Jaila Ashiri

Jaila Ashiri Journalist

17/03/2026

WATU WAWILI WAFA MAJI NA WANNE WAJERUHIWA KWA RADI MOROGORO.

MOROGORO.

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limetoa taarifa ya watu wawili Kufa maji na wengine wanne kujeruhiwa Kwa kupigwa na radi.

Akizungumza na wanahabari Jana March 16 2026, Kamanda wa polisi mkoani Morogoro SACP Alex Mk**a amewataja waliopoteza maisha ni Hamisi Waziri mwenye umri wa miaka 45 mkulima na mkazi wa Kisaye Morogoro pamoja na Nyerere Kidagati mwenye umri wa miaka 50 mfugaji na mkazi wa Mkonowamara wilaya ya Morogoro walikufa maji walipokuwa wakijaribu kuvuka kwenye maji ambapo maji yaliwazidi Nguvu na kuwasomba hatimaye kusababisha vifo vyao.

Matukio hayo yametokea Mnamo March 14 2026, katika kata ya Tegetero na Mkambarani Wilaya ya Morogoro.

18/02/2026

MWEZI UMEANDAMA RAMADHANI KUANZA KESHO ALHAMIS FEBR 19.

M***i na shekhe mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakar Zubeir ametangaza rasmi kuwa mwezi umeandama leo Jumatano Febr 18 2026, na hivyo siku ya Kesho alhamis Febr 19 mfungo mtukufu wa Ramadhan unaanza rasmi.

Ametaja maeneo yaliyoonekana mwezi ni Dar es salaam, Zanzibar pamoja na Lamu nchini Kenya.

Ramadhan kareem kwa Watanzania Wote.

13/02/2026

ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA MOROGORO FFU WACHANGIA DAMU.

MOROGORO.

Askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia maarufu k**a FFU waliopo Morogoro, wameshiriki katika zoezi la utoaji damu lililofanyika katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo pamoja na kushiriki katika shughuli za usafi katika hospital hiyo.

Akizungumza kwa naiba ya Mkuu wa Kikosi hicho, Mkaguzi wa Polisi Aisha Wesley ameeleza kwamba wamepata msukumu wa kuchangia damu kutokana na umuhimu wake kwani itaenda kuwasaidia watu wengi.

Kwa upande wa Maofisa wa kitengo cha Damu salama cha hospitali hiyo wameshukuru kwa ujio wa askari hao na kuwataka wasiishie siku ya leo badala yake wafanye hivyo mara kwa mara ili kuokoa watu wenye uhitaji.

Ikumbukwe kwamba huu ni muendelezeo wa shughuli za kijamii zinazofanywa na askari wa mkoa wa Morogoro kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Familia ya Polisi itakayofanyika kesho Febr 14 2026.

13/02/2026
06/02/2026

Hekima inamfundisha mtu kuwa na uvumilivu na subira, ambapo ni vitu muhimu sana katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye maisha.

Mtu aliyejaaliwa hekima anatambua ya kuwa mafanikio yanahitaji Muda, Juhudi na uvumilivu mnooo.

Hekima inaweza kuzuia migogoro katika jamii na kuleta Amani.

Tuombe Mungu atupe Hekima na Subira Kwa kila Jambo ili tushinde majaribu na tuweze kufanikiwa.

ULINZI KUIMARISHWA KATIKA MCHEZO WA YOUNG AFRICAN SC DHIDI YA AL AHLY.
30/01/2026

ULINZI KUIMARISHWA KATIKA MCHEZO WA YOUNG AFRICAN SC DHIDI YA AL AHLY.

HATIMAYE CHAMA AREJEA SIMBA SC.Klabu ya Simba Sc leo jumanne Jan 20 2026, wamemtangaza ramsi mchezaji Clatous Chama amer...
20/01/2026

HATIMAYE CHAMA AREJEA SIMBA SC.

Klabu ya Simba Sc leo jumanne Jan 20 2026, wamemtangaza ramsi mchezaji Clatous Chama amerejea katika kikosi cha timu hiyo.

Alipokuwa katika klabu ya Simba Sc Chama alikuwa mchezaji muhimu Sana katika kikosi cha Simba Sc akijulikana kwa uchezaji wake na kufunga mabao, hatua iliyowafanya mashabiki kumuita jina la utani la " Mwamba wa Lusaka" hii ni kutokana na ufanisi wake uwanjani.

Ikumbukwe kwamba Chama alishawahi kucheza kwenye klabu ya Simba Sc na kuisaidia kupata mafanikio kadhaa, kisha baadae Mnamo mwaka 2024 mchezaji huyo alijiunga na klabu ya Yanga Sc jambo lililozua gumzo kwa wanamichezo na kuzuka mijadala kadhaa.

Hatahivyo, ilipofika September 2025, Chama alihama kutoka klabu ya Yanga Sc na kujiunga na klabu ya Singida black stars, na mwaka huu 2026 amerejea tena katika klabu ya Simba Sc.

"Mudawakulisakatakabumbu".

15/01/2026

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAWAKUTANISHA POLISI NA WAFUGAJI MOROGORO.

MOROGORO

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro kupitia kwa Mkuu wa Polisi Jamii mkoa ACP Samuel Kijanga amekutana na Wafugaji wa kijiji cha Kambala kata ya Mkindo wilaya ya Mvomero kwaajili ya kutoa elimu namna ya kuzuia migogoro kati yao na wakulima.

Akizungumza na wafugaji hao jana Jumatano Jan 14 2026, amesema lengo la mkutano huo ni kukomesha mara moja mgogoro unaendelea kati ya kijiji hicho cha wakulima na vijiji jirani ambapo chanzo chake ni kukosekana kwa maeneo ya malisho baada ya maeneo yaliyotengwa kwa ufugaji kuyabadili kuwa kilimo.

YANGA SC YALETA MSHAMBULIAJI WA KATI.Klabu ya Yanga Sc leo alhamis Jan 15 2026, imemtambulisha rasmi mshambuliaji wa Kat...
15/01/2026

YANGA SC YALETA MSHAMBULIAJI WA KATI.

Klabu ya Yanga Sc leo alhamis Jan 15 2026, imemtambulisha rasmi mshambuliaji wa Kati Laurindo Dilson Maria Aurelio Depu.

Depu ni raia wa Angola ambapo awali alikuwa akikipiga nchini Poland na amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga Sc.

ALLAN OKELLO AJIUNGA NA YANGA.Klabu ya Yanga usiku wa kuamkia leo jumanne Jan 13 2026, imemtambulisha rasmi Allan Okello...
13/01/2026

ALLAN OKELLO AJIUNGA NA YANGA.

Klabu ya Yanga usiku wa kuamkia leo jumanne Jan 13 2026, imemtambulisha rasmi Allan Okello kuwa ni mchezaji wa timu hiyo.

Okello ni raia wa Uganda na kabla ya kujiunga na klabu ya Yanga alikuwa akikipiga katika klabu ya Vipers.

Address

Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jaila Ashiri posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share