
26/07/2025
TANZIA: MZEE DAUDI WALUGANO MWANJA AFARIKI DUNIA
Njiwa Media tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mzee Daudi Walugano Mwanja, ambaye ni Baba Mkwe wa Askofu Kenan Salim Panja wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini (KMT-JK).
Mzee Daudi Mwanja hakuwa tu mkwe wa Baba Askofu Panja, bali pia ni mzazi wa Mchungaji George Mwanja anayehudumu katika Ushirika wa Katumba, Jimbo la Kusini.
Taarifa za awali kuhusu msiba huu zimetolewa na mmoja wa wanafamilia wa karibu, na kwa jitihada za kumpata Makamu Mwenyekiti KMT-JK, Mch. Jair Sengo zimefanyika, ambapo amethibitisha kutokea msiba huu na kwamba Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Jumatatu 28/07/2025 huko Kijiji cha Ibungu Wilaya ya Ileje.
Njiwa Media inaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa za msiba huu, na itakuwa ikikuletea habari zaidi kadri zitakavyopatikana.
Apumzike kwa Amani Mzee wetu Daudi Mwanja. Amina.