04/06/2026
Jamaa mmoja aliingia saluni akakuta Pana watu k**a watano na kinyozi wa sita.
Akauliza k**a kuna foleni kubwa akajibiwa kwamba wanao nyoa ni watatu tu yaani aliyekuwa ananyoa kwa muda ule na wengine wawili waliokuwa wameketi kwenye sofa, hawa wawili wengine walikuwa washkaji zake kinyozi wanapiga tu story.
Basi yule aliyeuliza akashukuru huku akitoka saluni na kuelekea duka la madawa jirani na kisha kutokomea .
Baada ya wiki moja jamaa yule yule akarudi tena saluni na kukuta watu wengi wengi tu wakingoja kunyoa akauliza tena vipi foleni kubwa akajibiwa siyo kiviile.
Akatoka akaingia duka la madawa na kisha kutokomea.
Jambo lile likaanza kumshangaza yule kinyozi kwamba kwanini yule jamaa anakuja kuulizia foleni lakini habaki wala kurudi kunyoa kwa muda mwingine.
Baada ya wiki yule jamaa akarejea tena akahoji kuhusu idadi ya wanao nyoa baada ya kujibiwa k**a ada akaingia duka la madawa na kutokomea.
Kwa kuwa wateja wa pale saluni mara nyingi ni wale wale na wemezoeana na kinyozi yaani ni wateja wazoefu ambao wana kawaida ya kujadili mambo mbalimbali basi kinyozi alipo lalamikia tabia ya yule jamaa ya kuja kuulizia foleni bila kunyoa.
Ndipo mteja mmoja akamjibu kinyozi akisema;- "mbona jamaa yule akisha ulizia foleni huingia duka la madawa kununua kondomu na kuelekea nyumbani kwako!?"