01/06/2026
"MO hawezi kuiacha Simba kwa sababu yupo kimkataba. Hawezi kuamka tu na kusema anaondoka na kuiacha Simba. Hilo suala halipo. Ukiangalia nyaraka za uwekezaji utaona wazi, wala si jambo la siri. Mfadhili anaweza kuamua kuondoka wakati wowote, lakini MO ni sehemu ya Simba. Nilisikia wengine wakisema wanampa saa kadhaa aondoke, jambo ambalo linaonyesha hawafahamu uhalisia wa suala hili"
CRESCENTIUS MAGORI, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC