Dr Nila

Dr Nila Daktari wa kinywa na meno anayejitolea kuelimisha, kutibu, na kuimarisha afya ya kinywa na meno kwa jamii. Kila tabasamu lina thamani! Every smile matters.)

(Dentist dedicated to educating, treating & restoring oral wellness.

🦷 Harufu Mbaya ya Kinywani, Fizi Kuvimba, na Meno lulegea?Yote huanza na usafi wa kinywa usio sahihi...πŸ” CHANZO:– Kutopi...
31/07/2025

🦷 Harufu Mbaya ya Kinywani, Fizi Kuvimba, na Meno lulegea?
Yote huanza na usafi wa kinywa usio sahihi...

πŸ” CHANZO:
– Kutopiga mswaki mara 2 kwa siku
– Kutopiga mswaki kwa usahihi (sehemu zote za kinywa)
– Plaque (uchafu) kujikusanya na kuharibu fizi
– Kuachwa kwa uchafu kwa muda mrefu husababisha harufu mbaya, fizi kuvimba na meno kulegea

βœ… KINGA:
βœ”οΈ Piga mswaki mara 2 kila siku – asubuhi na usiku
βœ”οΈ Tumia dawa ya meno yenye madini ya floridi
βœ”οΈ Tumia nyuzi za meno (dental floss) Kwa Daktari wa kinywa na meno
βœ”οΈ Nenda kwa daktari wa meno angalau mara 2 kwa mwaka Kwa ajili ya uchunguzi na ushauri

πŸ’‰ MATIBABU:
πŸ”Έ Usafi wa kina (scaling & polishing)
πŸ”Έ Dawa za kuondoa maambukizi
πŸ”Έ Matibabu ya fizi au upasuaji kwa hali mbaya

πŸ“Usisubiri harufu ikue na meno kulegea β€” chukua hatua mapema!
Fika kwa uchunguzi wa kitaalamu:
Sibaba Dental Clinic – Musoma
Tarime SDA Dispensary – Tarime Mjini
πŸ“ž 0787 412 236

πŸ“’ Huduma bora ya uzazi wa mpango kwa wanawake wote – BURE kabisaa!πŸ‘©β€πŸ‘§β€πŸ‘¦ Unapochagua uzazi wa mpango, unachagua afya, uhu...
27/07/2025

πŸ“’ Huduma bora ya uzazi wa mpango kwa wanawake wote – BURE kabisaa!

πŸ‘©β€πŸ‘§β€πŸ‘¦ Unapochagua uzazi wa mpango, unachagua afya, uhuru na furaha kwa familia yako!
🦷 Na sasa kuna zawadi ya kipekee! Kila atakayefika atapatiwa UCHUNGUZI WA MENO – BURE KABISAA!

🩺 Zahanati ya Tarime SDA inakualika siku ya Jumanne – Tarehe 29, kwa huduma kamili na BURE za uzazi wa mpango:

1. Kitanzi – Salama na hudumu kwa miaka mingi

2. Sindano ya Majira – Rahisi na ya muda mfupi

3. Kipandikizi (Implant) – Kwa kinga ya muda mrefu

4. Kalenda – Kwa walio tayari kujifunza na kufuatilia

5. Vidonge vya majira – Kwa udhibiti wa kila siku

6. Condom – Kinga dhidi ya mimba na magonjwa ya ngono – BURE KABISAA!

🦷 Na si hayo tu – kila atakayefika atapatiwa uchunguzi wa meno bure kabisa!

πŸ•— Huduma zinaanza saa 2:00 asubuhi

πŸ“ Mahali: Zahanati ya Tarime SDA

πŸ‘£ USIKOSE!

Jitokeze mapema – pata huduma bora ya afya ya uzazi na meno kwa wakati mmoja – BILA MALIPO.

Tunapatikana Tarime Mjini – Mtaa wa Anglikana (Winani ya zamani).

Au tupigie moja kwa moja kwa haraka zaidi:
πŸ“žMapokezi: 0695 569 410
πŸ“ž Dkt. Furaha 0744 501 761
πŸ“ž Dkt. Nila: 0787 412 236

🧠 90% YA SABABU ZA MENO KUBEBANANA KWA MTOTO ZINAANZA NYUMBANI – ZUIA KABLA HAUJACHELEWA!1. Kung’olewa mapema kwa meno y...
25/07/2025

🧠 90% YA SABABU ZA MENO KUBEBANANA KWA MTOTO ZINAANZA NYUMBANI – ZUIA KABLA HAUJACHELEWA!

1. Kung’olewa mapema kwa meno ya utotoni
➑️ Mara nyingi hutokana na kuoza kwa meno (Early Childhood Caries)
➑️ Kuacha nafasi wazi kwa muda mrefu huchangia udumavu wa taya
➑️ Taya inakua ndogo kuliko ukubwa na idadi ya meno ya ukubwani β†’ meno yanabanana

2. Tabia zisizofaa mdomoni. Kunyonya kidole, kalamu, kuuma midomo, kutumia chuchu ya chupa kwa muda mrefu. Huzuia ukuaji wa kawaida wa taya na kuathiri mpangilio wa meno

3. Kupumulia mdomoni muda mwingi. Huchangiwa na matatizo ya njia ya hewa k**a tonsis, mafua ya mara kwa mara au mzio
➑️ Mdomo unapobaki wazi muda mwingi β†’ taya inakua vibaya

4. Meno ya utotoni kuchelewa kung’oka. Meno ya ukubwani huanza kuota pembeni au nyumaβ†’ husababisha kubanana
5. Ajali au maambukizi ya taya wakati meno yanakua. Huathiri ukuaji wa kawaida wa taya

6. Kurithi taya ndogo

πŸ“Muone daktari wa meno mapema. Kinga ni rahisi na nafuu kuliko tiba.

πŸ‘¨β€βš•οΈ Dkt. Nila
πŸ“ž 0787 412 236

Hongera kwa followers wangu wapya! Nimefurahi sana kuwa na ninyi kwenye safari hii! Karibuni sana!! Francis Benjamin Mat...
23/07/2025

Hongera kwa followers wangu wapya! Nimefurahi sana kuwa na ninyi kwenye safari hii! Karibuni sana!

! Francis Benjamin Matondo, Jenipher Dibogo, Godfrey S Mwanakatwe, Liz Molly, Sesaria Lusingu, Rey Joseph Silayo, Hamis Hamis, Khadija Ngezi, Raymond Magnus, Hedwiga Temba, Jambo Jm, Pendo Mafie, Stanyford Emanuel, Dk Halidi Haji Mruma, Bernadetha M***a, Salvatory Ruhasha, Sahani Paul, Amina Mohamed, Anyes Malimao, Paulo Miliari Molleltz, Mohammed Abdallah

πŸ”΅ Dalili zimeanza? Jitokeze mapema – Tupo hapa kwa ajili yako!πŸ€’ Unajisikia mwili kuchoka muda wote hata baada ya kupumzi...
21/07/2025

πŸ”΅ Dalili zimeanza? Jitokeze mapema – Tupo hapa kwa ajili yako!

πŸ€’ Unajisikia mwili kuchoka muda wote hata baada ya kupumzika?
Inawezekana ni dalili ya Brucellosis (Brusella)

🚨 Vipi kuhusu PID (Pelvic Inflammatory Disease)?
Husababisha maumivu ya tumbo ya mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni, mzunguko wa hedhi isioeleweka na huathiri uwezo wa kupata ujauzito salama.

😷 Harufu mbaya kinywani hata baada ya mswaki?
🦷 Meno ya mtoto yamebebana au yameanza kuoza, kulegea na kuuma?
Usisubiri madhara – chukua hatua sasa!

πŸ₯ Zahanati ya SDA TARIME inakukaribisha kwa huduma zote chini ya paa moja – masaa 24, siku zote!

βœ… Huduma za baba, mama na mtoto
βœ… Matibabu ya kinywa na meno – kusafisha, kuziba, kung’oa
βœ… Chanjo na huduma za RCH
βœ… Ultrasound & Maabara
βœ… Famasi (duka la dawa)
βœ… Huduma za kujifungua
…na zaidi!

πŸ“ Tarime Mjini – Mtaa wa Anglikana (Winani ya zamani)
πŸ“ž Dkt. Nila: 0787412236
πŸ“ž Mapokezi: 0695569410

πŸ‘‰ Jali afya yako na ya familia yako – tembelea Zahanati yetu leo!

18/07/2025
πŸ”΅ *"Chini ya paa moja – Huduma nyingi karibu yako, masaa 24!"**Zahanati ya SDA Tarime* inatoa huduma bora na rafiki za a...
18/07/2025

πŸ”΅ *"Chini ya paa moja – Huduma nyingi karibu yako, masaa 24!"*

*Zahanati ya SDA Tarime* inatoa huduma bora na rafiki za afya kwa wote, zikiwemo:
πŸ‘©β€πŸ‘¦ Kliniki ya baba, mama na mtoto
🦷 Tiba ya kinywa na meno
πŸ§ͺ Huduma za maabara
πŸ’Š Famasi (duka la dawa)
πŸ–₯️ Vipimo vya atrasaundi

πŸ“ *Tunapatikana Tarime Mjini, mtaa wa Anglikana – mahali palipokuwa Winani ya zamani.*

Kwa msaada au miadi:
πŸ“ž Dkt. Nila – 0787 412 236
πŸ“ž Mapokezi – 0695 569 410

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Latens Wella, Damas JD, Richard Lucas Njau, Charles Masha...
15/07/2025

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Latens Wella, Damas JD, Richard Lucas Njau, Charles Masha, Simon Badehe Madatula, Phillip Raphael Makoye, Jsh Clinch Mosha, Damian Bernard, Joackim Jomamu Musaye, Enock Isack, Anna Paul Mduma, Mudy Johari, Gervas Zacharia, John Elias Sule, Sam Safari, Lameck Ally, William Ngamba, Shuu Mohamed, Richard Batroba, Sipriane Faraay, Samson Mwita, Ït's Rancoh, Jeanny Love, Hellen John, Paskalia Sinda, Jeremiah Lima, Godleonard Mponzi, Leshawo Molly, Linah Swai

🦷 Mzazi, Je Hili Limekutokea?Mtoto wako ana miaka 5–7 na ghafla unaona meno mapya (ya kudumu) yameanza kuota kabla ya ya...
14/07/2025

🦷 Mzazi, Je Hili Limekutokea?

Mtoto wako ana miaka 5–7 na ghafla unaona meno mapya (ya kudumu) yameanza kuota kabla ya yale ya utotoni (ya maziwa) kung’oka?

‼️ Usishtuke! Hii hali huitwa lingual eruption na si ugonjwa wala mkosi.

Ni hali ya kawaida kwa watoto wengi – hasa meno ya mbele ya chini (mandibular incisors). Huwatokea watoto wengi na mara nyingi hujirekebisha yenyewe bila matibabu.

βœ… Nini cha Kufanya?

πŸ”Ή Mruhusu mtoto atikise meno ya utotoni kwa upole kila siku
πŸ”Ή Epuka kumpeleka kung’olewa bila ushauri wa daktari
πŸ”Ή K**a jino la utotoni halijatoka ndani ya wiki 2–4, fika kliniki ya meno kwa uchunguzi
πŸ”Ή Hakikisha mtoto anasafisha kinywa vizuri ili kuepuka kuharibika kwa jino jipya

πŸ“£ Chukua sekunde 5 kusambaza ujumbe huu β€” unaweza kuokoa jino la mtoto mmoja, au kupunguza hofu ya mzazi mmoja.

πŸ“ Musoma na Tarime
πŸ‘©β€βš•οΈ Dkt. Nila Jackson
πŸ“ž 0787 412 236
’oa

🦷 "Mdudu wa jino umehamia jino jingine!" – Alisikika mgonjwa akihojiNi kauli iliyozoeleka kutoka kwa wagonjwa Wengi huam...
10/07/2025

🦷 "Mdudu wa jino umehamia jino jingine!" – Alisikika mgonjwa akihoji

Ni kauli iliyozoeleka kutoka kwa wagonjwa

Wengi huamini kuwa maumivu ya jino ni ishara ya mdudu kuhamia jino jingine baada ya kung’oa.
Hii ni imani potofu inayopelekea watu kuahirisha matibabu na kuendelea kuishi na maumivu.

βœ… Ukweli ni kwamba

Maumivu ya jino si ishara ya mdudu kuhamia, bali:

πŸ”Έ Meno yanaweza kuoza kwa muda mrefu bila maumivu
πŸ”Έ Bakteria waliopo kinywani hutumia mabaki ya sukari kuzalisha tindikali inayotoboa meno
πŸ”Έ Mara nyingi, wakati unaling’oa jino moja, kuna jingine lililotoboka lakini halijaanza kuuma
πŸ”Έ Ndiyo maana baada ya muda, jino jingine linaanza kuuma – si kwamba mdudu amehamia, bali tatizo lilikuwepo kabla

🦷 Suluhisho ni nini?

1. Piga mswaki mara mbili kwa siku kwa dawa ya meno yenye madini ya floraid

2. Fanya uchunguzi wa meno angalau mara mbili kwa mwaka (Check Up x2)

3. Tibu jino mapema kabla halijaanza kuuma

4. Tumia huduma salama k**a:

Kuziba jino (filling)

Matibabu ya mizizi (root canal)

Usafi wa fizi (scaling)

🀝 Tunakuomba usiishie tu kujifunza β€”

πŸ‘‰ Shiriki ujumbe huu na waalike wengine!

πŸ“£ Jiunge nasi kwenye WhatsApp Channel ya

β€œAfya ya Kinywa na Meno kwa Jamii”

βœ… Masomo mafupi, ya lugha rahisi
βœ… Yamebeba ujumbe wa kubadilisha maisha
βœ… Yameandaliwa kwa kushirikishwa kwa jamii, ndugu na marafiki

πŸ‘‰ Bofya hapa kujiunga:
[https://whatsapp.com/channel/0029VbAtKzOBlHpeq9jtlP3m]

πŸ“Œ Elimu huondoa hofu. Uelewa huzuia kung’oa ovyo.

Dkt. Nila Jackson
0787412236

Address

Uhuru
Musoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr Nila posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share