Sio Kwa Ubaya Kikosi

Sio Kwa Ubaya Kikosi Nguvu Ya Kipaji Katika Kubadili Maisha

GROUP LA MUZIKI NA BURUDANI ๐Ÿ‘‡
12/09/2025

GROUP LA MUZIKI NA BURUDANI ๐Ÿ‘‡

WhatsApp Group Invite

DADA USILAZIMISHE KUOLEWA, KUWA SINGLE MOTHER SIO LAANA.Usipange kujuta hata siku moja eti kwasababu mume aliyekupa ujau...
01/09/2025

DADA USILAZIMISHE KUOLEWA, KUWA SINGLE MOTHER SIO LAANA.

Usipange kujuta hata siku moja eti kwasababu mume aliyekupa ujauzito amekukimbia au mume uliyezaa nae amekuacha na amekwenda kuoa mtu mwingine.

Usione aibu hata kidogo eti watu watakuonaje au watasema nini kuhusu wewe kutokuolewa na mwanaume uliyezaa nae.

Ndoa ni mpango wa Mungu unaofanikishwa na watu wa jinsia mbili tofauti waliokubaliana kwa hiyari kuishi maisha ya mke na mume siku zote za maisha yao.

Ndoa ni agano takatifu ambalo Mungu amelibariki.

Kwa kusudi la MUNGU mtoto anapaswa atokane na ndoa na haipaswi kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa na ndio maana likaitwa tendo la ndoa.

Lakini kutokana na madhaifu ya kibinadamu tunajikuta tunafanya zinaa na hata kuzaa kabla ya ndoa.

Neno linasema
1 Wakorintho 7:1
"Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke."

Kabla ya ndoa neno linatuhasa tusigusane.

1 Wakorintho 7:3
"Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake."

Baada ya ndoa ndio mume na mke wanapaswa kupeana haki ya ndoa.

Waebrania 13:4
"Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu."

Sasa imeshatokea zinaa imefanyika na mtoto amepatikana.
SWALI: Je, ufanye nini?

Single mother, narudia tena usijilaumu, usilie, usijihukumu wala usilazimishe ndoa na huyo uliyezaa nae.

K**a upo tayari na yeye yupo tayari kuoana basi ni jambo zuri na Mungu azidi kuwabariki. Lakini k**a haupo tayari au yeye hayupo tayari USILAZIMISHE.

Mrudie MUNGU, Jitunze, Jithamini Na Usifanye Tena Zinaa. Omba Ukiamini Na Mungu Atakupa Mtu Sahihi Wa Kuoana Nae.

K**a kuna madhaifu kadhaa ambayo pengine yalimfanya baba wa mtoto ashindwe kuanzisha maisha ya pamoja na wewe jitahidi urekebishe na uwe mwanamke bora zaidi ya alivyokukuta.

Kataa zile story za mashoga zako au ndugu zako eti kuna mganga mmoja mzuri twende nikupeleke mwambie nenda mwenyewe NDOA HAILAZIMISHWI.

Shirikiana vizuri na mzazi mwenzako katika malezi na matunzo bora ya mtoto. Usikubali kutumika tena kingono. TUNZA THAMANI YAKO.

Mwenyezi MUNGU awabariki single mothers wote na awatimizie aja zenu zilizo njema.

KIPAJI PEKEE HAKITOSHI KUKUTOA HAPO ULIPO, KUBALI KULIPA GHARAMA. ๐Ÿ—ฃ๏ธMtaani kuna watu wengi sana wenye vipaji vikubwa lak...
01/09/2025

KIPAJI PEKEE HAKITOSHI KUKUTOA HAPO ULIPO, KUBALI KULIPA GHARAMA. ๐Ÿ—ฃ๏ธ

Mtaani kuna watu wengi sana wenye vipaji vikubwa lakini miaka nenda miaka rudi wapo palepale yaani hawapigi hatua.

Kuna mtu ni mchezaji mzuri sana wa mpira wa miguu lakini hata kwenye timu ya mtaani kwao hapati nafasi ya kucheza.

Kuna mtu ni muimbaji mzuri na ana nyimbo nyingi zenye mafunzo na burudani lakini hata studio hajawahi kufika ila ukimuuliza atakwabia "mimi najua sana kuimba siku nikisema niingie studio Mondi mwenyewe haniwezi."

Sawa kipaji unacho lakini kipaji peke yake hakiwezi kukupa mafanikio yoyote k**a usipokubali kulipa gharama.

Kuna mambo mengi yanayoweza kukufanya ufanikiwe kupitia kipaji lakini leo tunashare machache tu k**a ifuatavyo;

1. Gundua kipaji chako, - Hii ni hatua ya mwanzo kabisa ya kufahamu wewe una kipai gani. Je, kucheza mpira, kuimba au kuogelea?

2. Fanya mazoezi, - Ukishagundua una kipaji gani pili unapaswa kujua ni mazoezi ya aina gani yatasaidia kukuza kipaji chako.

3. Jitokeze hadharani, - Kipaji hakiwezi kukutoa hapo ulipo k**a utabaki nacho chumbani. Toka nje, onesha watu uwezo ulionao ili waone uimara wako na yapi madhaifu yako kusudi wakurekebishe uzidi kuboresha kipaji chako.

4. Tafuta connection (ungana na watu.) - Siku zote hakuna mafanikio ya mtu mmoja. Tafuta watu wa kushirikiana nao au watakaokuwa tayari kukushika mkono na kufanikisha safari yako ya mafanikio kupitia kipaji chako.

5. Tafuta pesa, - Siku hizi kila kitu kinahitahi pesa. Bila pesa utashindwa kufanya vitu vingi sana muhimu katika kipaji chako.
MFANO: Mwanamuziki anahitaji pesa kwaajili ya kulipia studio, kushoot videos, mavazi, gharama za digital platforms nk.

NB: Mafanikio sio jambo la mojakwamoja bali ni mchakato wa muda mrefu ambapo ndani yake kuna kupanda na kushuka. Usisahau kuna kudhurumiwa pia but stay focused.

Usiruhusu kukata tamaa hatak**a umeshindwa kutoka mara ngapi. Jenga imai kuwa ipo siku kipaji chako kitakufikisha kwenye nchi ya ahadi na kula matunda ya jitihada zako.

MUNGU akubariki sana utimize ndoto zako.

๐ŸŒ

MUNGU HAKUPI UNACHOTAKA BALI ANAKUPA UNACHOSTAHILI.Kila mtu anapenda maisha mazuri na kila mtu anapenda vitu vizuri. Kil...
01/09/2025

MUNGU HAKUPI UNACHOTAKA BALI ANAKUPA UNACHOSTAHILI.

Kila mtu anapenda maisha mazuri na kila mtu anapenda vitu vizuri. Kila mtu anapenda mke mzuri na kila mtu anapenda mume mzuri.

Tukiwa shuleni kila mtu alipenda kupata Division I au First Class ya 5.0 GPA lakini sio wote tulifanikiwa kupata.

Tulipo hapa kila mtu anapenda aishi miaka mingi na hata siku akifa anapenda aende mbinguni lakini sio wote tutakao uona ufalme wa Mungu.

Neno linasema
MATHAYO 7:21
"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni."

Hapa tunajifunza kwamba kusema tu kwamba mimi nataka kuwa tajiri hakuwezi kukufanya wewe uwe tajiri.

Kusema tu kwamba mimi nataka kufaulu mitihani ya shule au chuo hakutoshi kukufanya wewe ufaulu.

Kusema tu kwamba mimi nataka kumuoa au kuolewa na fulani haitoshi kukufanya wewe kuoa au kuolewa na mtu huyo.

Matokeo mazuri ya kila jambo yana kanuni na hata kufeli pia kuna kanuni.

Maranyingi mtu anapata kile anachostahili na sio kile anachokipenda.

Ukiona mtu amepata kile asichostahili basi kuna mawili aidha amepata bahati au kuna nguvu zisizo halali zimetumika na kutumia nguvu zisizo halali ni lazima kutaleta madhara makubwa siku za mbeleni.

Furaha isiyotokana na haki haiwezi kudumu.

Tujifunze kulizika na kile MUNGU anachotujalia na tushukuru kwani ndicho tunachostahili kupata kinyume na hapo tutaishia kumkufuru yeye aliyetujalia.

K**a mafanikio uliyonayo ndio yale uliyotaka au k**a mume / mke uliyenae ndio yule uliyemtaka piga goti mwambie MUNGU Ahsante.

Lakini k**a bado ulivyo leo si vile unavyotaka kuwa endelea kuomba naye MUNGU atakupa unachostahili lakini hakikisha unafanana na kile unachokiomba.

Huwezi kupata mke mwema wakati wewe sio mwema wala huwezi kupata mume bora wakati wewe sio bora. Utapata unachostahili.

Neno linasema
Mathayo 7:6
"Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua."

Hivyo basi MUNGU hakupi unachotaka, anakupa unachostahili.

Address

Kilakala
Morogoro
KILAKALA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sio Kwa Ubaya Kikosi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share