakini tunapokuwa tumetoa kitambulisho, halafu mhusika haendi kuchukua, haya ni mambo ambayo yanakwamisha malengo mapana - Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba.

Amesema hayo wakati akiwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Utambulisho Duniani, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

๐Ÿ“Dar es Salaam - Tanzania.
๐Ÿ—“๏ธSeptemba 16, 2026.

๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐— ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—”๐—ช๐—”๐—ฆ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—”๐—ฅ๐—จ๐—ฆ๐—›๐—”, ๐—ž๐—จ๐—™๐—จ๐—ก๐—š๐—จ๐—” ๐—ž๐—ข๐—ก๐—š๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—Ÿ๐—” ๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐— ๐—œ๐—ฃ๐—”๐—ก๐—š๐—ขWaziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili mkoani Arusha ...
16/09/2026

๐—ช๐—”๐—ญ๐—œ๐—ฅ๐—œ ๐— ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—”๐—ช๐—”๐—ฆ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—”๐—ฅ๐—จ๐—ฆ๐—›๐—”, ๐—ž๐—จ๐—™๐—จ๐—ก๐—š๐—จ๐—” ๐—ž๐—ข๐—ก๐—š๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—Ÿ๐—” ๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐— ๐—œ๐—ฃ๐—”๐—ก๐—š๐—ข

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili mkoani Arusha leo Jumatano, Septemba 16, 2026, ambapo amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.

Dkt. Mwigulu yupo mkoani Arusha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kikazi, ikiwemo kufungua rasmi Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, litakalofanyika kesho Alhamisi, Septemba 17, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Address

Bagamoyo
61305

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari za Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share