Banana Fm Tz

Banana Fm Tz Banana FM Radio Banana FM is an urban top 40 radio station, the first of its kind in the Kilimanjaro region which aspires to inspire, entertain and educate

Wizara ya Afya Nchini Tanzania imetoa tahadhari juu ya uwepo wa mafua makali ya Influeza pamoja na UVIKO-19 ( COVID 19) ...
25/02/2026

Wizara ya Afya Nchini Tanzania imetoa tahadhari juu ya uwepo wa mafua makali ya Influeza pamoja na UVIKO-19 ( COVID 19) na kuwataka Wananchi kuchukua tahadhari kubwa.

Taarifa ya Wizara hiyo imesema kutokana na takwimu za ufuatiliaji zilizofanyika kwa kipindi cha mwezi Novemba hadi Aprili ongezeko kubwa la mafua makali ya INFLUEZA na UVIKO-19 hutokea hapa Nchini na Duniani.

Wizara imewataka Watanzania kuchukua tahadhari zifuatazo
— kufunika pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.

— kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono ili kuepuka misongamano isiyo ya lazima.

— Kuvaa barakoa unapokuwa na dalili, unapokuwa karibu na mtu mwenye dalili au ukiwa kwenye maeneo yenye msongamano.

— Kuzingatia usafi binafsi na wa mazingira

— Kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya kupata matibabu stahiki.

— kuepuka kujitibu au kutumia Antibiotiki bila ushauri wa Watalaam wa afya.

Aidha Wizara ya Afya imeeleza magonjwa hayo huambukizwa na kuenezwa kupitia majimaji kutoka kwenye mfumo wa njia ya hewa wa Mgonjwa mwenye maambukizi na husambaa wakati wa kukohoa, kupiga chafya au kuzungumza.

Imeongeza kuwa mafua makali ya Influenza na UVIKO-19 huweza kuenezwa kwa kugusa mazingira yaliyochafuliwa na majimaji yanayotoka kwa mgonjwa ambapo dalili za magonjwa haya ni homa kali, kikohozi, maumivu ya kichwa na mwili, mafua, kuwashwa koo na uchovu.

25/02/2026

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Bi. Mwajuma Abbasy kwa Usimamizi na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Katika Manispaa hiyo.

MOSHI.Daladala zinazofanya safari zake Moshi-Marangu-Kilema, Moshi-Holili na Moshi- Mwika zimegoma kutoa huduma kutokana...
25/02/2026

MOSHI.

Daladala zinazofanya safari zake Moshi-Marangu-Kilema, Moshi-Holili na Moshi- Mwika zimegoma kutoa huduma kutokana na kulalamikia kuvurungwa na bajaji zinatoa huduma Himo-Njia panda wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mgomo huo ambao umetokea tangu leo asubuhi umesababisha adha kubwa kwa abiria waliokuwa wanasafiri kuelekea maeneo mbalimbali.

Akizungumza na madereva wa Daladala na Bajaji hao, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava aliagiza viongozi wa mamlaka ya usafirishaji nchi kavu (Latra) mkoa kukutana na viongozi wa Daladala na Bajaji kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.

"Nielekeze kwa sasa Bajaji nendeni katika kituo chenu mlichokuwa mmepangiwa hapo awali na ninyi Daladala pia nendeni kwenye kituo chenu endeleeni kutoa huduma wakati vikao vitakaa ili kupata suluhu ya kudumu".

Hadi kufika majira ya saa tano asubuhi bado mgomo huo umeendelea huku wananchi wakipata adha ya usafiri.

Leo December 16,2024, kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu ambaye ...
16/12/2024

Leo December 16,2024, kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu ambaye pia ni Mgombea Uenyekiti wa Chama hicho, amesema Watu wasiojulikana wanapanga njama za kumuumiza kisha wamsingizie Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Lisu ameandika akiwataka waache kufanya wanalopanga kwakuwa watamchafua zaidi Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda.

Tundu Lisu ameandika yafuatayo “Enyi Watu wabaya mjulikanao k**a ‘Watu wasiojulikana,’ nimezisikia njama zenu, mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa Chama, Freeman Mbowe, ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe, ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept ‘17 na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka
nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao”

“Ndivyo mavyofanya kila mnapoua Watu wasio na hatia, mnasingizia Watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu, huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani, Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo Bungeni”

“Mkiniumiza k**a mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda mtamchafua zaidi na k**a ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept ‘17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia”

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewataka akina mama wajawazito wanaofika kwenye Kliniki za Uzazi, Mama na Mto kupimwa wingi...
02/05/2023

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewataka akina mama wajawazito wanaofika kwenye Kliniki za Uzazi, Mama na Mto kupimwa wingi wa damu, mkojo kuangalia wingi wa protini, shinikizo la damu pamoja na kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto bila kutozwa gharama zozote.

Haya ameyasema leo wakati wa kukabidhi vifaa tiba vya kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto kwa vituo ishirini vya halmashauri za Mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya Shilingi milioni 45 .

Waziri Ummy amesema kuwa vipimo hivyo ni muhimu kwa wajawazito ili kuweza kuepusha kifafa cha mimba na vifo kwa wajawazito.

“Ili kuweza kumuokoa mama mjamzito anapofika kliniki ni vyema kupimwa vipimo hivyo muhimu, vipimo hivi vyote ni bure na ni lazima viwepo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vyote nchini.

Aidha, waziri Ummy amesema Serikali itahakikisha upatikanaji wa 100% wa dawa za kuzuia kutoka damu wakati wa kujifungua, dawa za kuongeza damu na dawa za kuzuia kifafa cha mimba katika vituo vya afya vya umma nchini.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatimiza wajibu wake kwa kujenga majengo,kuboresha miundombinu, kuongeza ajira pamoja na kununua vifaa tiba , hivi sasa tunapata fedha za dawa kila mwezi shilingi bilioni 20, tutahakikisha hizi dawa tatu zitapatika kwa asilimia 100”. Amesema Mhe. Ummy

Hata hivyo Waziri Ummy amezitaka Timu za afya za uendeshaji za Halmashauri nchini kufanya usimamizi shirikishi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuwajengea uwezo watoa huduma za afya, “Huu ndio muelekeo wa wizara, twende kwenye masuala ya kuwawezesha wataalamu wetu kwenye vituo vya afya na kuona kipi kinafanyika tunaweza kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga k**a tutaongeza kutoa huduma bora za afya”. Alisisitiza.

Akitaja taarifa za Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya na Utafiti wa Kiashiria cha Malaria (DHS/MIS) ya mwaka 2022 zinaonesha kuwa nchi imepiga hatua katika viashiria vingi vya afya vya mama na mtoto mathalani vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimeshuka kutoka 67 kati ya vizazi hai 1000 mwaka 2015/2016 hadi 43 kwa kila vizazi hai 100.

Salaam Ndugu zangu,Kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, ...
02/05/2023

Salaam Ndugu zangu,
Kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, Asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi ,Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda ,Wanachama na viongozi wote waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali, Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa muhimbili na kotenilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu ,AHSANTENI SANA.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa na kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo k**a na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea MUNGU awabariki sana kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea MUNGU AWABARIKI SANA.

Nitakuwa mchoyo wa Fadhila nisipoishukuru Familia yangu Mke wangu ( ), kaka zangu, dada zangu Wadogo zangu na Familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mliomipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻

Ahsanteni
Joseph Haule (Prof. Jay)

❤️❤️❤️❤️

Tunasemaaaaa     .
02/05/2023

Tunasemaaaaa

.

Tunasemaaaaa     .
02/05/2023

Tunasemaaaaa


.

Hakika Tunafuraha Kuendelea kuwa na wewe na Habaki Mtu.
01/05/2023

Hakika Tunafuraha Kuendelea kuwa na wewe na Habaki Mtu.





Jumanne Hii Ndani ya   ni 🔥 Tupo na Odupoi Papaa  Afisa Msimamizi wa Kodi Mkoa wa Kilimanjaro.Mada: Matumizi Sahihiya EF...
01/05/2023

Jumanne Hii Ndani ya ni 🔥 Tupo na Odupoi Papaa Afisa Msimamizi wa Kodi Mkoa wa Kilimanjaro.

Mada: Matumizi Sahihiya EFD,kodi kwa Bajaji na Magari na Usajili wa Maghala.

Weka swali lako litasomwa.



..
22/04/2023

..

14/04/2023

Katika kuhakikisha ushirika unaendelea kusalia katika Mkoa wa Kilimanjaro Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) imeendelea kufanya vizuri katika kipindi Cha miaka miwili mfululizo kwa kufikisha mtaji wa Billioni 4.4 kutoka Billion 2.7 ulivyokuwa Mwaka 2021.

Meneja wa Benki hiyo Godfrey Ng'urah ameyasema hayo April 13,2023 Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza katika Mkutano na wanahabari.

Ng'urah amesema kwa sasa Benki hiyo imeimarika katika soko kwani mpaka sasa vyama vya ushirika kote nchini wamewekeza Billion 3.7 katika katika Benki hiyo ya KCBL.

Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania, Dr Benson Ndiege, amewata Wanaushirika, wadau na wafanyaBiashara kuwekeza kwa kununua hisa katika Benki hiyo.

Cc Banana Fm Tz Esther Machangu

Address

Shanty Town
Moshi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Banana Fm Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Banana Fm Tz:

Share