Macheshafm97.7MHz

Macheshafm97.7MHz RADIO YA KIJAMI
📍MPANDA, KATAVI
✉️ [email protected]
☎️ 0744269838


Jifunze, Elimika, Tabasam,

29/05/2026

Rais Samia atoa milioni 500, ndege maalum kwa Serengeti Boys
🗓️29.05.2026
📍Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ndege maalum aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kwenda Morocco kwa ajili ya kuisafirisha Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON U17), utakaochezwa Juni 2, 2026 nchini Morocco.

Hii ni hatua kubwa ambayo haijawahi kufikiwa na timu yoyote ya vijana chini ya miaka 17 nchini, na inaonesha maendeleo makubwa ya soka la vijana Tanzania.

Mbali na kufuzu fainali, Serengeti Boys pia wameweka rekodi nyingine ya kihistoria kwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia la U17, linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar mwezi Novemba 2026.

Akizungumza leo Mei 29, 2026 jijini Dodoma, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema Serikali imejipanga kuhakikisha timu hiyo inapewa sapoti ya kutosha kuelekea mchezo wa fainali.

Amesema Rais Samia pia ametoa Sh500 milioni kwa kikosi kizima cha Serengeti Boys pamoja na benchi la ufundi k**a pongezi kwa kufika hatua ya fainali.

Aidha, amesema endapo timu hiyo itafanikiwa kutwaa ubingwa, kila mchezaji na viongozi wa benchi la ufundi watapatiwa kiwanja katika eneo la Suluhu New City mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu huyo ameielekeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuratibu safari ya wadau mbalimbali wa michezo, viongozi wa wizara, Shirikisho la Mpira wa Miguu na wabunge, kwenda Morocco kwa ajili ya kuwapa hamasa vijana hao.

“Tunaamini kwamba, kwa kuwa Mheshimiwa Rais ametoa ndege kubwa aina ya Dreamliner, tutakuwa na nafasi ya kubeba kombe na watu wa kwenda kuwapa chachu vijana wetu ili warudi na kombe,” amesema.

29/05/2026

Bunge lampongeza Dkt. Samia kwa uwekezaji sekta ya michezo
🗓️29.05.2026
📍Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limempongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya michezo ambao umeendelea kuzaa matunda kupitia mafanikio ya timu mbalimbali za taifa katika mashindano ya kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa leo Mei 29, 2026 na wabunge mbalimbali wakati wakichangia baada ya Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya wakati kuwasilisha hoja bungeni kuhusu Azimio la Bunge la kuipongeza timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya AFCON 2026 inayoendelea nchini Morocco pamoja na kufuzu kushiriki Kombe la Dunia la vijana chini ya umri huo mwaka 2026.

Akiwasilisha hoja hiyo, Bulaya alisema uwekezaji wa Dkt. Samia katika michezo umewezesha Tanzania kupata mafanikio makubwa katika timu mbalimbali za taifa.

“Hivi tunavyozungumza, Serengeti Boys wameingia fainali na kufuzu Kombe la Dunia. Pia Tanzanite Queens (U-20) imefuzu kushiriki michuano ya dunia, huku Twiga Stars ikipewa nafasi ya kushiriki michuano ya wanawake Afrika (WAFCON),” alisema Bulaya.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge mbalimbali waliotumia nafasi hiyo kupongeza juhudi za Serikali katika kukuza michezo nchini pamoja na kuweka mazingira bora kwa vijana kuendeleza vipaji vyao.

28/05/2026

Dkt Samia:Nitajenga hospitali maalumu ya mama na mtoto Kurasini
🗓️28.05.2026
📍Dar es Salaam
Katika kusogeza huduma karibu za uzazi, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema atajenga hospitali maalumu ya mama na mtoto, eneo la Kilwa Road Kurasini, ili kurahisisha upatikanaji wa matibabu.
Ujenzi huo ni mwendelezo wa uboreshaji wa sekta ya afya katika hospitali ya polisi iliyopo katika hilo, wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.
Ameeleza hayo leo Alhamisi, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kozi namba 1/2025/ 2026 ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.
“Wakati nikinongo’na ndani kule na IGP, alinieleza haja kuwa na hospitali maalumu ya kina mama na watoto, pale katika hospitali ya Kilwa Road. Nami nimemuhakikishia hospitali umeipata, hospitalia umeipata na nakusudia itajengwa hivi karibuni,” amesema.

28/05/2026

IGP Wambura: Dkt Samia ametutoa kwenye vibanda, katujengea maghorofa
🗓️28.05.2026
📍Dar es Salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ( (IGP), Camillius Wambura katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jeshi hilo limepiga hatua kubwa ikiwemo maboresho ya makazi kutoka kwenye vibanda vya mabati hadi nyumba za kisasa za askari hao.

IGP Wambura amesema makazi ya askari yalikuwa katika mazingira magumu ikiwemo kuishi katika vibanda vilivyojengwa kwa mfumo wa mabati mithili ya nyumba za wavuvi wa samaki.

Wambura amesema hayo leo katika hafla ya kufunga mafunzo ya kozi namba 1/2025/ 2026 ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam yaliyohudhuriwa na Dkt Samia.

“ Mheshimiwa Rais yale yamejengo ulioyaona pale kwenye slide si kambi za wavuvi, bali ni makazi ya polisi ambayo askari walilala humo na kwenda kulinda raia na mali zao.Majengo hayo yameisha kwa muda mrefu, lakini wewe umeyakataaa.

“ Umetoa fedha na kuhakikisha majengo ya kisasa ya makazi ya askari yanajengwa hasa maghorofa, hii imeondoa hata yale makazi ambayo hata wavuvi wasingeweza kukaa.

Amesema “ sisi ni kina nani tusisimulie hadithi hii? Au kina nani tusiokuwa na roho ya shukrani ya kusimulia hadithi hii, mheshimiwa Rais asante sana,” amesema IGP Wambura.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi, amesema mabadiliko hayo yaliyofanywa na Dkt Samia yataachaa alama kubwa ndani ya jeshi la polisi na vizazi vijavyo sambamba na kuweka kumbukumbu ndani ya jeshi hilo.

Ameeleza kuwa uongozi wa Dkt Samia umewezesha pia Jeshi la Polisi kupata vyombo mbalimbali vya usafiri, yakiwemo magari ya kisasa sambamba ajira mpya katika jeshi hilo, upandishaji wa vyeo kwa askari na ujenzi wa vituo vya kisasa vya polisi.

28/05/2026

Dkt Samia: Jeshi la Polisi lijenge imani kwa wananchi
🗓️25.05.2026
📍Dar es Salaam
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura, kuangalia namna jeshi hilo litakavyojenga imani yake kwa wananchi, sekta binafsi na jumuiya za kimataifa zilizopo hapa nchini.

Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo, akirejea utafiti uliochapishwa na Shirika la Afrobarometer hivi karibuni, ukihusisha wananchi wa Afrika na imani kwa Jeshi la Polisi.

Kupitia utafiti huo, wananchi hao walihojiwa endapo watapata shida ya kisheria, imani yao ikoje kwa Jeshi la Polisi na ripoti imeonyesha asilimia 12 pekee ya Watanzania waliohojiwa walisema watakimbilia polisi.

Katika nchi 38 za Afrika zilizohusishwa kwenye utafiti huo, moja pekee ndiyo ilikuwa na alama za juu yaani asilimia 25, kwamba raia wakipata shida watakimbilia polisi.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo kwa IGP Wambura, leo Mei 28, 2026 wakati akihitimisha Mafunzo ya Maofisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, Kurasini, Dar es Salaam leo Mei 28, 2026.

Amesema taarifa hizo si za kuzibeza, bali ni kuangalia changamoto zilipo hadi wananchi wajibu hivyo na zifanyiwe kazi.

“Tunataka kuona namna Jeshi la Polisi linavyojenga imani yake kwa wananchi na sekta binafsi na jumuiya za kimataifa zilizopo nchini. Hapa tunaangalia legitimacy (uhalali) ya polisi,” amesema.

27/05/2026
26/05/2026

Wabunge:Hakuna ubaguzi wa dini, Tanzania ina uwezo kushughulikia changamoto za ndani

🗓️26.05.2026
📍📍Dar es Salaam
Baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamesema Tanzania hakuna ubaguzi wa dini, huku wakitayataka mataifa ya nje kuliheshimu Taifa hili ambalo linaweza kushughulikia changamoto zake za ndani.
Kauli za wawakilishi wa wananchi zinaunga mkono kile kilichosemwa asubuhi na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), kwamba Tanzania hakuna ubaguzi wa dini na viongozi dini mbalimbali wanaishi katika misingi ya amani, utulivu na upendo.
Chimbuko la suala hilo ni muswada uliowasilishwa kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje Marekani na maseneta wawili wanaotaka wanapendekeza Marekani kufanya tathmini mpya ya ushirikiano wa masuala mbalimbali ikiwemo ya kiusalama, kiuchumi na kidiplomasia baina ya taifa hilo na Tanzania.
Wabunge hao wameeleza hayo leo Jumanne Mei 24,2026 wakati wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Ikungi Magharibi mkoani Singida, Elibariki Kingu amesema Tanzania kuna wastani wa makanisa yasiyopungua 4,000 kati yao asilimia 98 ya nyumba hizo za ibada zinamilikiwa na mtu mmoja mmoja mbali na yale yanayomilikiwa na taasisi.
“Kusema Tanzania kuna ubaguzi wa kidini hapana…Wakati chini uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tumeshuhudia kuna uhuru mkubwa wa kuabudu. Leo Rais anakwenda katika kanisa na kuendesha harambee au Muislamu anakwenda kanisa kufanya harambee,”
“Mheshimiwa Spika Taifa hili halina mambo ya kutesana kidini, ndio maana leo tunazungumza pembeni yangu ameketi mbunge Muislamu, pembeni yangu amekaa mbunge Mkristo,” amesema Kingu.
Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amesema Tanzania ni Taifa huru linalopaswa kuheshimiwa hata linapopitia changamoto zake za ndani.
“Tupo huru, tunathamini mchango wao, lakini muhimu wakumbuke wasitumie changamoto tulizonazo kutuumiza, kutunyanyasa na kutukandamiza,”
“Uhusiano wa Tanzania na mataifa ya nje unapaswa kuheshimu uhuru na mamlaka ya nchi na kuiitaka Serikali kuchukua hatua za kidiplomasia kumaliza mvutano huo,” amesema.

26/05/2026

Dkt Samia:Majaji toeni uamuzi wa hukumu bila huba wala chuki

🗓️26.05.2026
📍Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amewaapisha majaji tisa wa Mahak**a ya Rufani ya Tanzania, akiwataka kwenda kuimarisha utendaji wa haki na kulinda uhuru wa mhimili huo nchini.
Pia, Dkt Samia amewaambia majaji hao, wamepata uteuzi huo kutokana uzoefu, weledi na utumishi utumishi waliounyesha katika nafasi zao mbalimbali walizotumikia Mahak**a.
Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumanne Mei 26,2026 Ikulu ya Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaapisha majaji hao aliowateua hivi karibuni.
“Hii ni ishara ya kuwa mmefanya kazi nzuri na Tume ya Utumishi ya Mahak**a imeitambua kazi yenu na imewapendekeza kupandishwa katika ngazi hii,” amesema Dkt Samia na kuongeza kuwa;
“Imani yangu kwamba kwa heshima hii mliyopewa mtafanya kazi kwa bidii zaidi, nendeni mkaongeze nguvu kwenye Mahak**a ya Rufani, kwa kutambua umuhimu wa haki k**a msingi wa amani, utulivu, maendeleo ya Taifa na ustawi wa wananchi kwa ujumla,” amesema.
Amewataka majaji hao kwenda kuitumikia nchi kwa weledi na uzalendo k**a walivyokula kiapo,”mmeapa mtafanya kazi bila upendeleo, huba na chuki. Kuna haka ka huba na kachuki sijui… nataka mkatizame vizuri ndani yenu katika kutoa uamuzi wa hukumu zenu,”
Amewaambia majaji hao kuwa dhamana hiyo si ya cheo tu, bali kulinda haki za Watanzania, na katika maamuzi wanayoyafanya, wakumbuke kuwatumikia wanadamu ni kumtumikia Mungu.
“Nimeshawaambia mara kadhaa, kwa hapa duniani ukiacha Mungu anayesimamia haki za wote, wengine ambao Mungu amewateua kusimamia haki za wenzenu ni nyinyi majaji katika ngazi tofauti. Kwa hiyo mnafanya kazi kubwa, hivyo mnadhima kubwa katika nchi katika kutenda haki,” amesema.

Benki ya Dunia:Tanzania inatumia vizuri fedha za miradi ya maendeleo🗓️25.05.2026 📍Benki ya Dunia (WB), imeipongeza Serik...
25/05/2026

Benki ya Dunia:Tanzania inatumia vizuri fedha za miradi ya maendeleo
🗓️25.05.2026
📍
Benki ya Dunia (WB), imeipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na taasisi hiyo.
WB imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa mataifa yanayoitekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi katika bara la Afrika.
Pongezi hizo zilitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkazi wa WB anayemaliza muda wake nchini, Nathan Belete, alipokutana na Dkt Samia Ikulu ya Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Belete amesema “miradi ya Tanzania ndani ya Benki ya Duniani ni miongoni mwa inayotekelezwa vizuri barani Afrika. Fedha zinazotolewa kwa Tanzania zinatumika vizuri na kuleta matokeo,” ameeleza.

Belete amesema katika kipindi chote alichofanya kazi Tanzania, ushirikiano kati ya Serikali na WB umeendelea kuimarika katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, afya, maji, nishati, miundombinu, hifadhi ya jamii na mageuzi ya kisera.

Rais Dkt Samia amemshukuru Belete kwa mchango wake tangu alipoanza majukumu yake Novemba 2022, akisema ushirikiano wake umeendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na WB katika kusukuma mbele ajenda za maendeleo.

Dkt Samia amesema,” Kwa sasa Tanzania inatekeleza programu na miradi 18 kwa ushirikiano na Benki ya Dunia katika sekta za usafirishaji, nishati, maji, elimu, maendeleo ya miji, hifadhi ya jamii, mageuzi ya kisera na ustahimilivu wa tabianchi,” amesema Dkt Samia.

19/05/2026

Arsenal 🏆

Address

Madukani
Mpanda
11503

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Macheshafm97.7MHz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share