04/12/2024
NANE WADAKWA TUKIO LA KILUVYA.
Na Mwandishi Wetu.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar limesema linawashikilia Watu 8 kwa tuhuma za tukio la Novemba 11, 2024 eneo la Kiluvya ambapo Watu kadhaa walifanya jaribio la kumteka Mfanyabiashara, Deogratius Tarimo, Mkazi wa Kibaha - Pwani
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi, Muliro J. Muliro - SACP amesema Watuhumiwa wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika Mikoa ya Dar, Songea Ruvuma na eneo la Mbingu Mlimba Morogoro, pia wamekamata gari aina ya Toyota Raum waliyoitumia wakati wa tukio ikiwa na namba T 237 EGE ambayo si halisi, ambapo uchunguzi umebaini namba halisi ni T237 ECF
Amewataja waliokamatwa kuwa ni Bato Bahati Tweve (umri Miaka 32 – Bondia), Yusuph Abdallah (32), Fredrick Juma (31), Nelson Elimusa Msela (24 - Dereva Tax), Benk Daniel Mwakalebela ‘Tall’ (40), Thomas Ephraim Mwakagile ‘Baba Mage’ (45), Anitha Alfred Temba (27) na Isack Mwaifani (Bondia)