16/01/2023
BODY CREAM YA LIMAO
MUHIMU KUZINGATIA USAFI.
Unatakiwa uwe na
- nta ya nyuki 50grams (beeswax) unaweza kuulizia kwa wale wanaouza asali au hata Instagram wapo watu kibao wanauza.
-shea butter 30grams
-mafuta ya n**i nusu kikombe
-mafuta ya mzaituni (olive oil) nusu kikombe
-malimao makubwa mawili
Anza kwa kukwangua maganda ya limao kwa kutumia grater (kile cha kukwangulia karoti au nyanya)
Ukishakwangua weka kwenye bakuli la udongo alafu mimina humo mafuta ya n**i, changanya vizuri
Chukua sufuria weka maji bandika jikoni, chukua lile bakuli uliloweka maganda ya limao pamoja na mafuta ya n**i weka juu ya sufuria hilo, fanya k**a unafunikia hapo yani liingie nusu kwenye sufuria, nusu liwe linagusa maji ya kwenye sufuria kwa hiyo maji yanavyochemka ndani ya sufuria na huku mchanganyiko unapata moto kupitia maji ya kwenye sufuria.
Mchanganyiko ukishapata moto humo weka beeswax, shea butter na olive oil.. Acha mpaka shea butter na beeswax viyeyuke kisha ipua.
Chuja kwa kutumia kitambaa cha shifon kisha weka kwenye bakuli safi.. Acha kwa dakika 20 ikianza kuganda chukua hand mixer au mchapo anza kumix... Mix mpaka iwe kitu kimoja, laini na nzito.. Body cream yako tayari.
[email protected]