26/12/2025
KISA CHA BUBU NA MAJARIBU YA DUNIANI🪄🔋
Siku moja katika pitapita zangu mtaani nilikutana na watu wa aina mbili tofauti, mwenye uwezo wa kutafuta hela na asiye kuwa na huo uwezo wa kuingiza hata 0.1% kwa siku.
Basi ilikuwa hivi, asiye kuwa na huo uwezo alikuwa ni
(BUBU) alipita karibu na ofisini kwangu akihitaji kupata msaada fulani ambao mimi nilishindwa kuufumbua kutokana na vile vitendo alivyoonesha kuwa ni kitu fulani.
Tulikaa k**a dakika 3, akatokea mzee ambaye binafsi yeye kabarikiwa na Mungu ridhiki anaipata vizuri bila shida. Mzee huyu alijaribu kushare baadhi ya vitendo na yule bubu. Hali ilikuwa hivi:
MZEE ;Bwana naomba ninunuliwe soda k**a hiyo unayokunywa.
BUBU;Aaah hapana bwana mimi mwenyewe nimenunuliwa kule na jamaa fulani.
MZEE;Aaah wewe ninunulie bwana, hela si hiyo umeshika?
BUBU;Hapana bwana..
MZEE;Wewe ninunulie moja bwana, hela umeshika mkononi...
BUBU;Nilishaambiwa nisimnunulie mtu yeyote, hata k**a atataka, kwa sababu hela hii imetolewa kwa ajili yangu tu.
MZEE;Lakini sisi tunasaidiana, unayokunywa si umegawiwa tu, sasa nawe unisaidie...
JE?Mzee Huyu yupo sahihi au kajishusha heshima na ni unyanyasaji au imekaaje?