
27/09/2024
i. Marafiki Wanaoibeza Ndoto Yako
ii. Marafiki Waharibu Maono
iii. Marafiki Wanaoshambulia Ndoto Yako
Aina ya kwanza ya marafiki wanaoua NDOTO.
- Marafiki Wanaoibeza Ndoto Yako.Hawa ni watu ambao hawaamini katika ndoto yako.Ni watu wanaoipuuza na kuidharau ndoto yako.Kwao wanaona k**a unania makuu. Au unaishimaisha dhahania.
- Ukiwaambia ndoto yako watakuambia ni kitu kisichowezekana. Watakuambia wamejaribu wengi na wameshindwa. Wewe ndio hutaweza kabisa hata kufika mbali. Watakubeza kwa kuangalia mwonekano wako. Au kwa kuangalia historia na mazingira yako yasiyo rafiki. Ni marafiki ambao ukiwaruhusu kwa muda mrefu watakufanya uanze kukata tamaa.
- Ukiona una rafiki anayekudharau na kukubeza basi jitahidi kukaa mbali na mtu/watu wa aina hiyo..
Joshua Ngoy Ministries