08/12/2018
UKO WAPI NIKUFATE ANGEL WANGU
(MV NYERERE 04)
Maneno ya Angel yalinfanya kujiona kwamba mimi ni nani na nini nifanye hapa duniani
"Idd, kumbuka kwamba mama ako ni k**a MAMA angu mzazi hivyo nitakuwa pamoja nanyi kwa kila hatua "
Pumzi ndefu nilishusha baada ya maongezi ya kina ndipo Angel akakata simu nami kufikiria yajayo juu ya MAMA angu
MWEZI MMOJA BAADAE
Mawasiliano kati ya Idd na Angel yalizidi kushamiri lakini Hakuna ata mmoja aloweza kufungua kinywa chake kumtamkia mwenzake kwamba tayari ana hisia nae za mapenzi
Kijana Idd uzalendo ukawa unamshinda ndipo akaamua kujaribu kurusha sumu yake ingawaje alifikiria sana itakuwaje endapo k**a angel atakataa
"Angel, kwakweli ni kipindi kirefu sana tangu niwe na mawasiliano naww na mengi umenisaidia ila tatizo lipo moyoni mwangu "
'tatizo gani Idd ongea tu usijali '
"Angel, kwanza natanguliza samahani k**a nitakukwaza kwa kile nitakachoenda kukwambia "
'ongea tu Idd kuwa huru '
"Angel, najijua wazi kwamba mimi ni maskini sina hadhi ya kuwa naww lkn ukweli nimekupenda sana, nahitaji huwe mke wangu Angel "
'uuuhfff, Idd kwann umeongea maneno ya kumuudhi muumba wako? Sisi matajiri hatuna tofauti na nyie tena yawezekana nyie mkawa mnaishi sana kwa amani kuliko sisi"
'lakini pia naomba muda nilifanyie kazi ombi lako Idd, sawa? '
Angel aliongea kwa sauti nzuri ingawaje bado inaonesha kwamba hakufurahia maneno yale ya Idd
****
Baada ya mawasiliano ya dakika kadhaa Angel alikata huku uso wa furaha ukianza kumchanua kwani alishagampenda kijana Idd tangu muda
'yes, sasa hapa nachotaka kufanya ni kumtumia pesa ya matumizi ili kumfanya Idd asiweze kuishi kwa taabu tena
****
Ndani ya dakika 13 Simu ya Idd ikaingia ujumbe mfupi wa maandishi huku kijana huyo akiwa biz na jembe kulipalilia shamba lake analolilima mboga mhoga za majani
"hafu hawa wa mtandao bhana unaweza ukakuta meseji ya kudiwa salio nililokopa "
Sasa kwa uchovu wa jua kali la kipindi hiki Idd aliifata simu ile alivofungua tu ujumbe akawa amepata nguvu .