18/04/2024
NEEMA YA MUNGU IKO JUU YA KILA MTU, ILA ANAYEIFAIDI NI MWENYE BIDII NA JUHUDI...
Tuzungumze kidogo kuhusu neema; kwa lugha rahisi sana, neema ni upendeleo, kustahilishwa, unaweza kupata kitu usichostahili kwa kuwa tuu neema iko juu yako imekufunika... Kwenye neema sheria huwa haifuatwi...
Na Mwl Migongo E.N.D
Kwa wasomaji wa biblia wanaweza tofautisha enzi za agano la kale, sheria ilifuatwa, ilikuwa ukitenda dhambi ni pale pale, unawakumbuka enzi za Nuhu, Sodoma na gomora, ni baadhi ya mifano michache ya hasira ya Mungu kwa watenda dhambi...
Unakumbuka hata hadithi ya Anania na mkewe Safira, walipodanganya kuhusu sadaka, waliposemeshwa kuhusu uongo wao wakaanguka wakafa?
Sasa ili uelewe kwamba neema inafanyaje kazi, jiulize mara ngapi umefanya k**a Anania, au yale ya sodoma na gomora, siku hizi si mpaka wanadai haki mahak**ani na wapo hadi makanisani na wengine wanaongoza...
Hiyo ndio nguvu ya neema si k**a Mungu haelewi, au haoni, hapana anaheshimu kanuni za ulimwengu wa roho, hasa baada ya kuiachilia damu ya Yesu ili itukinge na hasira zake pale tunapomkosea... Maana Yesu alitolewa ili awe upatanisho kwaajili yetu na Mungu, kazi zingine tunaitumia tu kwa umakini na kwa kibali na lazime uwe makini tofauti na hapo mmmhhh (kasome maandiko)
SASA ni hivi neema pamoja na kuw aimeachiliwa, ila inahitaji juhudi ili kuifurahia hiyo neema, ukizembea inakupita na utapoteza kila kitu kilichokusudiwa...
Usipoonesha bidii / juhudi hata Mungu hatakuwa na furaha nawe, wacha tutazame mfano huu wa kuzaliwa kwa PERESI na ZERA, hawa walikuwa mapacha, na saa ya kuzaliwa Zera, alipata neema ya kutokeza wa kwanza, maana yake huyu ndiye Kulwa, na Peresi alipaswa awe Doto...
Kilichotokea ni uzembe wa Zera kutoka tumboni mwa Tamari maana tayari aliwekwa na alama ya uzaliwa wa kwanza; Peresi akaona wacha atie bidii (nguvu) huenda mambo yakabadilika, na kweli akafanikiwa... SOMA kitabu cha Mwanzo 38... au wacha nikusaidie hapa...
Mwanzo 38 27 Wakati wa kujifungua kwake Tamari ulipofika, ikafahamika kuwa alikuwa na mimba ya mapacha. 28Basi, alipopata uchungu wa kuzaa pacha mmojawapo alitoa mkono nje, naye mkunga akaufunga kwa u*i mwekundu, akisema, “Huyu ndiye aliyezaliwa kwanza.” 29 Lakini huyo mtoto alipourudisha mkono wake ndani, ndugu yake akazaliwa wa kwanza. Mkunga akasema, “Mbona wewe umepita kwa nguvu?” Kwa hiyo akaitwa Peresi. 30Baadaye ndugu yake akazaliwa akiwa na ule u*i mwekundu mkononi, naye akaitwa Zera...
Sasa tazama madhara ya uzembe wa Zera ulivyomgharimu, thamani yake mbele za Mungu ikapotea, yaani kwa uzembe tuu wa kutoka saa ya kuzaliwa, thamani yake ikawa sifuri kuliko hata ya Rahabu yule kahaba, (kasome maandiko)...
Inapokuja suala la Yesu kuja duniani, unamuona Rahabu (kahaba mstaafu) na humuoni Zera, ila unamuona mzee wa spidi Peresi... Soma kitabu cha ukoo wa Yesu, kwa mtumishi Mathayo
Mathayo 1: 1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. 2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; 3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; 4 Aramu akamzaa Aminadabu 5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;
Hapo Zera kaishia kuoneshwa tuu alizaliwa, na bila shaka alizaa, ila nani anajali kusimulia habari za zake, kuna pahala aliyumba kuitumia neema, ila mkak**avu Peresi na kahaba Rahabu; NEEMA INATUHITAJI BIDII NA JUHUDI ILI KUFAIDIKA NA MEMA YANAYOAMBATANA NA NEEMA ILIYO JUU YETU...
Angalia usije laghaika na neema unayoiona juu yako, na ukabaki kutazama wengine ambao hawana neema hiyo kwa sasa, mwisho wa siku utawaona mahala ambapo utaishia tuu huyu kafikaje hapo, au ndio kuanza kujihesabia idadi ya uliowaombea wakapona wakati jirani yako anafanya ukahaba, au anasinzia kanisani saa ya ibada.
Migongo End