Ushauri wa mapenzi na maisha

Ushauri wa mapenzi na maisha Forgiveness and letting go are steps on the road back to happiness. We invite you to join us and reclaim your happiness.

24/08/2026

Kunyamaza nalo ni jibu ,si vita vyote vinahitaji majibizano au majibu

22/08/2026

Muombe Mungu akupe afya njema kwanza, mengine utamuomba huko mbele...bila afya njema hawezi patafuraha ya kweli

20/08/2026

Asilimia zako 80%usizitumie kwenye kulalamika kila siku ,mambo hayawezi badilika kwa malalamiko bali amua kuchukua hatua 1 leo

18/08/2026

Unaishi kwa sababu na wala siyo bahati mbaya 💖 usikubali mtu akakudharau , kukudhalilisha na kukuona hufai🙏 bora kukaa nae mbali

18/08/2026

Jipende siku zote na jichague kwanza kabla mwingine hajaanza kukuchagua

12/08/2026

Ukiulizwa Swali hili utajibu nini?
Hivi kwa sasa unayaona wapi mahusiano yako?

11/08/2026

Huwezi kubadili ambayo yameshatokea lakini unaweza badili hali yako, kuliko kuendelea kulalamika dawa ni kuamka na kusonga mbele

Wakati mwingine maumivu makubwa hayaletwi na kuachwa, bali na kuendelea kung'ang'ania mtu ambaye tayari ameondoa nafasi ...
06/08/2026

Wakati mwingine maumivu makubwa hayaletwi na kuachwa, bali na kuendelea kung'ang'ania mtu ambaye tayari ameondoa nafasi yako moyoni mwake.

Usipoteze amani yako ukijaribu kumbadilisha mtu asiyeona thamani yako. Mapenzi ya kweli hayahitaji kulazimishwa; yanahitaji mioyo miwili inayochagua kupendana kila siku.

Na kuhusu maisha, usikate tamaa kwa sababu ya changamoto za leo. Kila hatua ngumu unayopitia inaweza kuwa daraja linalokupeleka kwenye mafanikio makubwa kesho.

Linda moyo wako, heshimu utu wako, na usiogope kuanza upya. Mara nyingi mwanzo mpya ndiyo huzalisha mwisho mzuri zaidi.

04/08/2026

Kila nyakati huja kutufundisha ziwe za heri au Shari ...Usiogope unapopatwa na nyakati za shida jua kuna heri iko njiani❣️

04/08/2026

K**a hawez kukupokea na kukukubali jinsi ulivyo haina haja ya kujibadilisha ili uwe jinsi anavyotaka yeye...utaishia kuishi vibaya

Address

Mwanza

Telephone

0678004608

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ushauri wa mapenzi na maisha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share