Noni News

Noni News News around the World

Mamlaka ya Qatar inasema bado inawasaka watu wawili waliotoweka na kuyatambua mabaki ya binadamu baada ya shambulio la I...
11/09/2025

Mamlaka ya Qatar inasema bado inawasaka watu wawili waliotoweka na kuyatambua mabaki ya binadamu baada ya shambulio la Israel kuwalenga viongozi wakuu wa Hamas mjini Doha siku ya Jumanne.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa kuna wasiwasi katika duru za kijeshi za Israel kwamba shambulio hilo lenye utata mkubwa halikufanikiwa.

Wizara ya mambo ya ndani ya Qatar imeitambua miili ya wanachama watatu kati ya watano wa ngazi ya chini wa Hamas ambao kundi lenye silaha la Palestina lilisema waliuawa pamoja na afisa wa usalama wa Qatar.

Hamas imedai jaribio la kuua timu yake ya mazungumzo lilishindikana. Katika mahojiano na CNN, waziri mkuu wa Qatar hakufichua hatma ya mpatanishi mkuu wa Hamas Khalil al-Hayya.

"Hadi sasa... hakuna tamko rasmi," Sheikh Mohammed bin Abdul Rahman Al Thani alisema Jumatano jioni.

Pia alisema hatua ya Israel ni sawa na "ugaidi wa serikali" na kwamba anatumai washirika wa likanda wa Qatar watakubali "jibu la pamoja".

Rais wa Ghana John Mahama amethibitisha kuwa nchi hiyo imekubali kuwapokea raia wa Afrika Magharibi waliofukuzwa kutoka ...
11/09/2025

Rais wa Ghana John Mahama amethibitisha kuwa nchi hiyo imekubali kuwapokea raia wa Afrika Magharibi waliofukuzwa kutoka Marekani.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Accra, Rais Mahama alifichua kuwa watu 14 waliofukuzwa, wengi wao wakiwa Wanigeria na mmoja wa Gambia, tayari wamewasili Ghana chini ya makubaliano ya nchi mbili.

Rais Mahama alieleza kuwa Marekani iliwasiliana na Ghana kukubali raia watatu kuondolewa Marekani, na Ghana ilikubali kuwakubali raia wa Afrika Magharibi, akitoa mfano wa Itifaki ya ECOWAS kuhusu uhuru wa harakati huru. Itifaki hiyo inaruhusu raia wa nchi wanachama kuingia na kuishi katika nchi nyingine za Afrika Magharibi bila viza kwa hadi siku 90.

"Hatuna shida kuwakubali," Rais Mahama alisema, akiongeza kuwa Ghana iliwezesha kurejeshwa kwa rais wa Nigeria waliofukuzwa nchini mwao kwa basi, wakati raia wa Gambia akisaidiwa na mamlaka ya Ghana na ubalozi wa Gambia nchini Ghana.

Hii ni sehemu ya juhudi za utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kuwafukuza mamilioni ya wahamiaji ambao wako Marekani kinyume cha sheria, huku baadhi ya nchi za Kiafrika zikiwa tayari zinapokea wahamiaji waliofukuzwa. Rwanda, Sudan Kusini, na Eswatini zimekubali kuwapokea raia waliofukuzwa kutoka Marekani.

  Sept 10 2025
10/09/2025

Sept 10 2025

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imewasilisha ushahidi dhidi ya kiongozi wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army...
09/09/2025

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imewasilisha ushahidi dhidi ya kiongozi wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army nchini Uganda, Joseph Kony bila ya mtuhumiwa kuwepo mahakamani.
Mahakama inasikiliza kesi hiyo si kwa lengo la kutoa hukumu moja kwa moja, bali ni fursa kwa waendesha mashtaka kuwasilisha ushahidi wao. Kony anawakilishwa na wakili wa utetezi, lakini kwa mujibu wa sheria hawezi kuhukumiwa bila kuwepo mahakamani.
Kony anakabiliwa na mash*taka kadhaa ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, yakiwemo mauaji, ubakaji na utumwa wa kingono. Pia, anadaiwa kuongoza harakati za kikatili za LRA ziliyoitisha kaskazini mwa Uganda kwa miongo kadhaa.

Raia wawili wameuwawa na wengine 16 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya droni yaliyofanywa na Ukraine katika maeneo ya...
09/09/2025

Raia wawili wameuwawa na wengine 16 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya droni yaliyofanywa na Ukraine katika maeneo yanayodhibitwa na Urusi huko Donetsk
Raia wapatao wawili wameuliwa na wengine 16 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya droni na makombora ya Ukraine katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi ya Donetsk jana Jumatatu
Jumba la makazi la orofa tisa katika mji wa kiviwanda wa Makiivka kaskazini mwa Donetsk lililengwa na droni huku video katika mtandao wa kijamii ikionesha mashambulizi mazito ya makombora, pamoja na moja lililolenga kiwanda cha zamani cha kungenezea mifumo ya ufuatiliaji ya usalama wa anga mjini Donetsk
Mshirika ya habari ya Urusi yamewanukuu maafisa wa usalama katika maeneo yanayokaliwa wakisema droni kiasi 20 zimetumiwa katika mashambulizi mawili na vikosi vya ulinzi wa anga vimeingia kazini. Wamesema milipuko imesikika mjini Donetsk na anga la mji limegubikwa na moshi mzito.

Televisheni ya kitaifa nchini Nepal imeripoti watu 19 wameuwawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa, baada ya polisi ku...
09/09/2025

Televisheni ya kitaifa nchini Nepal imeripoti watu 19 wameuwawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa, baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji
Waandamanaji wanaitaka serikali kuondoa marufuku iliyowekwa kwa mitandao ya kijamii na kukomesha ufisadi. Msemaji wa polisi mjini Kathmandu, Shekhar Khanal, amethibitisha vifo hivyo
Polisi ilijaribu kuwadhibiti maelfu kwa maelfu ya waandamanaji hao wa Gen Z, kwa kutumia risasi za mpira, maji mazito na marungu, wakati waandamanaji walipojaribu kuvunja uzio wa polisi kutaka kuelekea bungeni
Ranjana Nepal afisa mmoja wa habari katika hospitali ya mjini Kathmandu amesema mabonu ya kutoa machozi yalirushwa pia hospitalini na kutatiza huduma za madaktari
Mitandao mengi ya kijamii ikiwa ni pamoja na Facebook, YouTube, na X, imefungwa tangu siku ya Ijumaa wiki iliyopita baada ya serikali kufungia mitandao ya kijamii 26 ambayo haijasajiliwa, hatua iliyowachanganya na kuwakasirisha watumiaji.

Kundi la Hamas Hamas, limesema liko tayari kwa makubaliano ya kina na Israel kuhusu kusitisha vita vya GazaTaarifa yake ...
04/09/2025

Kundi la Hamas Hamas, limesema liko tayari kwa makubaliano ya kina na Israel kuhusu kusitisha vita vya Gaza
Taarifa yake hiyo ya jana jioni inasema kundi hilo bado linasubiri majibu kutoka kwa Israel kuhusu pendekezo la hivi karibuni la wapatanishi wa kimataifa kuhusu kusitisha mapigano, aidha mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz masharti ya taifa lao katika makubaliano hayo ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka wote na kuondolewa kwa nguvu za kivita kwa Hamas
Aidha taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ilisema kuwa tangazo la Hamas ni propaganda nyingine tu ambayo haina jipya.

Timu za uokoaji nchini zinazoendelea na shughuli ya uokoaji nchini Sudan zimeipata miili 100 iliyokuwa imefunikwa chini ...
04/09/2025

Timu za uokoaji nchini zinazoendelea na shughuli ya uokoaji nchini Sudan zimeipata miili 100 iliyokuwa imefunikwa chini ya tope baada ya maporomoko makubwa ya ardhi kukisomba kijiji cha Tarasin, Darfur
Msemaji wa waasi wanaoliongoza eneo hilo Mohamed Abdelrahman al-Nair amesema juhudi za kuwatafuta manusura bado zinaendelea licha ya uhaba wa rasilimali, Makadirio ya awali yanaashiria kuwa karibu wakaazi wote zaidi ya 1,000 ya kijiji kilichokumbwa na maafa hayo wamekufa na mtu aliyesalimika ni mmoja pekee
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric amesema ukubwa wa janga hilo hadi sasa haufahamiki kwa kuwa eneo lililoathiriwa halifikiki kwa urahisi.

Mashirika ya misaada yataka jamii ya kimataifa kuongeza ufadhili kwa Afghanistan baada ya tetemeko kubwa la ardhiMashiri...
04/09/2025

Mashirika ya misaada yataka jamii ya kimataifa kuongeza ufadhili kwa Afghanistan baada ya tetemeko kubwa la ardhi
Mashirika ya misaada yataka jamii ya kimataifa kuongeza ufadhili kwa Afghanistan baada ya tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha richter 6.0 kuua angalau watu 1,400 na kuwajeruhi maelfu wengine.
Uingereza imetoa msaada wa dola milioni 1.3, ambapo fedha hizo zitaelekezwa kwa mashirika ya misaada na si kwa serikali ya Taliban, ambayo Uingereza haijaitambua rasmi, lakini pia korea Kusini siku ya Jumatano ilitangaza kuwa itatoa dola milioni 1 kupitia Umoja wa Mataifa
Tetemeko hilo lilitokea usiku wa Jumapili na kuathiri majimbo kadhaa ya mashariki ya Afghanistan yenye milima na yaliyo mbali, hili ni janga la hivi karibuni kuikumba Afghanistan, na ni tetemeko la tatu kubwa tangu kundi la Taliban lilipochukua madaraka mwaka 2021.

Shirika la umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi, limesema wimbi la wakimbizi wanaokimbia kutoka Burkina Faso na kuin...
04/09/2025

Shirika la umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi, limesema wimbi la wakimbizi wanaokimbia kutoka Burkina Faso na kuingia Mali, linaongeza hali ya dharura ya kibinadamu, UNHCR sasa ikitaka misaada zaidi kutolewa kuwasaidia
Tangazo la UNHCR hata hivyo limekuja kipindi ambacho mashirika mengi ya misaada kwenye eneo la Sahel yanakabiliwa na uhaba wa fedha kutokana na kupungua kwa ufadhili
Nchi za Burkina Faso na Mali ambazo zote zinatawaliwa na wanajeshi, zinakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi ya kijihadi yanayohusishwa na mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda na Islamic State
Kwenye taarifa yake, UNHCR imesema raia wanaokimbia kutoka Burkina Faso, wengi ni wanawake na watoto kutoka katika vijiji kadhaa vinavyopakana na Mali na wamekuwa wakikimbia tangu Agosti 5
Kati ya Agosti 7 na 15 mwaka huu, idadi ya watu waliosajiliwa na Tume ya Kitaifa ya Wakimbizi ya Mali (CNCR) iliongezeka kutoka watu 1,733 hadi 12,000, ikiwa ni sawa na wakimbizi 1,500 kwa siku
UNHCR sasa inasema bila usaidizi wa haraka kutoka kwa washirika wa kiufundi na kifedha, maelfu ya wanawake, watoto watakuwa hatarini kutumbukia katika dhiki.

Viwango vya kubadilishia fedha za kigeni Sept 4, 2025
04/09/2025

Viwango vya kubadilishia fedha za kigeni Sept 4, 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema katika mkutano wa Alhamisi na viongozi wenzake wa Ulaya, atapendekeza mazung...
03/09/2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema katika mkutano wa Alhamisi na viongozi wenzake wa Ulaya, atapendekeza mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine yafanyike mjini Geneva
Viongozi kadhaa wa Ulaya akiwemo pia rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky watakutana Alhamisi mjini Paris, huku wengine karibu 30 wakishiriki kwa njia ya mtandao katika mazungumzo ya kujadili suala la hakikisho la usalama kwa Ukraine baada ya vita
Hayo yakiarifiwa, Moscow na Kiev zimeendelea kushambuliana vikali ambapo watu wawili wameripotiwa kuuawa mjini Kiev na katika mkoa wa Zaporizhzhya huku shambulizi ya Ukraine katika mji mkuu wa mkoa wa Rostov nchini Urusi, likisababisha watu zaidi ya 300 kuhamishwa katika makazi yao.

Address

MBEYA, TZ
Mbeya
53119

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Noni News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share