18/12/2025
Unajua night walk ni nini? Umewahi kujaribu? K**a bado, basi ngoja nikuadithie kidogo.
Night walk ni matembezi ya usiku, mara nyingi kuanzia saa moja hadi saa nne, yakitegemea mazingira. Wakati mwingine hufanyika katika maeneo tulivu kabisa, na wakati mwingine katikati ya purukushani—stendi zikiwa zimejaa watu wakipambana kurejea majumbani, kelele za magari, vicheko, mijadala… wewe unatembea ukiwa mtazamaji, ukifurahia maisha yanavyoendelea mbele yako.
Kwa maeneo tulivu, night walk huwa ni tiba ya akili. Ni muda wa kupumzisha kichwa, kupunguza msongo wa mawazo, na kutafakari siku nzima iliyopita. Wengine hufanya kila siku, wengine mara chache—labda mara moja kwa mwezi. Mara nyingi hufanyika maeneo ya fukwe katika mikoa ya pwani, na kwa maeneo yasiyo na beach, hufanyika kwenye barabara tulivu zilizojaa upepo wa usiku na ukimya mtamu.
Mimi binafsi nime-observe mengi. Kuanzia vyakula visivyo rasmi lakini vyenye utamu wa kipekee:
vichwa vya kuku, miguu ya kuku ya firigisi, utumbo, mihogo, viazi vitamu, na ndizi k**a main core — vyote kwa bei nafuu sana. Experience hii imenifungua macho kuona kuwa hata masalia bado yana soko, bado yana thamani, na bado yanabeba ladha isiyoelezeka.
Kwa kweli, tembea usiku uone mengi. Night walk si matembezi tu, ni somo la maisha.
đź’¬Chriss _ mtembezi