Musoma Tv

Musoma Tv Musoma Tv is a Digital Multmedia Storytelling for Local News with the Public Interest.

17/09/2025

Tukomeshe Ndoa za Utotoni!

Mtoto wa k**e anapolazimishwa kuolewa mapema:
- Ananyimwa haki ya elimu,
- Anaumizwa kisaikolojia na kijamii,
- Jamii inapoteza mchango muhimu wa kesho.
- Tukatae mila na desturi zinazodhuru watoto wetu.

Simama nasi kulinda sauti na ndoto za mabinti zetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko!





17/09/2025

Arusha : Wahandisi kutoka Wizara na Taasisi zinazojihusisha na usimamizi wa miradi ya usafirishji hususani ile ya miundombinu wapo Mkoani A...

17/09/2025

Na MARY GWERA, Mahak**a-Dodoma Jaji Mkuu wa Mahak**a ya Tanzania, Mhe. George Masaju ametoa rai kwa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (...

WANAWAKE NA WASICHANA WATAJWA KUATHIRIKA ZAIDI NA NISHATI ISIYO SAFI YA KUPIKIARipoti mbalimbali zinaonesha kuwa wanawak...
16/09/2025

WANAWAKE NA WASICHANA WATAJWA KUATHIRIKA ZAIDI NA NISHATI ISIYO SAFI YA KUPIKIA

Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa wanawake, wasichana na watoto ni kundi linaloathirika pakubwa na matumizi ya nishati isiyo Safi ya Kupikia ya kuni na mkaa ambapo moshi unaotokana na matumizi ya nishati hizo huwa na gesi zenye sumu pamoja na chembechembe ndogo za vumbi zenye viambato vya sumu ambazo huweza kudhoofisha mfumo wa upumuaji na kusababisha magonjwa mbalimbali kwa binadamu.

Takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 zinaonesha kuwa ni asilimia 16 tu ya watanzania ndio wanatumia nishati safi ya kupikia, hivyo bado kuna magonjwa yanayotokana na moshi wa kuni na mkaa ambayo yanasababisha vifo vya zaidi ya watu 33,000 kwa mwaka nchini

Wanawake, wasichana na watoto hasa wa maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na wanaoishi katika mkoa wa Mara wanatajwa kuathirika zaidi na nishati isyosafi ya kupikia kutokana na wanawake na wasichana ndio wahusika wakubwa katika kupikia familia huku baadhi yao wakiwa wanapika huwa aidha wmewabeba watoto mgongoni au watoto wanakua karibu na mama au walezi wao jikoni wakisubiri chakula hali inayopelekea na wao kuathirika na nishati hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) inaeleza kuwa moshi unaotokana na matumizi ya nishati isiyo safi huwa na gesi zenye sumu pamoja na chembechembe ndogo za vumbi zenye viambato vya sumu ambazo huweza kudhoofisha mfumo wa upumuaji na kusababisha magonjwa sugu k**a kikohozi, homa ya mapafu, kifua kikuu, pumu na saratani ya mapafu. Vilevile, sumu hizo husababisha kuharibika kwa ujauzito, kujifungua kabla ya wakati au kujifungua watoto wenye matatizo ya kiafya.

Magonjwa mengine yanayohusishwa na sumu hizo ni pamoja na magonjwa ya moyo na macho, shinikizo la damu na kupooza. Waathirika wakubwa wa matatizo haya ya kiafya ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na wanawake ambao hutumia muda mwingi jikoni kuandaa chakula. Vilevile, ubebaji wa mizigo mikubwa ya kuni migongoni au vichwani huathiri uti wa mgongo, kichwa na miguu ya wanawake na watoto.

Athari hizi za kiafya husababisha kuelemewa kwa mifumo ya afya kutokana na magonjwa ambayo yangeweza kuepukika k**a nishati safi za kupikia zingetumika. Inakadiriwa kuwa takribani watu 33,024 hufariki kwa Mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa upumuaji yanayosababishwa na uchafuzi wa hewa katika makazi.

Mkakati huo pia unaeleza kuwa katika jitihada za kutafuta kuni, wanawake na watoto hukumbwa na matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa kutokana na kwenda kutafuta kuni maeneo ya mbali na makazi ya watu ambayo ni hatarishi. Sambamba na hilo, wanawake wengi hukumbwa na kadhia ya kupigwa na waume zao kutokana na kutumia muda mrefu kutafuta kuni hivyo kuchelewa kurudi nyumbani, jambo linalohatarisha maisha, ustawi wa ndoa na familia.

Chanzo: Mkakati wa taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia (2024-2034)

✍️Imeandikwa na Emmanuel Chibasa

16/09/2025

Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa wanawake, wasichana na watoto ni kundi linaloathirika pakubwa na matumizi ya nishati isiyo Safi ya Kupikia...

16/09/2025

Mbeya : Mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TACTIC) unatekeleza miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 51 katika halmashauri ya jiji la Mb...

Wekeza nyumbani, jenga taifa letu. Kupitia TISEZA, Mtanzania anapata nafasi ya kuchangia katika ustawi wa taifa kwa furs...
16/09/2025

Wekeza nyumbani, jenga taifa letu.

Kupitia TISEZA, Mtanzania anapata nafasi ya kuchangia katika ustawi wa taifa kwa fursa salama na endelevu za uwekezaji.

Tukichagua kuwekeza kwenye nchi yetu tunachagua kuimarisha uchumi, kuongeza ajira, na kujenga misingi imara ya maendeleo ya taifa letu. Jiunge nasi katika safari ya kuwekeza kwa ajili ya kesho bora ya Tanzania.

Chanzo: TIC

15/09/2025

Na Angela Sebastian Biharamulo : Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema kutokana na kampeni ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya K...

15/09/2025

Na Ghati Msamba Mara : Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amempokea Waziri wa Maji wa Kenya, Mhandisi Eric Mugaa pamoja na viongozi ...

15/09/2025

Musoma: Mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Christina Ndengo, amewaomba wananchi wa jimbo hilo wa...

15/09/2025

Na Angela Sebastian Biharamulo: Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi amewataka mkuu wa mkoa wa Kagera,wakuu wa Wilaya na wak...

14/09/2025

Na Angela Sebastian Ngara: Kikundi cha vijana wapatao nane wa Kata ya Kabanga Wilayani Ngara mkoani Kagera ambao wamejiunga pamoja na kuanz...

Address

Kawawa Street
Musoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Musoma Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Musoma Tv:

Share