26/07/2026
SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUFUTA MACHOZI YA WANANCHI WA KATA YA MPOMBO, HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSOKELO
Wananchi wa Kata ya Mpombo wameendelea kunufaika na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya Serikali kutoa Tsh 780,965,648.00 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Mpombo.
Leo, tarehe 26 Julai 2026, wananchi wameeleza shukrani zao wakati wa ziara ya Timu ya Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 ya Mkoa wa Mbeya, kwa kushirikiana na Kamati za Wilaya, zilizotembelea mradi huo unaotarajiwa kuwekewa Jiwe la Msingi wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026.
Mradi huu ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi, hivyo kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu.
Hongera Serikali ya Awamu ya Sita! Hongera Lutengano G. Mwalwiba, Mhe.Mbunge Jimbo la Busokelo, Hongera Anyasisye Njobelo, Mhe Diwani kata ya Mpombo, hongereni Wananchi wa Kata ya Mpombo kwa hatua hii muhimu ya maendeleo!