Kihahi Tv

Kihahi Tv ■KIHAHI TV ONLINE 📺
| Enter | Sports | Gospel | Trends |News
| Funny | Home Of Updates | Call us

|● +225626248355●|

Mahak**a ya Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga, Julai 17, 2025 imemhukumu Sadi  Mtangi, mkazi wa Maramba, kifungo cha miaka ...
17/07/2025

Mahak**a ya Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga, Julai 17, 2025 imemhukumu Sadi Mtangi, mkazi wa Maramba, kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya kubaka wanafunzi wawili wa k**e wenye umri wa miaka 13 na 9.

Awali, ilielezwa mahak**ani kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 11 Agosti 2024 dhidi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maramba na Shule ya Msingi Mapatano, wote wakazi wa Maramba.

Akisoma hukumu hiyo, Mheshimiwa Hakimu Deda alisema kuwa mahak**a imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kumhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kila kosa, adhabu itakayotekelezwa mfululizo.
King Kihahi

Kuna harufu ya mvutano mkubwa kwenye anga la soka Tanzania! Klabu ya Simba SC inadaiwa kuwa kwenye harakati za chini kwa...
05/07/2025

Kuna harufu ya mvutano mkubwa kwenye anga la soka Tanzania! Klabu ya Simba SC inadaiwa kuwa kwenye harakati za chini kwa chini kuhakikisha inamnasa kiungo hatari wa Yanga SC, Pacome Zouzoua! 😳🦁

Zouzoua, raia wa Ivory Coast, amekuwa mhimili mkubwa wa mafanikio ya Yanga tangu alipojiunga Julai 2023. Uwezo wake wa kutoa pasi za mwisho, kufunga mabao na kutawala eneo la kiungo umeifanya Simba kuonesha nia ya dhati ya kumvuta Msimbazi! 🚨⚽

Iwapo dili hili litakamilika, Simba SC watakuwa wamefanya usajili wa kishindo na kuwatoa jasho watani wao wa jadi – Yanga SC! 💣

📣 Je, unadhani Zouzoua atavuka mto na kujiunga na Simba?

Ukihitaji Tukutengezee matangazo Quality kwa mfumo wa audio na video
weka oda yako leo.
Message Dr Kihahi on WhatsApp. https://wa.me/255626248355

🚨 GOOD NEWS: Klabu ya Liverpool imeweka wazi kwamba itaendelea kuilipa mshahara Familia ya Marehemu Diogo Jota mpaka pal...
05/07/2025

🚨 GOOD NEWS: Klabu ya Liverpool imeweka wazi kwamba itaendelea kuilipa mshahara Familia ya Marehemu Diogo Jota mpaka pale Mkataba wake wa miaka miwili uliobakia kwenye Mkataba wake na Liverpool❤️
Jota ambaye alifariki wiki hii alikuwa analipwa kiasi cha Shilingi Milioni 370 kwa wiki.
Pumnzika kwa amani, DIOGO 🕯️🕊️
Kwa mahitaji ya huduma ya kutengeneza matangazo Quality kwa mfumo wa Audio na Video gusa link hii uweke oda yako.
https://wa.me/255626248355

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na Timu ya Taifa ya Ureno, Diogo Jota amefariki Dunia pamoja na kaka yake kwenye ajal...
03/07/2025

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na Timu ya Taifa ya Ureno, Diogo Jota amefariki Dunia pamoja na kaka yake kwenye ajali ya barabarani iliyotokea mjini Zamora, Uhispania wakati wawili hao wakiwa safarini kuelekea England.

Jota mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisafiri pamoja na kaka yake Andre ambaye pia ni mwanasoka wamepoteza maisha katika mji wa Zamora uliopo Kaskazini-Magharibi mwa Uhispania.

Jota ambaye amepoteza maisha siku 10 tu tangu afunge ndoa na mpenzi wake Rute Cardoso mnamo Juni 22, 2025 huku akiacha watoto watatu.

Nyota huyo wa zamani wa Wolverhampton amehudumu Liverpool kwa miaka mitano akiichezea timu hiyo mechi 123 na kufunga magoli 47. Pia ameichezea Ureno mechi 49 na kuifungia magoli 14.



Follow Kihahi Tv
Follow King Kihahi

02/07/2025

Ongeza ushawishi wa Huduma zako kwa Wateja kupitia matangazo Quality ya kibiashara Kwa Mfumo wa Audio na Video kwa Bei nafuu, Iwe ni..>kwa.
👇👇👇👇👇👇
●Mfanyabiashara.
●Taasisi binafsi.
●Mashirika ya uma.
●Mashirika Binafsi Na Makampuni Mbalimbali tutakusaidia kujitangaza vyema kwa wateja wako▪︎

■Pia Tunatengeneza [LOGO] na [POSTERS]
Kwa Bei Nafuu Sana.

■TUPE KAZI TAJIRI NA WEKA ODA YAKO KUPITIA NAMBA HAPO CHINI.
Wasiliana nasi kwa namba hizi (Whatsapp&Calls)
☎️ https://wa.me/255626248355

KIKAO CHA WANAUME HII INATUHUSU WANAUME WOTE KUITAFAKALI.   ...........................................
02/07/2025

KIKAO CHA WANAUME HII INATUHUSU WANAUME WOTE KUITAFAKALI.
...........................................

RC KIHONGOSI AKABIDHIWA OFISI NA PAUL CHRISTIAN MAKONDA. Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha, Mhe.Kenan Laban Kihongosi  amekabi...
30/06/2025

RC KIHONGOSI AKABIDHIWA OFISI NA PAUL CHRISTIAN MAKONDA.

Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha, Mhe.Kenan Laban Kihongosi amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ndugu Paul Makonda na kuanza kazi rasmi na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama na Serikali, watumishi wa Umma, viongozi wa dini, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo rasmi mapema leo mapema leo Juni 30, 2025.

Hafla hiyo ilianza kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu na shughuli za utekelezaji wa mkoa huo huku akieleza mafanikio yaliyopatikana kisekta kwa kipindi chote alichohudumu.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu mpya wa Mkoa Mhe. Kihongosi, amemshukuru Mwenyenzi Mungu kupitia Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa imani yake kubwa na kumpa dhamana ya kuongoza Mkoa wa Arusha na kumshukuru Mtangulizi wake Ndugu Makonda kwa kazi kubwa aliyoifanya katika mkoa huo, kazi ambayo ameacha alama kubwa mkoani hapo.

“Mhe.Rais amenituma Arusha kuja kuwatumikia wananchi wa Arusha na nimekuja kufanya kazi, ninachoomba kwenu ni ushirikiano ili kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo, tukiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wa Arusha wanafurahia matunda ya nchi yao”. Ameweka wazi Mhe.Kihongosi

Aidha, amesisitiza ktoruhusu kikwazo chochote kitakachojaribu kuzuia agenda ya maendeleo katika utendajinkazi, wajibu wake ni kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiweo matumizi sahihi ya fedha za Umma zinazoletwa kwa ajaili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta zote.

Zaidi amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu kwa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wote, ili i kila mtua aweze kufurahia matunda ya Serikali na Nchi yake.

Awali Mhe.Kihongosi amehamishiwa mkoani Arusha akitokea Mkoa wa Simiyu na kuagizwa na Mhe. Rais kuja kuwaaunganisha wananchi wa mkoa wa Arusha.

Cc. ✍🏻 King Kihahi

Kiungo Mkongomani, Fabrice Luamba Ngoma amehitimisha miaka miwili ya utumishi wake ndani ya klabu ya Simba Sc baada ya k...
29/06/2025

Kiungo Mkongomani, Fabrice Luamba Ngoma amehitimisha miaka miwili ya utumishi wake ndani ya klabu ya Simba Sc baada ya kuiaga klabu hiyo kufuatia kutamatika kwa mkataba wake na Wekundu hao wa Msimbazi.

Ngoma (31) aliyejiunga na vigogo hao wa Mtaa wa Msimbazi mnamo Julai 14, 2023 ametangaza kuondoka klabuni hapo kupitia ukurasa wake wa mitandao wa kijamii leo Juni 29, 2025.

“Habari za asubuhi nyote. Nataka kuchukua wasaa huu kuwashukuru kila mmoja aliyefanya nijisikie nyumbani hapa Simba Sc. Namshukuru Try Again na Bosi Mo aliyenileta hapa misimu miwili iliyopita.”

“Nawashukuru Kocha, wafanyakazi na wachezaji ambao tumeshiriki chumba cha kubadilishia nguo pamoja. Hatukufikia baadhi ya malengo yetu lakini kumbukumbu zote zitasalia akilini na moyoni mwangu milele.”

“Kwa mashabiki wa Simba Sc ahsanteni kwa kwa sapoti yenu. Tusiiangushe klabu, nyakati nzuri zipo mbele hususani chini ya kocha k**a Fadlu. Ahsanteni sana nawatakia muendelezo mzuri.”— Ngoma

🕊TANZIA😭Muigizaji Dorcas Yahaya, maarufu k**a Wema wa Shilingi iliyokuwa ikiruka kupitia Azam TV, amefariki dunia Jana 💔...
29/06/2025

🕊TANZIA😭

Muigizaji Dorcas Yahaya, maarufu k**a Wema wa Shilingi iliyokuwa ikiruka kupitia Azam TV, amefariki dunia Jana 💔😭

Taarifa hizi ziltolewa jana rasmi na familia kupitia kwa Hashim Mbuzini, Mjumbe wa Chama cha Waigizaji Tanzania.

📍 Msiba umefanyika: Kimanga Bonde la Mchicha, karibu na Kanisa la KKT.

🕯️ Mazishi yamefanyika Leo jioni.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. 🕊️

Soko Ni Gumu,Nimerudi Shule😂….Hivi Jela Ni Miaka Mingapi?😅  dollzSmall Girl,Big God
29/06/2025

Soko Ni Gumu,Nimerudi Shule😂….Hivi Jela Ni Miaka Mingapi?😅 dollz
Small Girl,Big God

Ameandika Afisa Habari wa timu ya Simba  kupitia ukurasa wake wa   👇Nianze na pole kwa Wana Simba kumaliza msimu bila ub...
27/06/2025

Ameandika Afisa Habari wa timu ya Simba kupitia ukurasa wake wa 👇
Nianze na pole kwa Wana Simba kumaliza msimu bila ubingwa katika mashindano tuliyoshiriki hususan ligi kuu ya NBC

Kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamiii na makundi ya Watsup, nimeona maoni mengi yenye uchungu ndani yake

Wana Simba tuepuke presha za mitandaoni na presha za wanaotuaminisha tumefeli kupita kiasi

Ni kweli hatujapata ubingwa lakini sote ni mashahidi kuwa timu yetu imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na miaka ya nyuma na hilo ndio lilikua lengo letu kutengeneza timu ya ushindani.

Msimu huu tumefanikiwa kucheza Fainali ya CAF ambayo tumeshindwa kufanya hivyo kwa miaka 31

Msimu huu ubingwa wa ligi umeamuliwa na Dkk 45 za Kipindi cha pili cha mechi ya mwisho, wakati msimu uliopita tulipigania nafasi ya tatu

Points tulizofikisha msimu huu hatujawahi kufikisha kwa miaka minne iliyopita

Tulipotoka na tulipo ni tofauti sana, mwangaza wa mafanikio hauko mbali yetu

Si mara ya kwanza Simba kukaa miaka minne bila Ubingwa, tushakaa miaka mitano kutoka 2012 hadi 2017 lakini tulijipanga 2018 tukachukua kwa miaka Minne mfululizo.

Kupoteza mara 5 mfululizo dhidi ya Mtani kusitufanye tukajidharau

Madrid amepoteza El Classico nne dhidi Barcelona tena kwa vipigo vya vikali lakini katu huwezi kuwaona Madrid wanajitukana

Sio mfano wa kujivunia lakini lazima tukubali nyakati hizi hutokea kwenye mpira

Pamoja na ukubwa wote Manchester United wanaenda mwaka wa 13 bila Ubingwa, Sitaki kutoa mfano wa Arsenal

Mifano hii itupe taswira kuwa hatuko peke yetu kwenye mapito ya namna hii na hata hawa wanaocheka sasa yapo magumu waliyopitia

Ombi langu wangu Wana Simba, tuwape nafasi viongozi wetu wafanye tathmini na baada ya hapo watupe muongozo tunaendaje mbele kuipambania Simba yetu

Heshima yetu itarudi kwa kushik**ana na kusimama pamoja

Nguvu Moja!!!!!!!"

✍️ King Kihahi

Address

Misungwi
Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kihahi Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share