Kanisa Katoliki Tanzania

Kanisa Katoliki Tanzania SALA NA KAZI

MASOMO YA MISA DESEMBA 13, 2025JUMAMOSI, JUMA LA 2 LA MAJILIOSOMO 1Ybs. 48:1-4,9-11Ndipo aliposimama Nabii Eliya, k**a m...
13/12/2025

MASOMO YA MISA DESEMBA 13, 2025
JUMAMOSI, JUMA LA 2 LA MAJILIO

SOMO 1
Ybs. 48:1-4,9-11

Ndipo aliposimama Nabii Eliya, k**a moto, hata na neno lake likawaka k**a tanuru. Yeye alileta taa juu yao, na kwa juhudi yake akawapunguzia hesabu yao; kwa neno la Bwana akazifungu mbingu, na mara tatu kutoka huko akateremsha moto. Jinsi unavyotisha kwa miujiza yako! Aliye mfano wako aona fahari.

Ukachukuliwa juu katika kisulisuli, katika gari la farasi wa moto. Ukaandikiwa kuwa utaleta makemeo, ili kutuliza hasira siku ile ya Bwana; kugeuza moyo wa baba umwelekee mwana na kuhuisha kabila za Israeli.

Bila shaka wamebarikiwa wale waliokuona kwa macho, wakafa; lakini wewe umezidi kubarikiwa, kwa maana unaishi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 80:1-2,14-15,17-18 (K) 3

(K) Ee Bwana Mungu wetu, uturudishe,
Utuangazishe uso wako, nasi tutaokoka.

Wewe uchungaye Israeli, usikie,
Wewe umwongozaye Yusufu k**a kundi;
Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
Mbele ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,
Uziamshe nguvu zako,
Uje, utuokoe. (K)

Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,
Utazame toka juu uone, uujilie mzabibu huu.
Na mche ule ulioupanda.
Kwa mkono wako wa kuume;
Na tawi lile ulilolifanya,
Kuwa imara kwa nafsi yako. (K)

Mkono wako na uwe juu yake,
Mtu wa mkono wako wa kuume;
Juu ya mwanadamu uliyemfanya,
Kuwa imara kwa nafsi yako;
Basi hatutakuacha kwa kurudi nyuma;
Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako. (K)

SHANGILIO
Lk. 3:4,6

Aleluya, aleluya,
Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake,
Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu,
Aleluya.

INJILI
Mt. 17:10-13

Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, wanafunzi wake wakamwuliza Yesu wakisema: Kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?

Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote; ila nawaambia ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.

Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

MASOMO YA MISA DESEMBA 9, 2025JUMATANO, JUMA LA 2 LA MAJILIOSOMO 1Isa. 40:1 – 11Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu...
09/12/2025

MASOMO YA MISA DESEMBA 9, 2025

JUMATANO, JUMA LA 2 LA MAJILIO

SOMO 1
Isa. 40:1 – 11

Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa, kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.

Sikiliza ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana, nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, na kila mlima na kilima kitashushwa; palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa. Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja, kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.

Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, na wema wake wote ni k**a ua la kondeni. Majani yakauka, ua lanyauka, kwa sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani. Majani yakauka, ua lanyauka, bali neon la Mungu wetu litasimama milele.

Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, panda juu ya mlima mrefu; wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, paza sauti kwa nguvu. Paza sauti yako, usiogope; iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu! Tazameni, thawabu yake I pamoja naye, na ijara yake I mbele zake. Atalilisha kundi lake k**a mchungaji, atawakusanya wanakondoo mikononi mwake; na kuwachukua kifuani mwake, nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 96:1 – 3, 10 – 13

(K) Tazameni, Bwana Mungu atakuja k**a shujaa.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Mwimbieni Bwana, nchi yote.
Mwimbieni Bwana likarikini jina lake,
Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.

Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki,
Atawahukumu watu kwa adili.

Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,
Bahari na ivume na vyote viijazavyo.
Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo,
Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha.

Mbele za Bwana, kwa maana anakuja,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi,
Atahukumu ulimwengu kwa haki,
Na mataifa kwa uaminifu wake.

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Siku ya Bwana i karibu, Tazama atakuja kutuokoa.
Aleluya.

INJILI
Mt. 18:12 – 14

Siku ile, Yesu aliwaambia wafuasi wake. Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliypotea? Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahi huyo Zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea.

Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

MASOMO YA MISA, NOVEMBA 27, 2025ALHAMISI, JUMA LA 34 LA MWAKA WA KANISA SOMO 1.Danieli 6:12-28Ndipo wakakaribia, wakasem...
27/11/2025

MASOMO YA MISA, NOVEMBA 27, 2025
ALHAMISI, JUMA LA 34 LA MWAKA WA KANISA


SOMO 1.
Danieli 6:12-28

Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, k**a ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika.

Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.

Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.

Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.

Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.

Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli.

Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.

Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba.

Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?

Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.

Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.

Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.

Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomsh*taki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.

Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu.

Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.

Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.

Basi Danieli huyo akafanikiwa katika enzi ya Dario, na katika enzi ya Koreshi, Mwajemi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI
Zab. 100 (K) Ufu. 19:9

(K) Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwanakondoo.

Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote,
Mtumikieni Bwana kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba. (K)

Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake. (K)

Kwa kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)

SHANGILIO
Zab. 25:4 , 5

Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.

INJILI
Lk. 21:20-28

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapitilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa. Ole wao wenye miamba na wanaonyonyesha katika siku hizo!

Kwa kuwa kutakuwa na shida katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.

Tena, kutakuwa na ishara katika jua; na mwenye, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazama mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu z ambinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Address

Moshi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kanisa Katoliki Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share