Ondoka Uangaze FB

Ondoka Uangaze FB KARIBU SANA TUTAJIKITA KATIKA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU, UJASIRIAMALI NA FAMILIA KWA UJUMLA MUNGU AKUBARIKI KWA USHIRIKIANO WAKO

30/04/2020

UNATAKA KUOLEWA? UMEJIPANGA?

Akina Dada Wanapenda Sana Kuolewa; Lakini Ni Wachache Sana Wanajua Namna Ya Kukaa MKAO WA KUOLEWA, Na Pia Namna Ya Kuchambua Kati Ya MWANAUME MUOAJI NA MWANAUME MUONJAJI!

Maua Yana Tabia Ya KUJIFUNGA, Lakini Yanajua Pia Muda Sahihi Wa KUCHANUA Na Kutoa HARUFU Inayowavutia NYUKI; Lakini Cha Ajabu Akina Dada Wa Digitali HAMJUI Haya, Mnazidiwa AKILI NA MAUA… Hii Ni Hatari Sana!

Ninapozungumzia Muda Wa UA KUCHANUA NA KUTOA HARUFU INAYOVUTIA NYUKI; Namaanisha Uwezo Wa Kutambua MAJIRA SAHIHI YA WEWE DADA KUOLEWA NA KUHAMA TOKA KWENYE KUNDI LA “MAUA YALIYOJIFUNGA” Yaani USICHANA Kuingia Kwenye Maua Yanayoingia Kwenye “UCHAVUSHAJI” Yaani Kuwa Mke, Mama Nakadhalika!

Nyuki Hawawezi Kuruka Kuja Kwenye UA LILILOJIFUNGA (Mdada Aliyekaa Mkao Wa KUTOONESHA DALILI ZA KUWA MKE), Bali Nyuki Huwa Wanaruka Kuelekea Kwenye MAUA YALIYOCHANUA NA YENYE HARUFU YA KUVUTIA!

K**a Dada, K**a Unaona Muda Wako Wa Kuolewa ULIOKUSUDIA Umekaribia, ANZA “KUCHANUA” Anza Kujenga Tabia Za Mke Na Si SISTA DUU Anayetafuta Mme.
Nyuki Wote Wanajua MAUA YALIYOCHANUA NA YENYE HARUFU NZURI; Vivyo Hivyo Kwa WANAUME WAOAJI, NAO WANAJUA BINTI GANI ANAFAA KUWA MKE!

Tabia Na Mfumo Wa Kuwa Mke HAUJENGWI NDANI YA NDOA; Unajengwa Ukiwa Bado Peke Yako, Unaanza KUPUNGUZA TABIA ZISIZOHITAJIKA KWENYE NDOA AMBAZO MABINTI WA KAWAIDA HUWA WANAKUWA NAZO.
Unaanza Kujenga Tabia Ya Kuwa Mama Mwenye Nyumba, Jifunze Kuwa Katika Namna Ya Mke Apaswavyo Kuwa.
Ukikaa Kwenye UHALISIA WA MKE ATAKIWAVYO KUWA; NYUKI WATAONA NA WATAKUJA, Halafu Wewe Ndiwe Utakayekuwa Na Kazi Ya KUCHAGUA YUPI KATI YAO NI MUOAJI NA YUPI KATI YAO NI MUONJAJI!

Kila Mwanadada Aliyekusudia Kuolewa Anaweza Kuolewa, Lakini Ni Lazima Uwe Na UFAHAMU WA KUTOSHA Kuhusu MKE Apaswavyokuwa Kabla Hauja-Attract Attention Ya Waoaji.

Mungu Awasaidie Akina Dada Wenye Nia Ya Dhati Ya Kuolewa Na Kuwa Na Miji Yenu!

19/04/2020

UJANA NI MAUA

NENO LA LEO: Ayubu 14:1-2
“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua k**a vile UA, kisha hukatwa; hukimbia k**a kivuli, wala hakai kamwe”
TAFAKARI:
Rafiki! Leo tunatafakari juu ya UA, wote tunajua kuwa UA LIKICHANUA KINACHOFUATA NI KUNYAUKA, na Jambo la kuvutia zaidi ni kuona linavyopendeza na kuvutia, mbali na wanadamu kupenda MAUA, hata wadudu pia utakuta wamejazana.
Maisha ya Mwanadamu ndivyo yalivyo, k**a UA linavyonyauka ghafla ndivyo maisha yanavyokatika, kumbuka sisi sote ni marehemu watarajiwa wasiojua muda wa kifo.
Vijana! Mwisho wa UA kuchanua ni kunyauka, wengi huutumia wakati huo vibaya, HAWATULII, Utakuta Binti mzuri eti anajirusha na Libaba ambalo halina Mpango wa kumuoa ili mradi ana Vijisenti – Hao ni WADUDU WAHARIBIFU. Tunaona baadhi ya MAUA yanavyoharibiwa na wadudu waharibifu, yanatobolewa na kuchafuliwa, ndivyo vijana WANAVYOPOTEZEWA DIRA YA MAISHA. Akili zikiwarudia na kutaka Kuolewa au kuoa wanajikuta wamechelewa – UMRI WA KUCHANUA UMEPITA, hata wakitumia MAKE UP, hazisaidii, wadudu wote wamekimbilia maua mengine yanayochanua.
Vijana! Habari za ku “PASS TIME” na vija wenzenu kwa maisha ya Ngono, Ulevi, Muziki n.k. yanawapotezea DIRA ya Maisha, tumeshuhudia wengi wanasukumwa na TAMAA, na Wengi wanatumika k**a VYOMBO vya kukidhi tama za wengine, mwisho wake ni kuachwa kwenye Mataa. MAISHA YOYOTE YA DHAMBI NI TANZI YA UHARIBIFU.
VIJANA WENGI WANAJUTIA KWA YALIYOPITA NA WENGINE NDIO WAMEZAMA.
SULUHISHO NI KUMTEGEMEA MUNGU – KWAKE YOTE YANAWEZEKANA

Address

Mapumulo

Telephone

+255758101996

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ondoka Uangaze FB posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ondoka Uangaze FB:

Share

Category