Richard Vako

Richard Vako Hi! All friends,fans,members and my fellows through my page,I salute and wish you happy new

HIVI ULIWAHI KUJIULIZA NINI MAHUSIANO YA KUMBIKUMBI,MCHWA,NA MALKIA WA MCHWA KUISHI PAMOJA NDANI YA KICHUGUU?Ameandika:F...
09/07/2023

HIVI ULIWAHI KUJIULIZA NINI MAHUSIANO YA KUMBIKUMBI,MCHWA,NA MALKIA WA MCHWA KUISHI PAMOJA NDANI YA KICHUGUU?

Ameandika:
Frank Aurelian Mbowe

Tupate elimu kidogo:-

✍ Je, mchwa huzaliwa na nani ?
✍ Kumbikumbi hutokeaje ?
✍ Malkia huzaliwa na nani ?
✍ Na je, dume la malkia hupatikanaje ?

Ni kawaida kila mara baada ya mvua kuanza kunyesha wadudu jamii ya kumbikumbi huonekana wakiruka huku na kule.

Je, umewahi kuona kumbikumbi wakiwa wawili huku wamekatika mbawa,halafu wanafuatana kwa karibu kabisa mmoja akiwa mbele na mwingine akiwa nyuma?

K**a umeona tukio hilo basi yule wa mbele ni jike na wa nyuma ni dume,wameungana pamoja k**a "couple".

Vile wanavyozurura wanatafuta sehemu yenye udongo mzuri unaofaa kwa ajili ya kuanzisha makazi mapya.
K**a hawatodhuriwa na maadui,wakifanikiwa kupata sehemu hiyo yule wa mbele ambaye ni jike atasimama na kuanza kuchimba kijishimo kidogo na kujifukia ndani huku dume akimsaidia.

Watafanya hivyo kwa kwenda chini hadi sehemu ambayo watajiridhisha kwamba ni salama kwao angalau wanaweza kujisitiri.
Wakishafika eneo hilo watasaidiana kupanua chumba kidogo ili kuwa na nafasi ya kutosha halafu jukumu la kuanza kumlisha yule jike ili anenepe litaanza kutekelezwa na dume peke yake.

Kwa maana nyingine ni kwamba dume la kumbukumbi anamuandaa Malkia.
Ataendelea na zoezi hilo mpaka pale jike atakaponenepa sana k**a picha inavyo onyesha,wakati hushindwa hata kujisogeza ila wakati sahihi ukifika basi yule Malkia atapandwa na dume kisha mayai yatatagwa.

Nakukumbusha kwamba familia ya kumbikumbi kwenye kichuguu kimoja imegawanyika k**a ifuatavyo:-

1.Malkia na Mume wake wale waliokuwa wamefuatana.

2.Mchwa watenda kazi "workers"

3.Askari mchwa "Soldiers" Hawa ni wale wenye mikasi mikubwa na vichwa vikubwa.

4.Kumbikumbi

Jambo la kushangaza hapa ni kwamba Malkia ana uwezo wa kuamua mayai atakayotaga yawe ya kundi gani kati ya hayo waliotajwa hapo juu.

Kwa mfano:

Kwa kuwa hawa wawili wamekutana na wameandaa chumba kidogo tu cha kuishi uzao wa kwanza utakuwa ni wa kundi la mchwa wafanyakazi zaidi ili waongeze vyumba na kupanua ngome.

Hawa watatengeneza kichuguu imara lakini kikianzia chini ardhini ili iwe k**a msingi imara wa kichuguu tutakachokuja kukiona kikimea huku juu ya uso wa Dunia.

Kutoka pale malkia alipo na mume wake watamsogeza chini zaidi kwa sababu za kiusalama kwa kuwa bado hawana jeshi lolote imara la kumlinda.
Kule kutakuwa na chumba kikubwa zaidi na Baba Mchwa ataacha kabisa shughuli za utafutaji kwa kuwa kazi hiyo itafanywa na uzao wa kwanza wa wafanyakazi mchwa.

Wote wawili wataendelea kutunzwa mpaka wakati ufaao wa malkia kupandwa na kutaga tena mayai mengine.

Awamu hii mayai karibu yote yatakuwa ni mchwa askari watupu ili kuimarisha ulinzi.

Kwa hiyo mpaka hapo kunakuwa na vitengo viwili muhimu:-

✍ Kitengo cha mchwa wa ulinzi
✍Kitengo cha mchwa wa ujenzi na chakula

Malkia akiwa anataga atazingatia upungufu wa kikosi kimojawapo kwa kila msimu na wakati huo huo shughuli zitakuwa zinaendelea kwa kasi kubwa wajakazi na askari mchwa wakijituma usiku na mchana mpaka kichuguu kinakuwa kikubwa na kirefu k**a ambavyo tumekuwa tukiona maeneo mbalimbali kwenye mazingira yetu tunayoishi.

Uimara wa jeshi mchwa na ukubwa wa kichuguu utapelekea siku moja jeshi na wajakazi wamuhamishe Malkia kutoka kule chini walipomuandalia Ikulu ndogo na kumleta upande wa juu wa kichuguu sehemu hii tunayoiona sisi ila ni pale katikati kabisa na eneo la kukaribia ardhi ambapo wanakuwa wameshaandaa Ikulu kubwa zaidi.

Sehemu hii ni nzuri zaidi kwa kuwa wakati wa joto ni rahisi wajakazi kufungua njia za upande ule unaopokea upepo na upande wa juu ili hewa safi iingie vizuri na kutokea juu au upande wa pili.

Sehemu hii ni nzuri pia kwa kuwa hata mvua ikinyesha wajakazi wanafunga tu vent zote hivyo mvua haitoingia ndani na hata k**a itazidi na kutafuta upenyo basi maji yakifika kule kwenye ikulu ndogo ya chini yatakuta malkia kahamishwa yuko sehemu salama huku katikati mwa kichuguu.

Hawa wadudu wana akili na hesabu kubwa mno asikwambie mtu aiseee !!😄😄

Wakati haya yote yakiendelea nakukumbusha kwamba zoezi la kutaga nalo litakuwa linaendelea kwa majira yake na Malkia ataamua aongeze idara ipi kulingana na mahitaji.

Kwa kuwa Malkia anajua yeye ni zao la Kumbikumbi basi ndio kuna wakati ambao hahitaji kuongeza Jeshi wala wajakazi ila ataongeza
kwa kutaga mayai ambayo watazaliwa Kumbikumbi ili wakitoka waweze kuruka mbali na kusambaa ili kuanzisha uzao wao na kuongeza falme za mchwa popote pale inapowezekana.

Kumbikumbi hao wataruka na baadae mbawa zitakatika watatafutana na kukutana wenye jinsia tofauti ambao wataanza harakati k**a nilivyoeleza kwa hawa wawili waliofanikiwa kutengeneza kichuguu kikubwa kabisa.

Nakukumbusha!

Kundi la wajakazi na Askari mchwa hawana jinsia,si madume si majike ni "Sexless" 😁😁

Kwa nini iwe hivyo?

Huu si ukatili bali ukiona kichuguu kinavyojengwa kwa ushirikiano usiku na mchana ni kwamba hawana muda wala hisia za kuwaza mapenzi wala hakuna atakayetumwa udongo wa kujengea yeye akapitia Guest kwanza kisa ana hamu zake 😄😄

Hapa kazi ni kazi na ulinzi ni ulinzi tu.
Hakuna kulinda na kuweka silaha chini kisa demu mkali kapita.
Kundi pekee lenye uzao na jinsia ni kutoka kundi la kumbikumbi tu.

Asante.

Address

Modeko Mazimbu
Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Richard Vako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category