07/11/2025
Nimesikitishwa sana kuona jina langu na sura yangu vikihusishwa na tukio la Police akifanya mashambulizi kwenye maandamano.
Napenda kusisitiza kuwa mtu anayeonekana kwenye ile picha si mimi, tumefanana tu. Kwa sasa niko Congo kikazi nikiendeleza majukumu yangu k**a dereva wa gari la mizigo, nikiwa mbali kabisa na yaliyoendelea.
Ni uchungu mkubwa kuona mtu akituhumiwa kwa jambo zito k**a hilo bila kosa. Heshima yangu, maisha yangu ya kazi, na usalama wangu vimeguswa na jambo hili. Naomba jamii, ndugu na marafiki waendelee kutuamini; ukweli upo wazi.
Naamini haki itasimama na jina langu litarejea katika heshima yake. Ahsanteni kwa uungwana, sala na msaada wenu wote wakati huu mgumu.
Hamza Msonga ๐ฃ