Gademittv

Gademittv ๐ŸšฆMatukio Yote Ya Barabarani ๐Ÿšฆ
Interviews ๐ŸŽ™| Simulizi & Mikasa ๐Ÿ“–
๐Ÿ’ฅ ROADLIFE ๐Ÿ’ฅ EXPERIENCE ๐Ÿ’ฅ
Please Subscribe Our Channel๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://www.youtube.com/

26/08/2026

Wadau mbali mbali wa roadlife watoa pongezi zao

26/08/2026

Maono ya madereva mbali mbali kuhusu afande marcus wa kitonga wakati wa hafra ya utoaji pongezi

20/08/2026

Prophet IPM azua gumzo baada ya kuonekana akibeba bia ukweni
Prophet IPM, mtumishi wa Mungu anayefahamika kwa umaarufu wake mitandaoni, ameibua gumzo baada ya kusambaa kwa video inayomuonyesha akiwa amebeba kreti ya bia katika eneo linalodaiwa kuwa ni ukweni kwake.
Katika video hiyo, IPM anaonekana akiwa ameshika kreti ya bia huku akieleza kuwa alipokuwa ukweni, baba mkwe wake alimuelekeza kubeba bia hizo na kuzipeleka ndani kwa ajili ya wageni.
Kauli hiyo imeibua mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wakijiuliza kuhusu nafasi ya mtumishi wa Mungu katika mazingira k**a hayo, wakati wengine wakiona kuwa kitendo cha kubeba bia hakimaanishi kwamba alikuwa akinywa.
Video hiyo imeendelea kusambaa kwa kasi na kuvuta maoni ya watu, huku jina la Prophet IPM likitajwa zaidi kutokana na tukio hilo lililoonekana kuwa tofauti na taswira ambayo baadhi ya watu wameizoea kwa watumishi wa dini.
Kwa upande wake, IPM ameonekana kulieleza tukio hilo k**a jukumu alilopewa akiwa ukweni, akisisitiza kuwa alipewa mzigo huo na baba mkwe wake.

08/08/2026

Ila majirani๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ

08/08/2026

Sio chai

07/08/2026

Ila upako๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†

06/08/2026

Mkubwa wa kazi kazini๐Ÿซก

04/08/2026

Fainali za michuano ya Likunja Cup zimehitimishwa Kibaha Zegereni Mkoani Pwani..ambapo mshindi wa kombe hilo kwa mwaka 2025-2026 ni timu ya Maili city iliyoibuka kidedea kwa Gori 1 dhidi ya 0 emirates Fc.akihitimisha fainali hizo ndg Rashidi Likunja ambae ni mwenyekiti wa mtaa wa zegereni lakini pia mwasisi wa kombe hilo ambalo ni msimu wa 11 tangu kuanzishwa kwake amesema amepokea maoni mbali mbali na ataendelea kuyafanyia kazi kwajili ya michuano ijayo kwani kombe hili hufanyika mara moja kwa kwa mwaka.

03/08/2026

UWANJANI, MAILI CITY FC YATWAA UBINGWA
Timu ya Maili City FC imeibuka mabingwa wa michuano ya Likunja Cup 2026 baada ya kuichapa Emirates FC kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa Zegereni, Kibaha mkoani Pwani.
Kabla ya pambano hilo, meneja wa Emirates FC alikuwa akizungumza kwa kujiamini na kujitamba kuhusu uwezo wa kikosi chake, akisisitiza kuwa timu yake ilikuwa imejipanga kikamilifu kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Hata hivyo, mambo yalikuwa tofauti mara tu mchezo ulipoanza. Maili City FC ilionyesha nidhamu, utulivu na ubora mkubwa uwanjani, na kufanikiwa kupata bao pekee lililoamua hatima ya fainali hiyo.
Licha ya tambo zote zilizotolewa kabla ya mchezo, Emirates FC ilishindwa kutimiza matarajio yake na kulazimika kukubali kipigo cha bao 1-0, huku Maili City FC ikitwaa rasmi taji la Likunja Cup kwa mwaka 2026.
Matokeo ya mwisho (Full Time):
Maili City FC 1-0 Emirates FC

03/08/2026

Hii ipoje?

Address

Dar Es Salaam
Masaki
0000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Gademittv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share