Abeid Mugeta

Abeid Mugeta from Allah, for Allah, to Allah

We arrive in this world crying, yet we must Walk through life with smilesMugeta 📌
14/08/2026

We arrive in this world crying, yet we must Walk through life with smiles
Mugeta 📌

Kutoka kwa Anas bin Malik رضي الله عنه amesema:Watu wawili walipiga chafya mbele ya Mtume rehema na amani ziwe jju yakeM...
13/08/2026

Kutoka kwa Anas bin Malik رضي الله عنه amesema:

Watu wawili walipiga chafya mbele ya Mtume rehema na amani ziwe jju yake

Mtume akamsomea dua mmoja wao, lakini hakumsomea mwingine. Yule ambaye hakusomewa dua akasema: “Fulani alipiga chafya ukamsomea dua, nami nimepiga chafya hukunisomea dua.” Mtume rehema na amani ziwe jju yake akasema:

*“Huyu amemsifu Allah, lakini wewe hukumsifu Allah.”*

Imepokelewa na Muslim, 2991.

Mafunzo: Hadithi hii inaonyesha jinsi Mtume rehema na amani ziwe jju yake alivyowafundisha Maswahaba wake adabu za kijumla, pamoja na adhkari na dua zinazofaa kusemwa katika hali mbalimbali.

Pia inatufundisha kwamba malipo huendana na aina ya matendo. Yule anayemsifu Allah baada ya kupiga chafya anastahiki kuombewa dua, lakini yule anayepuuza kumshukuru Allah hakusomewi dua hiyo.

Kwa hiyo, unapopiga chafya sema: Alhamdulillaah, ili upate dua ya ndugu yako: Yarhamukallaah.

Mwakani tenaDaima mbele Nyuma mwiko
12/08/2026

Mwakani tena
Daima mbele Nyuma mwiko

Albert kangwandasave the name as he goes
12/08/2026

Albert kangwanda
save the name as he goes

kwani kosa lake ni nini?
12/08/2026

kwani kosa lake ni nini?

Dear EX nimekaza, nimeshindwa nashusha mapanga leo  Dear Ex, you still hold a piece of my heart. I've realized my mistak...
12/08/2026

Dear EX nimekaza, nimeshindwa nashusha mapanga leo

Dear Ex, you still hold a piece of my heart. I've realized my mistakes and I'm truly sorry. I miss our laughter, our talks, and our love. I want to make it right and prove my devotion. I'll work hard to regain your trust. Can we start anew? I love you.

LEO AMEKWAMBIA NINI KUHUSU MIMI?K**a kawaida, asubuhi na mapema mtoto wa k**e yupo kiguu na njia kwa watu...Sijui ni umb...
09/08/2026

LEO AMEKWAMBIA NINI KUHUSU MIMI?

K**a kawaida, asubuhi na mapema mtoto wa k**e yupo kiguu na njia kwa watu...

Sijui ni umbea gani leo kabeba, ila asisahau kuhadithia na mazuri yangu...

Kwamaana mara nyingi, kapu lake kuhusu mimi kimekuwa likibeba taarifa za chuki, mbaya na huzuni....

Hapana, mimi sio m'baya kiasi hicho kuna ukurasa mwambie afungue pia utaona mwenyewe...

Sitafuti huruma yako, ila nachotaka kusema kuwa makini na maneno yake ni mazuri kwasasa ila kesho ni sumu...

Je, amewahi kusimulia mabaya yake, au yeye fundi wa mambo ya wengine tu?...

My intake is that rumors may cause you to hate innocent people, and trust the wrong ones be careful..

mchana mwema kwako, ewe ulio mkamilifu

Mugeta 📌

Kamwe hatuwezi kuwasahau walitumlikia, tulipokuwa  kwenye kiza kinene... Kipindi ambacho tuliowategemea na kuwaamini, wa...
07/08/2026

Kamwe hatuwezi kuwasahau walitumlikia, tulipokuwa kwenye kiza kinene...

Kipindi ambacho tuliowategemea na kuwaamini, walisonya walipo ona simu zetu...

Wakati ambao tuliijua leo yetu tu, kesho ilikuwa zaidi ya kibogoyo kupewa muwa atafune...

Mida ile, ambayo machweo hayakuwa miongoni mwa dua zetu...

Walipokuja wao, hatukujuana nao ila walikuwa sababu ya tabasamu hili tena...

Hakika kwa kinywa tunatamka , na kwa yakini na sadiki hatutowasahau daima dawamu...

Pale, mlipo toa kile kidogo Allah akawape jaza inshaaAllah....

Tungeweza kuwataja Kwa majina, lakini tutaandika nathali ngapi ili muenee..

Yote kwa yote, tunasema Alhamdulillah walakul hal...

Mugeta📌

TRUST A WOMAN AT YOUR OWN RISKMwanamke k**a sio mama yako mzazi, usimpe hata sekunde ya uaminifu wako...Samsoni alimpa D...
03/08/2026

TRUST A WOMAN AT YOUR OWN RISK

Mwanamke k**a sio mama yako mzazi, usimpe hata sekunde ya uaminifu wako...

Samsoni alimpa Delila, siri yake ikawa silaha dhidi yake...

Mark Antony alimwamini Cleopatra, mapenzi yakachanganyika na anguko la kisiasa...

Uaminifu ni dhahabu, usimpe kila anayekuita kipenzi...

Adam alimpa sikio Hawa, kilichofuata ni majuto yasiyoisha....

Agamemnon alithubutu kwa Clytemnestra, akarudi nyumbani bila kujua hatima yake....

Heracles alijitoa sana kwa Deianira, zawadi ikageuka kuwa maangamizi katika hekaya....

Historia inatukumbusha, moyo ukiongoza pekee, akili hulipa gharama usithubutu....

King Lear aliamini maneno ya Goneril na Regan, si kila sauti tamu inayokushauri ina nia njema....

Leo mapenzi yanaweza kuwa biashara iliyofichwa nyuma ya tabasamu, leo mtu anaweza kuondoka na kila kitu ulichomkabidhi...
Mwamini mtu kwa matendo, si kwa jina la mapenzi.

WHO UPLIFTS THE UPLIFTERS?Nani huwainua wanaoinua?, kaka kupitia wewe nimejifunza kuwa watu wema wapo bado duniani...Bil...
02/08/2026

WHO UPLIFTS THE UPLIFTERS?

Nani huwainua wanaoinua?, kaka kupitia wewe nimejifunza kuwa watu wema wapo bado duniani...

Bila kuwakosea heshima wahenga, kuandika sijafunzwa na mama ila Dunia imenielewesha....

K**a kesho kitakuja kilele changu kwenye tasnia hii ya nathali, basi nitakuwa na deni kwako....

Ninathubutu kukuita, a brother from another mother, who has never been ready to see me struggling i thank you....

Ukhty Maryam unakiti chako katika safari hii, nipe ruhusa niseme sifa zako ukiwa hai...

Sitaki siku hiyo ngumu ikija, ndiyo nianze kusema ulikuwa mtu muhimu kwangu I want to say it today loudly, proudly and boldly...

Ulisema nenda kwa Jumaa Bin Mbwana japo hayupo hapa nyumbani Tanzania ila atakuelekeza ni mtu poa...

Kwa macho yangu na kwa akili yangu, nathibitisha hukunidanganya nipo sehemu salama kabisa....

Amekuwa msaada mkubwa Kila mara nilipo muhitaji juu ya kukua kwangu, na leo kasema nisiache kuandika...

Ila najiuliza swali, ni nani huwanyanyua wanao nyanyua wengine?

Pindi nawao wanapo hitaji bega la kuegemea? ni nani haswa huwasaidia kusimama...

Sina mali, ila nina moyo wa upendo ahsante mara ishirini na sita...

Address

Mazimbu Morogoro
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Abeid Mugeta posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share