09/11/2025
Tambua Hili kuhusu mitandao
ya kijamii ambayo ni matokeo ya utafiti (Global social
media research)
uliofanywa duniani kote na kutolewa
januari 2023....... 1: Watu (zaidi ya) bilioni 4.76 sawa na 59% ya watu wote duniani hutumia mitandao ya kijamii.....Hii inatoa tafsiri kwamba zaidi ya nusu ya watu wote duniani wanatumia mitandao ya kijamii...
Hii ni kusema kwamba k**a unataka kukutana na watu wa ulimwengu wa leo, njia rahisi ya kukutana nao ni kupitia
mitandao.
“K**a unataka kukutana na watu wa
ulimwengu wa leo, njia rahisi ya kukutana
nao ni kupitia mitandao.”
2: Watu zaidi ya 4 hujiunga na mitandao ya
kijamii kwa kila sekunde..
Hii bado ikusaidie kufahamu kuwa k**a kuna eneo la kukutana na watu kwa urahisi basi ni katika mitandao ya kijamii....
Mitandao si kitu cha kawaida k**a unavyoidhania, Katika mitandao ndiko uliko ulimwengu wa kileo
3: Kwa wastani mtu hutumia masaa 2 na dakika 31 kwa siku katika mitandao ya kijamii...
Hii ni kwa mtu wa kawaida …. (jaribu kufikiri) …...Hii inamaanisha kwamba k**a utawekeza nguvu zako
kufanya mambo yenye tija kupitia mitandao ya kijamii,.... basi
utakuwa na nafasi ya kukutana na kila mtu kwa angalau masaa 2 na nusu kila siku
Mpaka hapa bila shaka unatambua nguvu ya mitandao ya kijamii. .
Hii ndiyo sababu Chris Young alisema;
“Mitandao ya kijamii ni nyenzo zenye nguvu
sana"
Prepared BySirLuquman
Think deep deeper
.com@ Kelvin Kibenje