19/02/2025
Tafakuri za Mc Charles Turuka ✍️✍️✍️
Katika Maisha Haya,Kuna watu Wema K**a Dada Yangu Mariam Mbano na Yusuph Pangoma na wengine Wengi MmAmbao Pengine Sujawataja hapa...
Watu Ambao Furaha yao ndiyo chanzo cha furaha ya watu Wengine na Chozi lao ni Chozi la Watu Wengine pia yaweza Kuwa Familia,Jamii au hata Watu Wengine...
Watu Ambao Wao hata Wakiwa Na Maumivu Makali namna gani,Watayaficha na Kuyavumilia mioyoni mwao ili Kuilinda Furaha ya Wale wanaoitegemea Furaha Yake,Hata K**a Atapitia Ugumu kiasi gani bado Ataonyesha Yuko Sawa Ili Kuilinda Amani na Furaha ya Wale wanaomtegemea!!
Ni watu ambao wapo Tayari Kuitega Migongo Yao K**a Ngao Ya wengine,Wapo tayari Kupokea Mishale katika Migongo au Kifua chao ili Kuwakinga Wengine wasipate Maumivu ya Shambulio.
K**a wewe Ni Mtu wa Namna Hiyo!
Mungu Mwema Akutunze sana na Awe Upande wako Nyakati zote Kwani watu wa namna hii,Mara Nyingi Huwa Shujaa wa Familia zao na Huwa hawana wa Kuwatetea au Kusimama Upande wao🙏🙏
K**a Uko Hapa Mungu Asikusahau Hata Mara Moja.
Amen🙏
Wakti Mwema🙏
Follow Charles Sylvester Marwa