JAMII FM RADIO

JAMII FM RADIO JAMII FM ni kituo cha redio cha kijamii kilichoanza kutoa huduma mwezi Septemba 2016 kwa lengo la kuwapa jamii jukwaa la kuzungumzia maendeleo yao.

JAMII FM RADIO haitawajibika kwa maoni yatakayotolewa yenye kukiuka sheria za nchi. JAMII FM is a Community Radio that was launched in September 2016 for the purpose of giving community members particularly from rural areas access to information and means of communication. The programmes are basically focused on issues that directly or indirectly reflects community livelihood including people with

special needs. Through Jamii FM Radio, educational and developmental information is disseminated and exchanged; important local issues are aired; a free market place of ideas and opinions is opened up and people are given the opportunity to express themselves. Broad participation by community members is always encouraged in Program production. JAMII FM RADIO gives voice to the voiceless. Vision
The VISION of Jamii FM is to see the community of Lindi and Mtwara Regions particularly from rural areas have access to information and increased capacity to play a meaningful role for their own development through media. Mission
The MISSION is to enable local communities to use media as a tool for enhancing participatory communication in order to achieve sustainable rural development. Location
JAMII FM Radio Station is located at Naliendele area 9km from Mtwara Town along Mtwara-Newala road. The station is opposite to Naliendele Agriculture Research Institute. Coverage:
JAMII FM RADIO owns its 60 metres transmission tower that enables to reach the huge population from both Mtwara and Lindi regions, from Mtwara Municipal up to Nanyamba, Tandahimba, Newala, Nachingwea, Lindi and some parts along the boarder with neighbouring country-Mozambique. Programme Schedule
0600 – 1000hrs – Dira ya Asubuhi
1000 – 1300hrs – Kapu la Jamii
1300 – 1600hrs – Mchakamchaka
1600 -- 1610hrs – Habari (News Bulletin)
1610 – 1800hrs – Sauti ya Jamii
1800 – 1900hrs – Radio France International (RFI)
1900 – 1910hrs – Habari (News Bulletin)
1910 – 2000hrs – Dimba la Michezo (Sports)
2000 – 2100hrs – Makala Maalum
2100 – 2200hrs – Usiku Mwema
2200 – 0000hrs – Love Boat
0000 – 0600hrs – Music Mix

Location
https://www.google.co.tz/maps/place/Jamii+Fm+Radio/@-10.3559624,40.1615128,17z/data=!3m1!4b1!4m5!3m4!1s0x188d5a1f07878dd3:0x3a55ced2bafdf73e!8m2!3d-10.3559624!4d40.1637015?hl=en&hl=en

Wanafunzi sasa ni mtelezo hasa inapofika muda wa kujisomea baada ya kuzinduliwa kwa umeme, Bonyeza hapo kwenye picha ili...
25/07/2026

Wanafunzi sasa ni mtelezo hasa inapofika muda wa kujisomea baada ya kuzinduliwa kwa umeme, Bonyeza hapo kwenye picha ili kusoma zaidi.....

Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi amewasha umeme katika Shule ya Sekondari Mtiniko, Nanyamba, na kusema Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 203 kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vya Mkoa wa Mtwara Na Musa Mtepa Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius…

Kikosi kazi cha kupambana na Uhalifu wa usafirishaji haramu wa Binadamu Mkoa wa Mtwara kimeaswa kuwajibika kwa vitendo i...
24/07/2026

Kikosi kazi cha kupambana na Uhalifu wa usafirishaji haramu wa Binadamu Mkoa wa Mtwara kimeaswa kuwajibika kwa vitendo ili kutokomeza kabisa tatizo hilo.

Akizungumza Leo Julai 24, 2026 kwenye ukumbi wa Hoteli ya Luwa wakati wakifunga semina ya siku mbili, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mtaki Kurwijila amesema kikosi kazi hicho kinatarajiwa kufanya kwa vitendo yale waliyofundishwa wakati wa Semina.

ACP Kurwijila amesema kikosi kazi hicho, kinapaswa kwenda kuchukua hatua stahiki za usafirishaji haramu wa Binadamu kabla ya kusubiri matokeo ya tatizo kutokea.

Ameongeza kuwa, Kikosi kazi kiende kusaidia Jamii katika kupata elimu ya namna ya Kuzuia,kulinda na namna ya kushughulikia taarifa au matukio ya Usafirishaji haramu wa Jamii kwenye ngazi zao, ikiwemo kutoa taarifa kwa vyombo husika.

ACP Kurwijila amesema katika Mkoa wetu changamoto hizo za usafirishaji haramu zipo na Jamii inaweza ikawa inafanyaka kwa kujua au kwa kutokujua, hivyo wanapaswa kukemea na kuacha kabisa kufanya matendo hayo haramu.

Nao baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho cha Mkoa, wamesema wataenda kuwajibika ipasavyo kulingana na mafunzo waliyopata na wameomba ushirikiano kutoka kwa Jamii hasa pale wanapohitaji ufafanuzi au kuhitaji Taarifa kutoka kwao.

Semina hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na CVM kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Sekretarieti ya kupambana na usafirishaji Haramu wa Watu (ATS) kwa ufadhiri wa serikali ya Itali, ambao umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta za Serikali na Asasi za kiraia.

Furaha zimetawala wilaya ya Newala kwa kuishukuru serikali kwa umeme wa kV 33
23/07/2026

Furaha zimetawala wilaya ya Newala kwa kuishukuru serikali kwa umeme wa kV 33

Wananchi wa Newala wameishukuru Serikali kwa kuzindua laini ya umeme wa kV 33 kutoka Masasi hadi Newala, wakisema itaimarisha shughuli za kiuchumi, kuongeza uzalishaji wa wajasiriamali na kuboresha huduma zinazotegemea umeme wa uhakika Na Musa Mtepa Wananchi wa Wilaya ya…

Wadau kutoka Taasisi mbalimbali Mkoani Mtwara wameaswa kuimarisha ushirikiano katika kupambana na usafirishaji Haramu wa...
23/07/2026

Wadau kutoka Taasisi mbalimbali Mkoani Mtwara wameaswa kuimarisha ushirikiano katika kupambana na usafirishaji Haramu wa Binadamu, kupitia kutoa elimu kwa wananchi na utaratibu wa pamoja wa hatua za kisheria na utendaji.

Wito huo umetolewa Leo Julai 23, 2026 Mkoani Mtwara na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt Benedicto Ngaiza wakati akifungua semina ya kuhusu Usafirishaji haramu wa Binadamu na Uhamiaji salama.

Dkt Ngaiza amesema, Usafirishaji haramu wa Binadamu ni uharifu mkubwa unaokiuka haki za Binadamu na kuvunja utu wa Mwanadamu.

Ameongeza kuwa uhalifu huu unathiri sana Wanawake, Watoto, vijana pamoja na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi.

Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema, imekuja kwa wakati muafaka na ni muhimu sana na ni mambo ambayo yamekuwa yakitokea kwenye Jamii zetu na Kuna wakati wananchi wanafanya kwa kujua na kutokujua.

"Kuna vijana waliletwa na kushawishiwa kutoka Dar es Salaam na walihaidiwa kuja kufanya kazi hapa Mkoani Mtwara, lakini walivyofika ile kazi waliyohaidiwa hawakupata, ndipo kijana mmojawapo, alimtumia ujumbe baba yake kuwa tangu wamefika hapa hakuna kazi yeyote inayoendelea naomba nitumie hela ya chakula, sababu aliyewashawaishi aliwaambia waje na hela zao na wakifika watarudishiwa, lakini baada ya kufika, aliwazungusha na bila kuwarudishia hela zaidi ya mwezi, ndipo baba wa kijana huyo alipiga simu na akatueleza sehemu alipo huyo kijana na tukampata huyo mtu aliyewaleta na tukamwambia awarudishe vijana wote 30 na kurudishwa Dar es Salaam" amesema Bahati Sendela Naibu Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mtwara.

Semina hiyo imeandaliwa na shirika la CVM kwa ufadhili wa serikali ya Italia kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Sekretarieti ya kupambana na Usafirishaji Haramu wa Watu (ATS) ambao imewashirikisha wadau kutoka vyombo vya ulinzi na Usalama, Mahakama, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Uhamiaji, Maafisa Ustawi wa Jamii, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Serikali Wawakililishi wa Asasi za kiraia.

Wilaya ya Newala sasa kuanza kwa fursa mpya zitokanazo na Umeme
22/07/2026

Wilaya ya Newala sasa kuanza kwa fursa mpya zitokanazo na Umeme

Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi amezindua laini ya umeme ya kilovoti 33 kutoka Masasi hadi Newala, mradi utakaoboreshwa upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi wilayani humo Na Musa Mtepa Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo Julai…

KIPAZA CHA LEO 🎤Kumekuwa na baadhi ya watu wenye ulemavu wanawatumia watoto wadogo katika kuomba misaada" Jamii Inazungu...
16/07/2026

KIPAZA CHA LEO 🎤
Kumekuwa na baadhi ya watu wenye ulemavu wanawatumia watoto wadogo katika kuomba misaada" Jamii Inazungumziaje ili swala.
MCHAKAMCHAKA SHOW
Thursday 😄
Host Buda 🎤

https://radiotadio.co.tz/jamiifm

Sikiliza Jamii FM Radio kupitia kiunganishi kilichopo hapo juu

KIPAZA 🎤Ebu tuambie ukweli kati ya muziki wa singeli na muziki wa hip-hop upi unafanya vizuri sana kwenye majukwaa makub...
15/07/2026

KIPAZA 🎤
Ebu tuambie ukweli kati ya muziki wa singeli na muziki wa hip-hop upi unafanya vizuri sana kwenye majukwaa makubwa hapa nchini.
MCHAKAMCHAKA SHOW
Host Buda
https://radiotadio.co.tz/jamiifm

Sikiliza Jamii FM Radio kupitia kiunganishi kilichopo hapo juu

Wanachama wa MFICO’S Msangamkuu wameiomba serikali kukamilisha vifaa vya boti ya mkopo yenye thamani ya zaidi ya Sh mili...
14/07/2026

Wanachama wa MFICO’S Msangamkuu wameiomba serikali kukamilisha vifaa vya boti ya mkopo yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 102, wakisema upungufu wa vifaa umewazuia kuanza uvuvi na kurejesha mkopo. Kusoma kwa undani wa habari hii bonyeza picha hapo chini.......

Wanachama wa MFICO’S Msangamkuu wameiomba serikali kukamilisha vifaa vya boti ya mkopo yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 102, wakisema upungufu wa vifaa umewazuia kuanza uvuvi na kurejesha mkopo Na Musa Mtepa Wanachama wa Chama cha ushirika cha msingi…

KIPAZA 🎤Unafahamu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari.Twenzetu pamoja kitaa kimeongea kwenye kipaza 🎙️MCHAKAMCHAKA SH...
14/07/2026

KIPAZA 🎤
Unafahamu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari.
Twenzetu pamoja kitaa kimeongea kwenye kipaza 🎙️
MCHAKAMCHAKA SHOW
HOST Buda
https://radiotadio.co.tz/jamiifm

Sikiliza Jamii FM Radio kupitia kiunganishi kilichopo hapo juu

Usikose kusililiza kipindi cha Dira ya Asubuhi tarehe 14.07.2026...Tuma maoni na ujumbe wako utasomwa kwenye kipindiChil...
13/07/2026

Usikose kusililiza kipindi cha Dira ya Asubuhi tarehe 14.07.2026...Tuma maoni na ujumbe wako utasomwa kwenye kipindi
Children in Crossfire
Utpc TZ
Tanzania ECD Network
Ikulu Mawasiliano
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Wizara ya Afya

Address

Naliendele, Mtwara/
Mtwara

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JAMII FM RADIO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to JAMII FM RADIO:

Share

Category