Dizzim Fm

Dizzim Fm Official page for Dizzim fm | Instagram & Twitter | Frequency 93.1 Morogoro |

Bunge la mpito la Burkina Faso limepitisha rasmi sheria mpya inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja, na kuanzisha adhabu ...
02/09/2025

Bunge la mpito la Burkina Faso limepitisha rasmi sheria mpya inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja, na kuanzisha adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitano jela.

Sheria hiyo, iliyopendekezwa kwa mara ya kwanza Julai 2024, iliidhinishwa rasmi na kuanza kutumika Septemba 1, 2025 Chini ya sheria hiyo mpya, wahalifu wanakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka miwili na mitano pamoja na faini.

Waziri wa Sheria Nchini humo Edasso Rodrigue Bayala alieleza kuwa hatua hiyo inatumika sio tu kwa raia lakini pia kwa raia wa kigeni, ambao pamoja na vifungo vya jela wanaweza kukabiliwa na kufukuzwa.


Mashambulizi ya Jeshi la Israel yameua Wapalestina 17, wakiwemo watu sita waliokuwa wanakitafuta misaada, huku Israel ik...
02/09/2025

Mashambulizi ya Jeshi la Israel yameua Wapalestina 17, wakiwemo watu sita waliokuwa wanakitafuta misaada, huku Israel ikieleza kuwa mashambulizi hayo yalilenga kundi la Hamas na waliofariki ilikuwa ni kwa sababu zingine.

Al Jazeera imeripoti kuwa, Israel ilitumia vifaru kulipua magari yaliyokuwa katika kitongoji cha Sheikh Radawan usiku wa kuamkia leo pia ilifanya mashambulizi ya anga kwa kutumia makombora.

Aidha wakazi wa eneo hilo wemesema, wanajeshi wa Israel pia walituma magari ya zamani ya kivita katika maeneo ya mashariki ya kitongoji hicho kilichojaa watu wengi, kisha kuyalipua kwa mbali na kuharibu nyumba kadhaa na kulazimu familia kuyakimbia makazi yao.

"Ulikuwa usiku wa kutisha, milipuko haikukoma na ndege zisizo na rubani ziliendelea kufanya doria angani katika eneo hilo.

Watu wengi waliacha nyumba zao wakihofia maisha yao, huku wengine wakiwa hawajui pa kwenda," imelezwa.


🙏

Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) katika barabara ya Mbagala, ambayo awali ilitarajiwa kuanza leo Jumatatu, ...
01/09/2025

Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) katika barabara ya Mbagala, ambayo awali ilitarajiwa kuanza leo Jumatatu, Septemba 1, 2025, imesogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa miundombinu muhimu, ikiwamo mageti janja ya ukataji tiketi na kituo cha kujazia gesi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dk. Athuman Kihamia, amesema licha ya mabasi 151 kuwasili tayari, huduma hiyo imeahirishwa ili kutoa nafasi ya kukamilisha miundombinu.

> “Mabasi yamewasili, lakini hatutaweza kuanza kutoa huduma leo k**a tulivyoahidi, kwa kuwa baadhi ya miundombinu haijakamilika. Mageti janja bado hayajafungwa, na kituo cha kujazia gesi kilichopo kwenye karakana ya Mbagala hakijakamilika. Hata hivyo, taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo tutaitoa baada ya wiki moja,” amesema Dk. Kihamia.

Mabasi hayo yaliwasili katika karakana ya Mbagala Rangi Tatu usiku wa Agosti 29, 2025, yakitoka bandarani, baada ya shughuli ya uhamishaji iliyodumu kwa siku mbili.


Gazeti la The Washington Post limeripoti kuwa Marekani inapanga kuwahamisha wakaazi wote wa Ukanda wa Gaza na kuchukua u...
01/09/2025

Gazeti la The Washington Post limeripoti kuwa Marekani inapanga kuwahamisha wakaazi wote wa Ukanda wa Gaza na kuchukua udhibiti kamili wa ukanda huo chini ya mpango unaozingatiwa na utawala wa Rais Donald Trump.

Chini ya mpango huo Ukanda wa Gaza ambao umegeuzwa kuwa kifusi kufuatia mashambulizi ya Israel, unatarajiwa kuwa chini ya usimamizi wa Marekani kwa angalau miaka 10.


Vijana zaidi ya elfu sita miatano wanatarajia kupatiwa ajira kwenye sekta ya uchimbaji wa madini ya dhahabu Nyazaga Geit...
01/09/2025

Vijana zaidi ya elfu sita miatano wanatarajia kupatiwa ajira kwenye sekta ya uchimbaji wa madini ya dhahabu Nyazaga Geita chini ya uongozi wa Rais Samia,Perseus Mining imewekeza takribani dola milioni 523 katika Mradi wa Dhahabu wa Nyanzaga-Geita (NGP), unaotarajiwa kutoa dhahabu ya kwanza katika Robo ya Kwanza ya 2027 kwa mtindo wa mgodi wa wazi (open-pit).

Uwekezaji huo unafadhiliwa kupitia mikopo isiyo na riba kutoka kwenye fedha na dhahabu ya Perseus yenye thamani ya dola milioni 801. Kazi za awali zimetekelezwa ikiwemo ujenzi wa kambi za muda, kazi za ardhi, na utekelezaji wa Mpango wa Uhamishaji Makazi (RAP). Awamu ya kwanza ya mgodi itadumu kwa miaka 11, ikiwa na akiba ya dhahabu inayokadiriwa (Probable Ore Reserve) ya tani milioni 52 kwa kiwango cha 1.40 g/t, sawa na zaidi ya 2.3 milioni oz za dhahabu. Uzalishaji unatarajiwa kuwa kati ya 200,000 hadi 246,000 oz kila mwaka, na gharama ya uzalishaji kwa oz (AISC) ni dola 1,211 Ikiwa thamani ya dhahabu itakuwa dola 2,100 kwa oz.

Hata hivyo Mradi wa NGP unatarajiwa kuleta faida ya fedha taslimu (free cashflow) ya dola milioni 1,133 kabla ya kodi na dola milioni 706 baada ya kodi. Thamani ya sasa ya mradi (NPV) inakadiriwa kuwa dola milioni 404 kabla ya kodi na dola milioni 202 baada ya kodi, huku kiwango cha faida cha mradi (IRR) kikiwa asilimia 26 kabla ya kodi na asilimia 19 baada ya kodi, Mradi wa Nyanzaga-Geita utazalisha ajira jumla ya 6,500 za moja kwa moja.


Nadhani jezi za timu zote tatu Yanga SC, Simba SC na Azam FC mmeziona za msimu huu wa 2025/26.Hapa kila timu imebuni kwa...
01/09/2025

Nadhani jezi za timu zote tatu Yanga SC, Simba SC na Azam FC mmeziona za msimu huu wa 2025/26.

Hapa kila timu imebuni kwa kiwango chake ikiwemo ubora wa Jezi zenyewe mpaka rangi.

Mpaka sasa ni nani jezi zake ni kali zaidi ya wenzie?

1. Yanga SC
2. Simba SC
3. Azam FC


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mat...
31/08/2025

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofauti ya picha aliposalimiana na Majirani zake wakazi wa Chamwino Mkoani Dodoma wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu leo August 31,2025.


Jeshi la Polisi nchini limeeleza kuwa limeshaanza kushughulikia wamiliki wa magari walioweka usajili wa namba SSH 25 30 ...
31/08/2025

Jeshi la Polisi nchini limeeleza kuwa limeshaanza kushughulikia wamiliki wa magari walioweka usajili wa namba SSH 25 30 kwani hazitambuliki kisheria

Kauli hiyo imetolewa Agosti 29.2025 jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime wakati akijibu swali la Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) Devis Minja aliyetaka kujuwa uhalali wa namba hizo na usalama wa wananchi, katika mdahalo wa kitaifa wa usalama wa waandishi wa habari

DCP Misime amesema kuwa tayari changamoto hiyo imeshafanyiwa kazi na haionekani tena, 'tumeshalifanyia kazi natumaini huzioni, kwasababu hazipo katika mfumo ambao umehalalishwa kwahiyo ukiziona tena tupe taarifa tutazirukia mara moja na sheria itachukua mkondo wake"


Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikielez...
30/08/2025

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikieleza kuwa Gasper Temba (30) ametekwa Jijini Arusha.

Akifafanua tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema kuwa taarifa sahihi ni kwamba Gapser Temba ambaye ni mkazi wa Arusha hajatekwa, bali amek**atwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma zinazomkabili za kughushi Nyaraka.

SACP Masejo amebainisha kuwa tukio hilo llilifunguliwa huko Jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa amek**atwa kwa mujibu wa sheria na taratibu nyingine za kisheria zinafuata.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika zinazoweza kusababisha taharuki katika jamii.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2025, amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa matumiz...
30/08/2025

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2025, amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika magereza 129 nchini.

Uzinduzi huo umefanyika katika Gereza la Karanga, Moshi mkoani Kilimanjaro, ukiwa ni mwakilishi wa magereza yote nchini.

Kwa sasa, vyanzo vya nishati mbadala vinavyotumika katika magereza ni gesi vunde (biogas), mkaa mbadala (briquettes), kuni poa, gesi asilia (natural gas) pamoja na umeme.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema hatua hiyo ni ya kupongeza kwa kuwa inaunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha jamii inatumia nishati safi, hivyo kupunguza madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyo rafiki kwa mazingira na afya.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Utunzaji wa Mazingira kutoka Jeshi la Magereza, SACP Daimu Mmolosha, amesema lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha kunakuwa na vyanzo zaidi ya kimoja vya nishati ili kuepuka utegemezi wa kuni na mkaa.


Mahak**a nchini Thailand imemwondoa madarakani Waziri Mkuu Paetongtarn Shinawatra (39), mwaka mmoja tu baada ya kushika ...
29/08/2025

Mahak**a nchini Thailand imemwondoa madarakani Waziri Mkuu Paetongtarn Shinawatra (39), mwaka mmoja tu baada ya kushika wadhifa huo, kwa madai ya kukiuka maadili ya uongozi.

Uamuzi huo umetokana na mazungumzo ya simu yaliyovuja kati ya Shinawatra na kiongozi wa zamani wa Cambodia, Hun Sen, ambayo yalisababisha taharuki wakati mataifa hayo mawili yalipokuwa karibu kuingia kwenye mzozo wa kijeshi.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM  Dkt. Samia Suluhu Hassan akipunga mkon...
29/08/2025

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM
Dkt. Samia Suluhu Hassan akipunga mkono kwa wananchi alipowasili katika Viwanja vya Ngerengere Mkoani Morogoro tayari kwa Mkutano wa hadhara wa Kampeni za uchaguzi Mkuu Leo August 29,2025.


Address

Mtawala
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dizzim Fm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category