Kili new tv

Kili new tv Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kili new tv, TV Channel, Kilimanjaro, Moshi.

03/03/2026

Mambo yameanza kua magumu

02/03/2026

Idadi ya vifo vya raia nchini Israel yazidi kuongezeka kupitia mashambulizi anayoyafanya Iran katika taifa la Israel.

Viongozi wa juu wa Israel wamepiga marufuku kutangaza au kupiga picha mashambulizi anayoyafanya ndani ya Israel.

Lakini tukumbuke Iran alitangaza akasema vita hii ni ya mwisho na katika vita hii nani ataonekana ni mbabe na nani ataonekana ananguvu ndani ya middle east.

Iran amesema hatoacha vita mpaka hahakikishe Israel ameimaliza kabisa.

01/03/2026

: Moja ya tukio kubwa katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo ni goli lililofungwa na Selemani Mwalimu kisha Mwamuzi msaidizi Kassim Mpanga kunyoosha kibendera kuashiria Mwalimu alikuwa oneo la kuotea (Offside)

Ipi ni tafsiri yako katika tukio hilo, goli au siyo goli (Offside?

FT: Yanga 0-0 Simba

01/03/2026

Kikosi kazi cha leo dhidi ya Simba SC


01/03/2026

Picha mbalimbali zikionyesha mwili wa aliyekuwa Kiongozi mkuu wa Iran Ali khemenei baada ya shambulizi la rais wa marekani Donald trump shambulio lililopelekea khnemenei aangukiwe na ukuta na kupoteza maisha

“Leo hii tunakosa kitu kinachoitwa Umma wa Kiislamu kuna nchi nyingi za Kiislamu duniani tupo zaidi ya Waislamu billion ...
01/03/2026

“Leo hii tunakosa kitu kinachoitwa Umma wa Kiislamu kuna nchi nyingi za Kiislamu duniani tupo zaidi ya Waislamu billion mbili duniani lakini neno UMMA halifanyi kazi kwetu kwasababu hatujaungana, neno UMMA hutokana na Watu walioungana na kuelekea njia moja kwa lengo moja, sisi Waislamu hatupo hivyo tumegawanyika na hiyo ndio inasababisha tukaribishe Maadui wengi sana hadi baadhi ya nchi za Kiislamu zinapambana kuungana na Marekani ili wapate msaada”

- Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran (Desemba, 2025)

Toa maoni yako


19/02/2026

Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Said Ally Bungara, maarufu k**a "Bwege," ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha ACT Wazalendo.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma 18 Februari 2026, Bwege ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na hiyari yake mwenyewe k**a mtu huru, baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kugundua kuwa ACT Wazalendo si "rafiki sahihi" katika safari yake ya kisiasa k**a alivyokuwa amefikiria awali.

“ACT Wazalendo si rafiki sahihi kwangu, nilivyofikiria ni tofauti na nilivyohisi. Kuanzia sasa mimi si mwanachama wa ACT Wazalendo tena kuanzia tarehe 18/2/2026. Mengine nitaongea baadaye. Ninategemea kushirikiana na kulitumia jukwaa la CHADEMA katika siasa za kudai demokrasia na maendeleo la taifa langu nilipendalo-Tanzania”, ameandika Bwege. news tv

19/02/2026

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi, hususan barabarani na kwenye njia za waenda kwa miguu, k**a sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila. Maagizo hayo yalitolewa wakati wa ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo, katika hafla iliyohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Chalamila alisema kuanza kwa shughuli katika soko hilo kutaambatana na kufunguliwa kwa barabara zote zinazoingia na kutoka Kariakoo ili ziwe wazi kwa matumizi ya umma. Alisisitiza kuwa ingawa maamuzi hayo yanaweza kuwa magumu kwa baadhi ya wafanyabiashara, ni muhimu kwa ustawi wa jiji, akieleza kuwa haiwezekani kuendeleza miundombinu bora huku barabara zikiwa zimezibwa. Aliongeza kuwa diplomasia itatumika kuhakikisha zoezi hilo linafanyika bila kutumia nguvu.

Februari 17, 2026, matangazo yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Jiji, Elihuruma Mabelya, yalibandikwa Kariakoo yakiwataka wafanyabiashara wote wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi, hususan barabarani na kwenye njia za waenda kwa miguu, k**a sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila Kariakoo, Dar es Salaam Kili new tv

Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo maarufu k**a Ibraline, amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari kati...
19/02/2026

Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo maarufu k**a Ibraline, amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la Kirinjiko, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo imetokea Februari 18, 2026 wakati Mbunge huyo akiwa katika ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt Mwigulu Lameck Nchemba.

Mbali na Mbunge huyo, manusura wengine wa ajali hiyo ni dereva wake pamoja na katibu wake.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Simon Maigwa, amesema kuwa bado hajapata taarifa rasmi za ajali hiyo.

“Nami nimesikia taarifa hiyo, nipeni muda nifuatilie kwa RTO, nitawarudia,” amesema Kamanda Maigwa,

Address

Kilimanjaro
Moshi
5889

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kili new tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category