16/12/2025
*KINACHOSABABISHA MENO KUTOBOKA*
Kitaalam huitwa dental cavity.
Hii ni hali ya jino kuwa shimo. Shimo hili kwenye jino huanza taratibu na huendelea kutanuka k**a halitatibiwa mapema. Mwanzo wa hili tatizo huwa kunakua hakuna dalili yeyote ambayo mtu anaipata na hivyo ni vigumu kufahamu k**a ana changamoto mwanzoni.
*Dalili za meno kutoboka*
1. Meno kupata ganzi
2. Meno kutengeneza alama kwenye sehem ya juu ya jinoe
3. Maumivu ya jino wakati umetulia, ukila vyakula au kunywa vinywaj vyamoto
4. Uwepo wa shimo kwenye meno
5. Utando mweusi kwenye jino
*Nini sababu ya meno kutoboka*
1. Maambukiz ya bacteria wabaya kwenye kinywa na meno.
2. Upungufu wa vitamin kwenye lishe( A, E na Vitamin D)
3. Matumizi makubwa ya vyakula vyenye asili ya tindikali
4. Upungufu wa madini k**a vile calcium , magnesium na phosphorus
5. Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi
*KUMBUKA*
Kila mtu ana bacteria kwenye kinywa ambao ni wazuri na hulinda afya ya kinywa. Bacteria hawa hubadili mabaki ya chakula kuwa tindikali , hii tindikali ndio huanza kumomonyoa jino na kuruhusu bacteria kushambulia jino.
Ndio maaana unashauliwa kusafisha kinywa si chini ya mara mbili kwa siku ili kuzuia kuzalishwa kwa tindikali kinywani
*HATUA ZA KUZUIA MENO KUTOBOKA*
๐ค๐ปEpuka vyakula vya sukari kwa wingi.
Sukari ndio sababu namba moja kwenye visababishi vya meno kutoboka, pia ni chanzo cha magonjwa mengine k**a vile: Uzito mkubwa kupita kiasi, kitambi, pressure, magonjwa ya moyo na kuvurugika kwa hormones mwilini.
๐ค๐ปPunguza matumizi ya vyakula vyenye tindikali nyingi. Mfano soda, juice zilizo sindikwa, vyakula vya kukobolewa na kusafishwa, matunda k**a limao kwa wingi.
๐ค๐ปTumia mazao ya maziwa na vyakula vyenye virutubisho kwa wingi...
*TIBA YA MENO KUTOBOKA*
1. Kutokana na sababu ambazo huleta changamoto ya meno kutoboka. Tiba yake htegemea mambo yafuatayo
2. Pata lishe kamili na punguza sana vyakula ambavyo pelekea tatizo
3. Usafi wa kinya angalau mara 2 kwa s