zinga_newsmedia

zinga_newsmedia News_Media ---------->Sports,Entertainment,Politics,lifestyle and more updates

Bei ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa imeshuka kwa mwezi octoba kulinganisha na mwezi septemba sababu zikita...
02/10/2024

Bei ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa imeshuka kwa mwezi octoba kulinganisha na mwezi septemba sababu zikitajwa ni pamoja na kushuka kwa gharama za soko la mafuta uarabuni.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi oktoba huku bei ya rejareja kwa bandari ya Dar es Salaam petrol ni tsh. 3011, dizeli ni tsh. 2846 na mafuta ta taa tsh. 2943 bandari ya Tanga petroli Tsh. 3,016. dizeli 2859 na mafuta ya taa 2989 huku bandari ya Mtwara petroli 3016, dizeli 2862 huku mafuta ya taa 3016.

Aidha bei ya kikomo ya mafuta rejareja kwa miji mbalimbali hapa nchini katika vituo vya mafuta Dar es salaam petrol itauzwa tsh. 3,011, dizeli tsh. 2,846, mafuta ya taa tsh 2,943 Arusha petoli itauzwa tsh. 3,073, dizeli tsh. 2,916, mafuta ya taa tsh. 3,027 huku kwa jiji la Dodoma petrol itauzwa tsh. 3,070 dizeli tsh. 2,905, na mafuta ya taa tsh. 3,002.

Address

Nyegezi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when zinga_newsmedia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share