Swahili News Hub

Swahili News Hub Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Swahili News Hub, Media/News Company, PO BOX 92, Mtwara.

Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini m...
30/03/2026

Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders - POE), na Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan Kusini, amekutana leo na timu ya mpira wa kikapu ya Dar City inayoshiriki Michuano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basketball Africa League (BAL) 2026, inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Katika mazungumzo na timu hiyo iliyoambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabit pamoja na Viongozi wengine kutoka Serikalini, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ameipongeza Timu ya Dar City kwa kufikia hatua hiyo muhimu ya mashindano, akieleza kuwa mafanikio hayo ni ishara ya kukua kwa kiwango cha mpira wa kikapu nchini Tanzania.

Aidha, amewatia moyo na kuwapa ari wachezaji ya kupambana katika mchezo wao mmoja uliosalia kabla ya kufika fainali, akisisitiza umuhimu wa nidhamu, kujituma na kujiamini wanapoingia uwanjani. "Kwa hatua mliyofikia, nina imani kabisa mnaweza kutinga fainali na hatimaye kubeba kombe hili, labda itokee miujiza", alisema Dkt. Kikwete akizungumza na wachezaji hao.

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete, ambaye amewahi kuwa mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) huku akiwa mstari wa mbele katika kuendeleza mchezo huo wakati wa uongozi wake, ametumia fursa hiyo pia kutoa pongezi kwa dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaofanyika katika sekta ya michezo nchini. Aidha, ameipongeza Wizara yenye dhamana ya kusimamia Michezo pamoja na Shirikisho la TBF kwa kusimamia vizuri maendeleo ya mpira wa kikapu, huku akibainisha kuwa mafanikio ya timu ya Dar City ni mojawapo ya matunda ya Serikali kuwekeza katika michezo.

Mheshimiwa Dkt. Kikwete yupo nchini Afrika Kusini kwa ziara ya kikazi ambapo amekutana na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, k**a sehemu ya kutekeleza majukumu yake ya kikanda akiwa k**a Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la SADC, pamoja na jukumu lake jipya chini ya Umoja wa Afrika la kusaidia kutafuta suluhu ya mgogoro wa Sudan Kusini.

๐—ง๐—”๐—ก๐—ญ๐—œ๐—”: Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Seleman Bungara almaarufu Bwege amefariki Dunia mchana huu, akiwa kwen...
30/03/2026

๐—ง๐—”๐—ก๐—ญ๐—œ๐—”: Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Seleman Bungara almaarufu Bwege amefariki Dunia mchana huu, akiwa kwenye Hospitali moja ya binafsi huko Kigamboni, Dar es Salaam,

Kwa mujibu wa Abbas S.A. Bungara ambaye ni Kaka wa marehemu, ambapo amesema marehemu alifikishwa Hospitalini hapo kwaajili ya kufanyika Dialysis k**a ilivyokuwa ikifanyika kawaida, na ndipo umauti ulivyomfika,

Amesema kwa sasa mipango ya mazishi inaendelea, na taarifa zaidi zitatolewa hapo baadae ila msiba (kwaajili ya watu kuhani) ni Temeke nyumbani kwa Abbas Bungara,

Enzi za uhai wake marehemu Bwege amewahi kutumikia vyama vya siasa vya CUF, ACT Wazalendo na hivi karibuni alitangaza kujiunga na CHADEMA, ingawa mchakato rasmi wa kukabidhiwa kadi ya chama hicho ulikuwa haujakamilika.


# WorldNews
# TRT

Video ya Rais wa Rwanda Paul Kagame akiagiza baadhi ya maafisa wa serikali kusimama wakati wa hotuba yake Machi 23, 2026...
30/03/2026

Video ya Rais wa Rwanda Paul Kagame akiagiza baadhi ya maafisa wa serikali kusimama wakati wa hotuba yake Machi 23, 2026 imesambaa mitandaoni.

Akionekana kukasirika, Kagame aliwaambia maafisa hao kusimama kwa sababu baadhi yao walikuwa "wanalala" wakati yeye akizungumzia kuhusu masuala muhimu ya utendakazi wao na maslahi ya wananchi.

Katika hotuba yake, Kagame alieleza kuhusu makosa ya taasisi za umma, kutotafuta wafanyakazi hodari, kutozingatia vipaumbele mahsusi, matumizi mabaya ya raslimali za umma, na kushindwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya serikali.

Hali hii ilijitokeza katika Chuo Cha Kijeshi cha Rwanda huko Gako, kilichoko Mkoa wa Mashariki nchini humo.

Idadi ya wanajeshi wa Israeli waliopoteza maisha tangu shambulio la kuvuka mpaka lililoongozwa na Hamas la tarehe 7 Okto...
29/03/2026

Idadi ya wanajeshi wa Israeli waliopoteza maisha tangu shambulio la kuvuka mpaka lililoongozwa na Hamas la tarehe 7 Oktoba 2023 imefikia 930.
Cc: NEW YORK POST

MICHEZO๐Ÿšจ Viongozi wakuu wa Real Madrid wanaamini kwamba sasa ni wakati wa klabu kuanza tena kuwekeza kwa wachezaji ambao...
29/03/2026

MICHEZO
๐Ÿšจ
Viongozi wakuu wa Real Madrid wanaamini kwamba sasa ni wakati wa klabu kuanza tena kuwekeza kwa wachezaji ambao tayari ni wa kiwango cha dunia, na kwa muda fulani waachane na mkakati wa kutegemea zaidi vipaji vya vijana.

Miongoni mwa majina makubwa na yaliyokomaa ambayo wamekuwa wakiyafuatilia, Rodri ndiye mwenye mafanikio zaidiโ€”anaonekana k**a mchezaji anayeweza kuleta mchango wa haraka mara moja.

Address

PO BOX 92
Mtwara

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Swahili News Hub posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share