25/08/2025
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa , , ametangaza kuwa tamasha la mwaka huu la Simba Day litakuwa na tukio maalum la kuwaaga rasmi wachezaji wawili wa zamani waliotoa mchango mkubwa kwa klabu hiyo — John Raphael Bocco na Jonas Mkude.
Ahmed Ally amesema:
“Siku ya Simba ni nafasi kubwa ya kuwapa heshima watu waliofanya makubwa ndani ya Simba. Tunatambua, tunakumbuka na tunathamini mchango wao. Mwaka huu kwenye Simba Day tutawaalika wachezaji wetu wawili wa zamani ambao wamefanya makubwa ndani ya Simba yetu.”
Kuhusu Bocco, Ahmed alisema: “Nahodha wetu wa zamani ambaye amedumu Simba kwa miaka 6, ametupa makombe 4 na kutupeleka Robo Fainali mara 4. Kwa sasa amestaafu rasmi soka hivyo ni nafasi ya sisi kumpa shukran John Raphael Bocco.”
Na kuhusu Jonas Mkude, alisema: “Siku hiyo hiyo tutaenda kumuaga nahodha wetu mwingine aliyeitumikia Simba kwa miaka 15. Ameondoka mwaka juzi lakini hatukupata nafasi ya kumuaga. Hii ni fursa ya kipekee kwetu kumuaga kipenzi chetu Jonas Mkude.”